Wadau na wazoefu naomba tuelezane. Mtoto mdogo wa ana umri wa miaka mitatu lakini huwa anampiga mama yake na wakati mwingine kumng'ata.
Mama yake akimkataza kitu anamfuata na kuanza mpiga au kumrushia kitu au kumuuma meno..
Nikirudi mm nyumbani kutoka miangaiko yangu hataki mtu amguse zaidi yangu..si kumlisha wala kumuogesha...
Wadau kuna mwenye uzoefu na Hili..nini inaweza kuwa reason...
Kwa mujibu wa utafiti wangu ninaoendela kuufanya nimegundua kuwa kuna tabia watoto wanakuwa nazo ambazo zinatokana na vile mtoto anavyolelewa tokea anazaliwa.
Wazazi wanajisahau kuwa mtoto akianza kuongea na kutembea hapo anakuwa sio amejifunza kuongea tu,sio amejifunza kuongea tu bali kajifunza pia namna gani ahandle pale anapoudhiwa na kugombwa jjuu ya jambo fulani.
Wazazi wengi wanadhani mtoto akijua kuongea na kutembea ati amejifunza mambo hayo tu.
No,kumbuka wakati anajjifunza kuonngea huku amezaliwa na mdomo kumbuka pia amezaliwa na macho yake ushawahi kujiuliza hayo macho tokea anazaliwa mpska anafikia kuongea na kutembea hayo macho kwake yana kazi gani ?
Kazi ya macho sio kujifunza kwa kusikia bali kazi ya macho ni kujifunza kwa kuona.
Kuna matukio mtoto anayaona na kuyasikia hivyo anajua kwamba tukio hili likitokea nifanye vipi baada ya kuwa ashaliona.
Jambo la ajabu zaidi ni kuwa namna unavyoishi na mtoto ndivyo naye atakua hivyo hivyo.
Kuna mtoto wa jirani yangu hanakaribia miaka miwili anatembea,anaongea vizuri tu huwa ni mkorofi korofi,siku moja nimekaa akanichapa na kitu ikaniuma nikamuangalia tu kwa hasira kisha nikaondoka pale nikamuhama,tokea siku hiyo kila nikimuona nampotezea mpaka akajua kuwa jamaa hataki ujinga sasa hivi kaacha ujinga wake wa kunipiga bila kutumia nguvu.
Watoto ni viumbe tunahitaji uweledi kuishi nao,usimuache mtoto atazame mambo ambayo wewe hupendi aje kuwa nayo baadae ni hatari.
Movie za kupigana,movie za mapenzi ni mbaya kwa mtoto kwa sababu mtoto ni mtu ambaye anatafuta matukio ili ayaishi hivyo liwe zuri ama baya yeye analidaka tu mradi baadae atakuja kulitumia katika kuishi kwake.
Leo mtoto wa mwaka miaka miwili hajui hili zuri au baya,hivyo ukimuona na baya mkemee kabla hajakuwa.