saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nishati Januari Makamba wamepoteza sifa za kuendelea kubaki kwenye madaraka yao kwa kitumia vibaya nafasi zao za uwaziri kumdanganya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan juu ya mambo mbalimbali ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara zao ili lile lengo lao liweze alilosema Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila liweze kutimia.
Waziri Mwigulu anafahamu fika kuwa nchi yetu kwa mujibu wa taarifa za Benki ya Dunia tuko uchumi wa kati ila yeye kwa kwa makusudi na sababu anazozijua yeye akaenda kumwambia Mh Rais kwamba tumeshuka hatuko tena uchumi wa kati na Mh Rais akaliambia Taifa kuwa tumeshuka kutoka uchumi wa kati.
Waziri Makamba naye anampelekea taarifa za wizara yake Mh Rais kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere litakamilika Mwaka 2024 huku akijua fika kuwa Mkataba walioongeza ni wa mwaka mmoja hadi Juni 2023 lakini kwa sababu anazozijua yeye (Za Chalamila ) akamdanganya Rais wetu na kusababisha taharuki kubwa miongoni mwa watanzania.
Viongozi wetu wakuu wastaafu Mh Jakaya Mrisho Kikwete, Mh Mizengo Kayanda Pinda, Mh Joseph Warioba, Mh Joseph Butiku na viongozi wa dini mbalimbali tunaomba muongee na Mh Rais juu ya utendaji mbovu wa mawaziri wake hawa wawili.
Na kimsingi hao wawili ndio wanaochafua taswira nzima ya Serikali ya awamu ya Sita tofauti na Simbachawene na Mwigulu walivyomsambulia Prof Muhongo bungeni kwamba amedanganya juu ya nchi yetu kushuka kutoka uchumi wa kati.