Kwanini mtu anajiua kwa ajili ya mapenzi?

Typhoid

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
226
Reaction score
70
Mtu kujiua kwa ajili ya mapenzi sio jambo geni masikioni mwetu! Nimeamua kutuma huu uzi baada ya best friend wangu kujiua kisa gf wake amemsaliti!
Je kujiua kwa ajili ya kusalitiwa ktk mapenzi ni suruhisho?
Kwa maoni yangu naona kujiua eti kwa sababu mpenzi wako amekusaliti sio suruhisho kabisa!
Zifuatazo ni sababu anuai ambazo zaweza sababisha mtu kwenda ahera eti kisa mapenzi.
1. Wivu... Hapa huwa tunapatikana wote me/ke na yeyote anaweza kujiua kutokana na degree ya wivu
2. Mapenzi ya dhati: hapa wasichana wengi huwa wanajiua maana hujisikia vibaya wanaposalitiwa.
3. Stress za maisha. Hapa pia inaweza kumuathiri zaidi msichana kuliko mwanaume.
Wanajf kuna sababu mbalimbali ambazo husababisha wenzetu kuchukua maamuzi magumu ya kujiua! Je tutasaidianaje hapa ili kupunguza hili tatizo? Tunajua kuna mapenzi ya dhati kabisa baina ya wapendanao lakini mwisho wa siku kunakuwa na kutokuelewana baina yao na mmojawao kuamua kujiua! Tushirikiane kupunguza hili tatizo!
 

Akili mbaya tu. Huyu mtu mmekutana mitaani sasa utajiuaje kwa ajili yake. Akili chafu tu!!! Huyu ni mla nawe, wala hatakufa nawe, ila mzaliwa nawe-wahenga walisema (Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe) sasa kwa nini ujiue kwa mla nawe!!!!!
 
ni ushamba.
 
Kupenda kupita kiasi unapenda 50/50
 
Sumu ya penzi ni kali sana. Hata unywe maziwa huponi.
Hao wengi ni chipukizi wa penzi, fresh graduate ambao hawana hata experience.
Kwa sisi tulio na 10+ experince, hata nikimkuta live, naondoka kama sijaona.
 
Nasema ni ujinga mtupu, I would never consider any permanent solution for temporary problem. Coz too man fish in the pool, just cool off and move on.

Hao wanaojiua kwakweli ni very naive to my thought
 
Kati ya mambo ya hovyo ni haya!
 
Ni kutokujiamini, unadhani hutapata mwingine wa kukupenda, ovyoooooo!
 
inawezekana ni kweli ni ushamba lakini je tutauondoaje?
 
Kungekuwa na connection huko walikoenda tungewauliza kwa nini. Ila kwa mtizamo, ni ujinga tu maana haiwapunguzii kitu wanaobaki.
Hapo umeongea maneno ya kuweza kumtoa mpaa obama white house....Big up.
 
Sumu ya penzi ni kali sana. Hata unywe maziwa huponi.
Hao wengi ni chipukizi wa penzi, fresh graduate ambao hawana hata experience.
Kwa sisi tulio na 10+ experince, hata nikimkuta live, naondoka kama sijaona.

Ninakuunga mkono 100%
 
Msicheze na mapenzi nyie!

Mtu unaweza ukajikuta unaambiwa na mpenzi wako bweka kama mbwa na wewe kweli ukabweka!
 
Kwasababu wanakua wamependa bila kikomo wala mipaka na zaidi ya hapo wanaongozwa na hisia zaidi.

Ni rahisi nyie wengine kutukana na kuwaita watu wa aina hii majina ya kila aina bila kufikiria kwamba wao sio nyie. . . mioyo yao sio sawa na yenu. . .akili zao hazofanyi kazi sawa na zenu. Mtu wa aina hii anahitaji mtu mwingine amshawishi kwamba kuachwa/danganywa sio mwisho wa maisha na sio kutupiwa maneno. Hivyo shukuru wewe unaweza ukadhibiti hisia zako bila kumdharau yule asiyeweza. . . akipata wa kumfundisha/saidia hata yeye anaweza akawa ngangari.
 
Sasa ukijiuwa si ndio unawaachia waungwana wajisevie kwa raha zao!! huyo lazima atakuwa mnyarukolo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…