Kwanini mzazi analazimika kumlipia Tsh 400,000 mwanaye anayesoma shule ya Serikali ya Kiingereza wakati Serikali inatoa elimu bila malipo?

Kila kitu kulalamika? Hujalazimishwa mpeleke huko ambapo elimu ni bure. Kupanga ni kuchagua
 
Bunge Primary, Olimpio na wenzao maeneo ya Posta jijini Daslamu
 
Elimu Tanzania haijawahi kuwa bure. Hawa wanaosema elimu ni bure na kuwapeleka watoto,inawagharimu maisha yao yote. Lengo la kusema elimu bure ni kuhakikisha masikini wanaendelea kuwa masikini wa kutupwa na koo za watawala na matajiri wanaendelea kudominate.
Peleka mtoto shule ya kiswahili aende sekondari ya kata tupate bodaboda na mpiga kura. Wenyewe watapeleka Tanganyika international school halafu chuo marekani akirudi aje agombee ubunge mwanao ampigie debe na kumpigia kula.
 
Ungeleta na ulinganifu wa vitu hivi katika shule hizo za serikali ili tujue zimetofautiana lugha yabkufundishia tu au lah...
1. Final exam results
2. Number of employers (teachers)
3. Extra curriculum activities nk
Kubwa zaidi zingatia namba hiyo namba moja.
 

Nijuavyo mimi hayo sio malipo ya ada bali ni makubaliano ya bodi ya shule na wazazi kuwezesha baadhi ya programu hapo shuleni.
 
Nijuavyo mimi hayo sio malipo ya ada bali ni makubaliano ya bodi ya shule na wazazi kuwezesha baadhi ya programu hapo shuleni.
Hapana ni ada. Na kwa sasa ada ni 500,000 kwa mwaka. Na kiwango hicho hakina tofauti na Medium schools nyingi nchini ukiondoa jamii ya Tanganyika na Fedha Schools.

Makubaliano ya wazazi na bodi ya shule yako kwenye mchango wa chakula na usafiri. Hivyo kwenye hizi medium schools za serikali michango yote kwa mwaka inaweza kufikia 1.2M au zaidi ikitegemea mkoa shule ilipo pia umbali wa mwanafunzi alipo kuifikia shule
 
Kiingereza ni balaa
Kuna shule hapo Ubungo kuna tetesi inavunjwa ili iwe English medium la sivyo ina maana ingebaki kuwa hivyo hivyo ilivyo πŸ˜„
Teh! Hii comment sijui kwanini ilipitwa no comment, no likes! Ni Ubungo NHC nini? Kiingereza kina mazingira yake; even appearance ya walimu na wanafunzi must be different as well as the surrounding environment!
 
Teh! Hii comment sijui kwanini ilipitwa no comment, no likes! Ni Ubungo NHC nini? Kiingereza kina mazingira yake; even appearance ya walimu na wanafunzi must be different as well as the surrounding environment!
Hii nchi ina ujinga mwingi sana
 
Mrudishe Kayumba isiwe nongwa.....ukitaka huko lipa 400k...
 
Tamko lilishatolewa tangu enzi za Mwendazake. Kwamba shule zote za English Medium (za serikali) zitaendelea na utaratibu wao. Kwamba serikali haitazipa ruzuku ya kuendeshea shule hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…