Kwanini mwaka 1997 ilinyesha mvua kubwa sana ya El Nino lakini maziwa hayakuleta mafuriko?

Mjadala wa globa warming umeuleta wewe. Hapa swala lilikuwa kwa nini maziwa yanaongezzeka kina cha maji, kitu ambacho hakina uhusiano wowote na global warming, mimi ninavyoona
Al gore mwaka 97 akati anazungumzia global warming effects, alizungumzia kuwa mlima Kilimanjaro baada ya miaka 10 theluji itayeyuka pale juu ,kutakua na unexpected climate changes ambazo zitasababisha mafuriko na bahari na maziwa kujaa duniani kote .

Nimeileta Kama nilivyoisikia kwa Al gore mwaka 97, nafahamu swala la bahari kujaa Lina direct link na myeyuko wa barafu huko Antarctica , Ila kujaa kwa maziwa inaeza kuwa indirect, hasa na hizi mvua ambazo kwa sasa hazina pattern inayoeleweka , Mana tuna mvua toka mwezi wa name mwaka Jana kwa baadhi ya maeneo, maziwa na mito hayakupata kiangazi cha kutosha amabcho kwa kiasi flan huwa kinapunguza kina cha majia

Sent
 
Tuna milima mingapi hapa kwetu yenye theluji ambayo theluji yake ikishayeyuka, inasababisha maziwa yetu kuongezeka kina cha maji, ikiwemo ziwa lenye kina kirefu zaidi duniani kama Tanganyika?
Theluji ya mlima Kilimanjaro imetajwa Kama kielelezo tu , haina maana kuwa kuyayuka kwa theluji ndio kumejaza mito na maziwa la ,ni matokeo tu ya global warming. Ilitajwa milima Kama minne , nilikariri Kilimanjaro sababu upo kwetu. Na yote sasa hivi haina theluji tena

Sent
 
Mvua za mwaka 1997/98 uliziona kubwa kwa sababu miundombinu haikuwa imeimalika kama miiundombinu ya sasa. Hivyo unaipima kwa kulinganisha na madhara ya miundombinu ya wakati huo.

Mvua za mwaka huu hujaona madhara makubwa ya miundombinu kwa sababu imeimalishwa. Lakini mvua za mwaka huu ni kubwa sana na zimenyesha kwa kipindi kirefu sana. Kumbuka baada ya mvua za vuli huwa kunakuwa na mapumziko kisha masika inafuata. Lakini mvua za mwaka huu za vuli na masika zimeunga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kina cha ziwa Victoria kumepungua kwa sababu mbalimbali kubwa zikiwa ni siltation yaani vijimichanga vidogo vidogo (silt) kutuama bottom kabisa na kusababisha kina kupungua, na sababu ya pili ni Eutrophication ambapo ziwa linakua limepokea nutrients (sana sana phosphate na nitrogen) hivo linazidi kua shallow.

Kuna mambo meeengi yanachochea hivo vitu, mengine yanatokana na shughuli zetu za kilimo pembeni mwa ziwa, uvuvi, maendeleo kama ujenzi etc lakini pia mengine ni natural.

Ziwa kama walivyo viumbe hai lina stage, kuanzia kuzaliwa, kukua, kuzeeka na kufa. Nadhani ushawahi kusikia marshlands.

Kufupisha story, siku hizi kina za ziwa Victoria kimepungua sana. Kwahiyo mvua ikipiga maji yanafurika.
 
Tangu tupate uhuru mpaka leo, hakuna mvua kubwa ambayo imeshawahi kunyesha na ikazidi ile ya El-nino. Kama huko mbele ya safari itakuja kutokea mvua kubwa kuzidi hiyo, basi itaitwa La-nina, kama sikosei. As long as La-nina bado haijatokea, then ni obvious kwamba mpaka leo hakuna mvua nyingine tena kubwa ambayo imewahi kunyesha ikazidi ile ya El-nino
 
Usiwe unahusisha matamko ya wana siasa na Sayansi, isipokuwa tu pale ambapo mwana siasa huyo atakuwa anaongea kama mwanasayansi na si mwanasiasa. Yeye alijuaje kama kuyeyuka kwa theluji ya Mlima Kilimanjaro inatokana na Global Warming, so far?

Angalia facts hizi hapa kwamba:
  • Mlima Kilimanjaro ni Dormant Volcano
  • Kama ni volcano iliyolala, then kuna uwezekano kuwa kuna volacanic activities somewhere below its peak, ambazo zinaweza kuwa zinasababisha joto la mlima kwa ujumla kupanda
  • Joto la mlima linapopanda kutokana na activities aidha kwenye base ya mlima, au below, linasababisha theluji juu ya mlima kuyeyuka.
Je, mtu akija na hypothesis/ argument ya namna hii utamkatalia kuwa hayuko sahihi?
 
Hiyo unasemea kidunia mkuu. Mvua kubwa zaidi ya mvua zote zilizowahi kunyesha ikinyesha Tanzania tu au kwa nchi za Afrika pekee kamwe haitapewa jina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…