kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Natafakari tu kwamba REA wamepeleka umeme vijijini lakini wananchi awautumii, waliweza kumudu kuwasha taa chache ndani na kwa muda mfupi saa yaani saa moja Hadi saa nne usiku then ukipita vijiji vingi saa tano utadhani umeme hakuna.
Wakati wanawasha taa chache kwa muda mchache walikuwa wananunua umeme wa elfu tano wanapewa units 40+, na walizitumia kwa zaidi ya miezi mitatu. Nadhani wenye ndugu vijijini na wanaokaa vijijini mtakubaliana na Mimi.
Serikali imefanya Nini? Kwanza, serikali imefuta punguzo lililokuwepo kwa watumiaji wa chini ya units 70 kwa mwezi. Hivyo badala wanunue units 40+ kwa elfu tano watanunua units 14 kwa elfu tano na hii ina maana umeme uliokuwa unanunuliwa wa elfu au elfu mbili hautakuwepo maana units zake Ni chache Sana. Kwa msingi huu aliyekuwa anashindwa kununua umeme wa elfu tano ukiwa units 40+ ameambiwa anunue units 14, je huyu mpiga kura atawasha umeme kwake au atatafuta sukari na unga wa watoto?
Serikali hiyohiyo chini ya wabunge 360+ wakaenda kupitisha Tena tozo ya nyumba kijijini Hadi mjini. So akitaka kununua umeme wa elfu tano atapata wa elfu nne. Ukifuatlia walioweka hizi tozo kwa wananchi wao kudi na tozo hizi wanalipiwa na serikali.
Ndo maana najiuliza tuna uhakika atujaenda kuzima umeme kwa watu Hali ya chini? Tumeangalia athari za kuzima umeme kwa wafanyabiashara wadogo? Je haiwezekani kuwa Kuna watu wanampango wakutumia hii fursa kukwamisha TAnesco ili wauze solar na vyanzo vingine vya nishati?
Wachumi saidieni Taifa.