watu hulia kwa sababu mbalimbali kama maumivu,furaha au woga.
mtu akiwa na kidonda,alikia,kinachomliza si maumivu ya kidonda tu bali ni maumivu ya mawazo kuhusu hicho kidonda.mawazo hayo hupelekea kumwagwa kwa homoni ambazo husaidia kidonda kupona mfano Leucine enkephalin(natural painkiller) husaidia kupunguza maumivu.
homoni hizi zinatakiwa kuwa katika kiwango kinachohitajika hivyo basi zinapozidi ndio pale mtu analia anatoa machozi kabisa,machozi hutoka na hizo homoni.
mtu akiwa na stress,homoni ya Adrenocorticotrophic(ACTH) husababisha homoni ya Cortisol humwagwa kwenye damu,na ikizidi huleta matatizo ya kiafya, sasa ili hayo matatizo ya kiafya yasitokee inabidi hiyo ACTH ipunguzwe na hukoka kwa njia ya machozi(hapo utaona mtu analia). hiyo hufanya na kiasi cha cortisol kupungua.
pia kuna sumu nyingi,Endorphins ambazo hutolewa kwa machozi(machozi kutoka ndio mtu kulia).
wanawake hulia zaidi ya wanaume,wao wana homoni kama oestrogen na prolactin hizi huwafanya wawe wepesi kulia.
wanaume wana testosterone homoni zinazowafanya wawe wagumu kulia.kwa sababu ya ugumu huo, zile sumu ambazo zilitakiwa zitoke kwa machozi, hutolewa kwa njia ya jasho( ndio maana wanaume hutokwa sana jasho kuliko wanawake).
Ukiona mtu anacheka mpaka analia ni kwamba wakati anacheka tezi za machozi zimebonyea hivyo machozi yakatoka.
kisaikolojia kulia huonesha hisia za mtu kama kuchukia, kufurahi, na kupenda hasa mtu anapolia kwa ajili ya mtu mwingine.