Kwanini Mzee Kilomoni anaishikiria hati ya Simba je ndiye mmiliki au anaidai Simba?

Kwanini Mzee Kilomoni anaishikiria hati ya Simba je ndiye mmiliki au anaidai Simba?

1150456
 
Asante kwa kunipanikia
Swali lako ni la msingi sana kwa mtazamo wangu, namna alivyoipata ndio kunampa nguvu ya kuishikilia kana kwamba ndiye mmiliki wa simba au mmiliki wa lile jengo. Tuanzie hapo.
 
Wadau nimekuwa nafuatilia sana nyuzi mbalimbali humu juu ya Klabu ya Simba.Pia nimemsikia Mzee Kilomoni akisema anayo Hati Klabu ya Simba na haitoi.Najiuliza kwanini Mzee Kilomoni anakuwa na Hati ya Klabu ya Simba?Pili kwanini Mzee Kilomoni anasema Haitoi kwa Uongozi?Je Klabu ya Simba ni mali ya Mzee Kilomoni?Je Mzee Kilomoni anaidai Klabu ya Simba ndio sababu ya kuishikiria Hati?Na mwisho kama Hati ni ya Klabu ya Simba kwanini iwe kwa mtu binafsi na isiwe Klabuni?
KILOMONI, KILOMOMI UNAITAKIA NINI SIMBA WEWE KILOMONI, HUONI MAMBO YALIVYO MUKIDE, in Maulidi Kitenge's voice
 
Si uhakika sana lakini baada ya mzee Kilomoni kuchaguliwa kuwa mdhamini wa mali za Simba pamoja na wenzake wawili ndipo akautumia mwanya huo kung'ang'ania hati za jengo la Simba. Kuna wakati viongozi walijaribu kumuondoa kwenye udhamini lakini ilishindikana kwa sababu walikosea utaratibu. Kiutaratibu hizo hati ni mali ya Simba na zinatakiwa zihifadhiwe ofisini Msimbazi kwenye safe (kasiki) na sio nyumbani kwa mtu.

Lakini nafasi ya kumuondoa bado ipo cha msingi wanachama wanatakiwa wafuate utaratibu kama katiba ya Simba inavyotaka. Akishaondolewa kuwa mdhamini kama katiba inavyotaka kitakachofuata ni kusajili muhtasari wa maamuzi ya wanachama RITA na ofisi nyingine za serikali hapo itatakiwa kisheria Mzee Kilomoni akabidhi hati za jengo na mali zote za Simba alizonazo mikononi mwake kwa wadhamini wapya akigoma sheria itachukua mkondo wake.

Ukiangalia hili suala la Kilomoni linakuzwa tu bila sababu kwa sababu suluhisho lake ni viongozi kufuata taratibu za kisheria kupitia katiba ya Simba basi.Itachukua muda kidogo lakini kutakuwa na suluhisho la kudumu. Lakini kinachoonekana ndani ya viongozi wenyewe kuna kuzunguukana kama alivyosema Mo. Inaonekana kuna viongozi waligombea wakitegemea Simba itakuwa ya upigaji/ulaji kama miaka iliyopita lakini sasa walipogundua kuwa mirija imekatwa wakabaki mchana kuwa na Mo ikifika usiku wapo na Kilomoni lengo lao timu iende kwenye bakuli kama Yanga kwani bakuli halina usimamizi kuwa zimeingia ngapi, zimetumika ngapi na zimetumikaje tumikaje.

Nafikiri ni wakati muafaka kwa viongozi badala ya kulia lia waitishe mkutano waangalie viongozi gani wanaikwamisha Simba kuendelea kutoka hapa ilipofika. Utaratibu ufuatwe viongozi wasaliti waondolewe wachaguliwe viongozi wengine na baraza la wadhamini jipya basi mjadala ufungwe.
 
Sisi ngozi nyeusi tuna roho mbaya na wivu wa kijinga sana, wengi wanaopinga udhamini wa Mo simba hawana point ya maaana, uwekezaji wa mpira ni kama baishara nyingine, manataka MO apate hasara au faida? Pili hao wazee wanao uwezo wa kuwekeza simba au kutafuta muwekezaji mwenyewe moyo, nguvu na motisha kama Mo Dewji?

Sawa labda kuna taratibu hazikwenda sawa, kwa nini wasikae pamoja na kuzitatua? Zaidi hawa wazee mana mchango gani kwenye mpira wa kisasa wenye ushandani mkubwa na pesa nyingi?

Haya mambo sijui ya wazee wa timu sijui nani ndio yanafanya vilabu vyetu na timu ya taifa tunakwama kabisa.

Huyu mzee anaweza baki nayo hiyo Hati kama na simba ikaendela na mashabiki tukafarahi.
Mwisho, haww wazee wakekosa sehemu ya kula kama zamani, hakuna pesa ya mwindi inatoka kifala kama wanavyodhani wanafikiri Mo atawaita chemba awape mpunga wakutosha ndio watoe?

Bora achane na simba kuliko kuwaonga awachie tuone what next..
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom