Kwanini naunga mkono tozo

Kwanini naunga mkono tozo

Huko ktk nchi uliko wananchi mnatozwa kodi mara mbili hata mara tatu au nne ktk pato la pesa ileile wakati uleule (double taxation?)

Hivyo malalamiko ni kwa wafanyakazi wa serikalini pekee?. Makato ya mfanyakazi sita ongelea au kulinganisha na nchi nyingine.

Double taxation zipo ingawa watu hawajui mfano kampuni zinalipa kodi na wamiliki wa kapuni ambao ni shareholders wanalipa kodi tena kutokana na kipato kilekile.

Kwa ujumla wake Watanzania ni walalamishi wakati huohuo hawafuatilii mambo wakati yakitokea. Bunge limekaa na kujadili hili mlikuwa hamsemi lolote, serikali wakati inatoa mapendekezo wazi kwa umma mlikuwa hamsemi chochote kwasababu mlifikiri ni wengine ndiyo watalipa. Imefika wakati badala ya kulalamika tafuta kipato zaidi. Tanzania ni nchi ambayo uzalishaji ni mdogo sana kiasi kwamba vitu kama hivi vitalazimisha watu wafunguke na kwenda kujishughulisha na uzalishaji. Wananchi wanatakiwa wahoji baada ya mwaka hiyo miradi ya umwagiliaji lakini vilevile tuhoji wale ambao hawajishughulishi. Lakini wafanyakazi wa serikali wasilalamike kama kazi za serikali hazilipi kajiendeleze kwa kutafuta sehemu nyingine. Karibu Dunia nzima kazi za serikali nyingi ni za viwango vya chini. Tumia muda mwingi hapa kutafuta namna nyingine za kipato na kuuliza maana utakuwa una lalamika kila mwaka huu ndiyo mfumo mpya wa nchi. Tozo zitapungua pale tu uzalishaji ukiongezeka. Badala ya kulalama husle ndugu yangu hao wengine ni watanzania kama wewe.
Baada ya kusoma hapa sasa naweza kuthibitisha bila shaka yoyote kuwa hujui lolote namna mfumo wa kodi ufanyavyo kazi...

Yaani unajadili ishu kwa hisia/dhahania badala ya uhalisi wa kisheria. Na nimegundua hata hujui maana ya "double taxation" na kwamba hilo linapofanywa na mamlaka za kikodi, basi linakuwa ni kosa kisheria...

In case kama ulikuwa hujui, kodi hutozwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge...

Serikali haichukui tu fedha za watu kwa sababu wanafanya kazi na kujipatia fedha. Ikifanyika hivi, huo ni wizi. Hatufanyi kazi ili serikali ije ichukue tu fedha zetu nje ya utaratibu kwa jina la "kodi au tozo". Huo ni wizi..

Hiki ndicho kinachofanyika sasa na hoja zako zote zimejikita katika mantiki hii...

Rudi kwenye sheria na taratibu za kikodi. Kisha njoo tena tujadiliane...
 
Baada ya kusoma hapa sasa naweza kuthibitisha bila shaka yoyote kuwa hujui lolote namna mfumo wa kodi ufanyavyo kazi...

Yaani unajadili ishu kwa hisia/dhahania badala ya uhalisi wa kisheria. Na nimegundua hata hujui maana ya "double taxation" na kwamba hilo linapofanywa na mamlaka za kikodi, basi linakuwa ni kosa kisheria...

In case kama ulikuwa hujui, kodi hutozwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge...

Serikali haichukui tu fedha za watu kwa sababu wanafanya kazi na kujipatia fedha. Ikifanyika hivi, huo ni wizi. Hatufanyi kazi ili serikali ije ichukue tu fedha zetu nje ya utaratibu kwa jina la "kodi au tozo". Huo ni wizi..

Hiki ndicho kinachofanyika sasa na hoja zako zote zimejikita katika mantiki hii...

Rudi kwenye sheria na taratibu za kikodi. Kisha njoo tena tujadiliane...


Nakushukuru kwa mawazo yako. Kazi iendelee
 
Kampuni zinalipa kodi ni kweli? Hiyo pesa wanaikata kwenye nini? kwenye faida baada ya kampuni kupata faida.
Tena hizi kampuni za kigeni zina msamaha wa kodi( Tax relief), ulisikia lini mfanyakazi ana msamaha wa kodi? uliona wapi wananchi wamesamehewa kodi zao?

Kampuni zinaondoa kiwango kikubwa cha pesa kwa kutumia mfumo wa depreciation na non discrimination service kama chai ya Asubuhi. au chakula cha mchana.

Kampuni nyingi ile Net profit inayotakiwa kukatwa kodi inakuwa imepungua mno, kwa kutumia mbinu ya Tax evasion, Hivyo usielezee jambo usilolijua.

Kampuni nyingi zinatunza kiwango kikubwa cha pesa kama kama Reserve hivyo kukwepa kukatwa Umemzungumzia Mwanahisa(shareholder) ambaye anapokea gawio(Divinded) huyu yupo liable kulipa withholding tax kwa kuern pesa kutokana na uwekezaji wake na sio double taxation.

mkuu hivi unafahamu maana ya double taxation kweli? unafahamu sheria ya Tz na kimataifa haziruhusu jambo hili, kwa nini huoni ni tatizo?

Itakuwa mlamba asali wewe
Ni Mwigulu si mwingine kamanda! Huyu mzandiki tunaumia halafu anatuandikia ulimbukeni wa Texas!.
 
Wewe ni laana kwa tumbo lililokubeba miezi tisa pamoja na hao waliokutuma.
 
Baada ya kusoma hapa sasa naweza kuthibitisha bila shaka yoyote kuwa hujui lolote namna mfumo wa kodi ufanyavyo kazi...

Yaani unajadili ishu kwa hisia/dhahania badala ya uhalisi wa kisheria. Na nimegundua hata hujui maana ya "double taxation" na kwamba hilo linapofanywa na mamlaka za kikodi, basi linakuwa ni kosa kisheria...

In case kama ulikuwa hujui, kodi hutozwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge...

Serikali haichukui tu fedha za watu kwa sababu wanafanya kazi na kujipatia fedha. Ikifanyika hivi, huo ni wizi. Hatufanyi kazi ili serikali ije ichukue tu fedha zetu nje ya utaratibu kwa jina la "kodi au tozo". Huo ni wizi..

Hiki ndicho kinachofanyika sasa na hoja zako zote zimejikita katika mantiki hii...

Rudi kwenye sheria na taratibu za kikodi. Kisha njoo tena tujadiliane...
Wizi Tena wa dhahiri.
 
Kwanini hizo tozo mnazokata kila dakika kwenye miamala ya simu hatuambiwi mapato na matumizi yake kila mwezi kama ilivyokuwa mwanzo?

Kwanini kwa huo ukimya wa waziri wa fedha tusiamini sehemu ya hizo pesa za tozo zinachezewa hasa tukiskia tuhuma za kumiliki timu ya mpira wa miguu, na mabasi 60 kuingizwa nchini?

Kuna mtu anawatumia, sasa kamwambie akupe majibu ya hayo maswali ndio urudi hapa.
huyo ni mpuuzi fulani.hakuna anayekataa tozo kinacholalamikiwa tozo ni kubwa na zinakatwa kiholela.mshahara unatozwa kodi kwa nn ukienda benki kuchukua mshahara wako utozwe tena?we jamaa umeandika mengi lkn ni utumbo mtupu.wananchi tukusanye nguvu 2025 kuiondoa ccm madarakani.hakuna mwenye huruma ndani ya ccm.wabunge wote wafyekelewe mbali hawana msaada kwa wanyonge.wanaharakati hakikishe mnaenda vijijini kuwaelimisha wananchi madhara tutakayoyapata endapo tukikirudisha hiki chama madarakani.
 
Kwanza tuweke mambo sawa tozo ni aina ya kodi. Hivyo tusiongelee tozo kama vile sio kodi.

Mimi binafsi sijaona ubaya wowote wa serikali kuweka tozo na nina fikiri hakuna njia nyingine kwa wakati huu zaidi ya tozo na nitajaribu kuweka hoja hapa vizuri. Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji pesa ili iweze kuwekeza kwenye miradi mingi sana kuanzia elimu, maji, barabara, umeme, kilimo, ulinzi, n.k

Sasa vyanzo vya mapato ni hivi;
  1. Missada kutoka nje
  2. kodi na tozo
  3. mikopo
Tanzania tumeshakopa na bado tutaendelea kukopa kama tutapata mikopo nafuu lakini vilevile tunakusanya kodi mbalimbali. Lakini ukiangalia vizuri budget zetu pesa ya kodi ambayo haitoshi hata kwenye budget bado inaenda kwenye shughuli ambazo sizo za kimaendeleo hivyo sio uwekezaji wa nchi bali ni matumizi.

Kuna miradi tunalipia kwenye kodi kama ya maji na umeme lakini wakati wa Kikwete pesa karibu yote ilikuwa ni kulipa mishahara na matumizi ya serikali.

Sasa kama nchi tuko kwenye kipindi cha uwekezaji kwa mara ya kwanza tunaanza kuona barabara za kisasa, shule bora, hospitali na umeme hasa vijijini. Sasa tumefikaje hapa ? Ni kuwekeza kwa kodi mpya na tozo.

Umeme mfano wa vijijini umepelekwa na tozo maalamu kwenye luku za nyumbani na barabara za vijijini nyingi zinatengenezwa na tozo kwenye mafuta. Lakini ili kama nchi tuweze kuwekeza na kuongeza walipa kodi ni lazima tuwekeze kwenye kilimo.

Kilimo kitaongeza mapato kwenye kodi lakini tatizo hatuna mfumo mzuri wa kilimo kuwa na uazalishaji wa uhakika. Bashe amekuja na mpango mzuri wa kuongeza uzalishaji kwa kufanya yafuatayo (1) Serikali itatoa ruzuku kwenye mbolea (2) Serikali itawekeza kwenye umwagiliaji (3) watatoa mbegu (4) watafuta wawekezaji wa viwanda (5) kutafuta masoko.

Hii ndiyo mojawapo kubwa ya kuongeza ajira na kodi lakini mtaji wa yote haya ni karibu Trillion moja sasa mtaji unatoka wapi? Hii ndiyo sababu imeenda kwenye tozo hivyo tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji wa uhakika wa kuongeza kodi kwa miaka ijayo. Lakini ni tukiangalia vizuri tatizo letu ni utamaduni mbovu watu wengi walizoea kukaa bila kulipa kodi wala tozo.

Mimi ni diaspora wa muda mrefu sana na naishi na kutafuta maslahi yangu jimbo la Texas. Hili jimbo letu linajulikana kwa kuwa na kodi ndogo lakini ngoja niwape data kidogo ili mgundue tonavyolipa kodi.
  • Nyumba kila mwaka nalipa 3% ya thamani ya nyumba. Hivyo kwa mfano kama nyumba pale Tanzania yenye thamani ya Tsh 100,000,000 basi unatakiwa kulipa kila mwaka Tsh 3,000,000. Hakuna mjadala kwenye hili na usikolipa unapekwa mahakamani na nyumba inapigwa mnada.
  • Jumuia na majiradi vilevile wana kitu kinaitwa HOA-Housing Owners Association hii ni jumuia ya makazi yako na majirani kila nyumba inalipa $350-$1000 kwa mwaka kwa usafi wa jumla kama kukata majani na kusafisha mitaro. Hii ni nje ya nyumba yako hii nayo ni lazima na kisheria wanaweza kwenda na utaratibu mpaka wakapiga mnada nyumba.
  • Tuna tozo za maji na kuchukuwa taka. Kila wiki wanapita kuchukuwa taka kwenye magaloni maalumu. Hii inafanywa na manispaa huwezi kuchoma matakataka ovyo ovyo. Maji unalipa kutokana ma matumizi lakini taka utalipia unataka au hautaki jumla sio chini ya $100 kila mwezi. Ukitupa uchafu ovyo ni faini, usipoweka uchafu vizuri kwenye mifuko ni faini.
  • Barabara nyingi zinajegwa kwa mikopo inayoitwa goverment bonds hivyo ni lazima ilipwe. Kila nikienda kazini kwa mfano ni lazima nipitie kwenye barabara za kulipia "toll roads" na natumia sio chini ya $5-$7 kwenda kwa siku moja na kurudi. Tena hii ni rahisi New York wanatumia $12-$15.
  • Ukienda kwenye hotel na kokodi chumba karibu 35% ni kodi na tozo, kwenye simu, cable za TV au Dish hivyohivyo.
  • Kwenye super market kila ukinunua kitu kuna 5% ya tozo inaenda kusaidia “Metro" ambayo ni kama mwendo kasi yetu.
  • Lakini hapa kuna bima ya karibu kila kitu nyumba ni lazima uwe na bima na kwenye hizi bima kuna pesa zinaenda kusaidia idara kama zimamotto na ambulance.
Hapa sijaongelea tozo na kodi za mishahara. Lakini mjue hapa bado tuna nafuu sana kulinganisha na nchi za Ulaya au Canada ambako Tozo na kodi zipo juu sana. Familia yangu ina bahati tuna nyumba Uninio sehemu ambayo ina thamani sana lakini kodi zetu pale hazifiki hata 1% ya thamani wakati bodaboda wanalipa kodi kwenye mafuta. Hivyo kuna sehemu kiukweli wanaonufaika ni matajiri tu kusema ukweli.

Kuna ambao watasema huko Ulaya na US pesa inaonekana ni kweli tuna shule kwenye kila mtaa za watoto zina mabasi na ni bure lakini tunalipa 3% kwenye thamani ya nyumba na pesa inaenda huko. Hivyo hoja ni yaanze mayai au kuku lakini kodi ni muhimu na maendeleo ni muhimu.

Ndiyo maana hoja yangu ni kwamba tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji na utaratibu mpya wa kuongeza wigo la walipa kodi na kuweka mifumo ya kimaendeleo.

Tatizo kubwa ni mazoea ya watu wengi walikuwa wamezoea kukaa bila shughuli na kubangaiza lakini kama tunataka umeme vijijini, barabara za lami na hospitali ni lazima zitengenezwe, kuwe na pesa za matengenezo kila mara na pesa za wahudumu.

Ni lazima kuwe na mfumo wa mapato na wananchi ni lazima wazalishe ili waweze kuwa na mifumo hii. Huwezi kukaa kijijini hulipi kodi yeyote, huzalishi chochote halafu unahitaji barabara, maji, umeme ... pesa inatoka wapi? Ni lazima serikali iwekeze kwenye kilimo ili wewe mwanakijiji uweze kuchangia kodi na maendeleo na ndicho kinacho fanyika kwa sasa.
Waartabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba!!
 
20220910_001513.jpg
20220910_001149.jpg
 
Back
Top Bottom