Waswahili wanamsemo usemao usilolijua ni kama usiku wa giza, samahani kama nitakuwa nimeukosea huo msemo. Ila kwa suala zima la watu kujiua kwa ajili ya mapenzi haitakuwa sahihi tukisema ni ujinga, ni kweli kujiua sio suluhisho ila mkumbuke mpaka mtu anachukua uamuzi huo tayari anakuwa kwenye hali ambayo amekata tamaa, kuchanganyikiwa,anajihisi hopeless, ana kuwa na msongo wa mawazo na mambo mengine mengi ambayo kwa wakati ule yanamfanya kutokuwa normal na kushindwa kuona upande wa pili.
Mtakumbuka ule wimbo wa Msondo ngoma ulioimbwa na Marehemu TX Moshi ambapo ndani yake kuna maneno haya namnukuu......"Mapenzi yakikuchanganyia ni faraja moyoni ila yakikuchachia yaweza kuwa sumu inayoweza kuua kwa dakika chache......akaendelea kwa kusema .....wakati hawa wanafunga ndoa pale mtaa wa pili kuna kijana amejinyonga kwa sababu ya mapenzi... ni wimbo mzuri kama una nafasi utafute uusikilize.
Sio kwamba natetea watu kujiua kwa sababu ya mapenzi ila hoja yangu ni kupingana na watu wanaosema hao wanao jinyonga ni wajinga hapana, Mwombe Mungu yasikukute, kuna watu wamepitia mambo magumu sana ukikaa nao wakakueleza utawasikitikia na ilifika mahala wakawa na mawazo ya kujiua ila kwa rehema za Mungu walisalimika ukipata wasaa wa kuzungumza nao unaweza ukanielewa nina maanisha nini kusema sio wote wanaojiua ni wajinga, na sio kwamba wanapenda kujiua hapana.
Anyway.