Kwanini Mwenge Kijijini panapendelewa sana na serikali?

Kwanini Mwenge Kijijini panapendelewa sana na serikali?

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
2,864
Reaction score
8,328
Mtaa wa Mwenge umegawanyika katika mitaa miwili ndani ya kata ya Kijitonyama, wilaya ya Kinondoni . Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwenye kata ya Kijitonyama kuna mitaa miwili ya Mwenge. Mwenge Kijijini na Mwenge Nzasa.
Lakini Mwenge Kijijini tangu mwaka 1974 kuna lami barabara zote, Mwenge Nzasa wanasaga vumbi.

Sasa Mwenge Kijijini kuna barabara nyingi za lami, uwanja wa mpira wa kisasa, soko la kisasa, stand ya daladala na ya mwendo kasi vinajengwa, Mwenge Nzasa hamna hata barabara moja ya lami inajengwa.

Mwenge Kijijini mfumo wa maji taka ni wa uhakika, Mwenge Nzasa tunaelea tu kwenye maji taka yanayotoka Sinza huko?
 
Mitaa ya kina Mropa Sadala ni Kijijini au Nzasa? Na huku kwa kina Samuel Mwachilo wale watoto wa Maryland Bar je?
 
Back
Top Bottom