Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakati iraq anavamiwa kwa kisingizio cha wmd ilikuwa karne ya 8 ?Kwenda shetani wewe century ya 20s unaweza vita .Dollar moja ni 0001 ruble . Watu wamekufa .Ukraine ni nchi independent .Idi amini alivyo taka bukoba Nyerere akamuondoa kwa vita so puleeese
sisi tutanunuaKuna wakati nilitaka kununua kitabu chako cha Ujasusi wa Kidola, ila nilivyosoma hoja zako hapa nimepata wasiwasi mkubwa na uelewa wako wa mambo.
Democracy gani ambayo huruhusiwi kufanya maamuzi yoyote kwenye rasilimali zako na kupewa masharti magumu kimikataba ili uzidi kunyonywa tu kiuchumi tangu 1961 TZ ipate uhuru?Unahubiri demokrasia halafu unashabikia udikteta wa Putin.
Tangu na tangu haijawahitokea na haitatokea Rais yeyote kukubaliwa na Raia wake wote 100%.Swali langu moja tu.
Kwa ufafanuzi huu wenye mantiki kubwa hivi (plausible), inakuwaje Putin anakosa uungwaji mkono mkubwa na wananchi wake hadi kutegemea kuwa na bunge ambalo ni "rubber stamp", kudhibiti upinzani kwa mkono wa chuma, kutumia vikosi vya wasiojulikana kudhibiti ukosoaji (police state), kuimarisha tawala za kidikteta huko Belarus na Venezuela, n.k.
Wnanachi wa Urusi wamesikika wakilalamikia vikwazo vya NATO na Marekani kwamba si fair kwao kwani wao "hawakumchagua" Putin kuwa rais wao! Hiyo ni vita yake binafsi! Akwamishwe yeye na wapambe wake; sio raia wote wa Urusi.
Inafahamika kuwa huko Urusi, utawala wa Putin ni "one man show": hashauriwi, hakosolewi wala hapingwi na mhimili wowote. In maana kuwa ni yeye peke yake anayejua na kuyaona maslahi ya Urusi na ya Warusi? Wananchi wa Urusi hawana habari ndugu zao wakinyanyaswa na kuuawa huko Donbass, Crimea na Georgia? Warusi wote hawaoni janja ya Marekani na NATO kujiimarisha kijeshi kutishia usalama wa Urusi kupitia Ukraine na nchi zingine jirani (former USSR)?
Hoja yako inashawishi (plausible) lakini inatia shaka - doesn't sound rational. Ingekuwa hivyo, huyu mtu angetambuliwa na watu wake kama shujaa na sauti yao kumkubali ingesikika bila mikwaruzo. Au Marekani pia wamefanikiwa kudhibiti kikamilifu sauti halali ya Warusi? Au wamewageuza Warusi wengi kuwa vibaraka wao?
Marekani aliua wangapi hovyo hovyo huko Iraq,Afghanstani,Syria,nk?Ndiyo aue watu hovyo hovyo hivyo?
Hayo mawatu hayatofautiani na yale yaliyoaminishwa ujinga kuwa bila ya kununua na kupakaa mafuta ya upako ya yule Nabii wa uwongo basi hayawezi kuponywa na changamoto za kidunia.Vijana wengi humu wanasikiliza BBC, CNN na vyombo vingine vya magharibi hawajishughushi kabisa kupata habari au kusoma historia ya dunia kuanzia vita ya pili ya dunia hadi vita baridi vilivyopelekea Umoja wa Urusi kusambaratika...
Wengi wao hata ukiwauliza kwa nini NK na SK zilitengana hawajui, ila wanaishi kwa propaganda za Marekani tu.
Akikujibu hili swali nijulishe tafadhali [emoji28]Mbona halijawahi kupiga kura kuilaani Marekani mkuu??
Hatimaye nimekutana na makala yenye uchambuz wa msingi kuhusu hii vita. Nilikuwa naunga urusi bila kuwa na nguvu ya hoja kama hii. Asante yerico sasa na kitab chako nanunua! Una akiliPicha ya kwanza juu ni kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk bwana Denis Pushilin, Na picha ya chini ni kiongozi wa Jamhuri ya Watu wa Luhansk bwana Leonid Pasechnik, Jamhuri hizo ni majimbo yaliyojitenga toka Ukraine.
Naomba nianze utangulize wa makala yangu kwakusema, Dunia ili iwe salama inatakiwa kuwa na wakubwa wawili au zaidi (balance of power), sio mmoja tu anaamua yeye kwaajili ya dunia na hapingwi, Mbele ya Urusi sasa hatutaona vita vya holela vya Marekani na washirika wake.
Sababu ya kwanza ya kuunga mkono Urusi ni kwamba ni hatua muhimu ya kukomesha mauaji ya miaka karibu kumi sasa yanayofanywa na Ukraine dhidi ya Wananchi wa Majimbo ya Luhansk na Donetsk. Kwa msiojua Mtangulizi wa Rais Zelensk wa Ukraine, bwana Petro Poroshenko tangu ashike madaraka 2014 aliendesha mauaji ya wapinzani wengi katika majimbo ya DPR na LPR yaliyotaka kujitenga hadi alipoondoka tu vita havikumalizika.
Alipoingia Zelensk nae akafuata nyayo za mtangulizi wakw, akaigeuza Ukraine kuwa jehanamu kwa aliowaita waasi, aliendesha mauaji makubwa sana hasahasa 2021 dhidi ya raia kule katika miji ya Donbass katika kile alichokiita kudhibiti waasi wanaotaka kujitenga. Dunia hii ilikaa kimya, Urusi ikawa ndio pango la kupokea wakimbizi zaidi la laki tatu,
Kiongozi Jimbo la Donetsk Bwana Denis Pushilin amenusurika mauaji zaidi ya marakumi hadi alipoomba ulinzi wa kimataifa kutoka Moscow, na mwisho akaongoza mapambano na kufanikiwa kujitangazia Uhuru.
Vile vile kiongozi wa jimbo la Luhansk bwana Leonid Pasechnik nae ilimlazimu kutafuta hifadhi ya kisiasa Moscow kwa lengo la kunusuru maisha yake dhidi ya Rais wa Ukraine bwana Zelensk aliyeapa kufuta uasi katika majimbo hayo, Aliongoza mapambano kwa ushirika wa Kiongozi wa jimbo la Donetsk bwana Pushilin na hatimaye wiki jana wamefanikiwa kumshinda Zelensk na Kujitangazia Uhuru.Urusi imeyatambua majimbo hayo kama nchi huru, Belarus na nchi nyingine tano yayari zimetambua. Ukraine imepinga uhuru huo ikaapa kuendesha vita nzito zaidi dhidi ya waliojitenga, Hatua hiyo ikawalazimu viongozi wa mapinduzi waombe msaada wa kijeshi kutoka Urusi. Na wameupata. Oparesheni ya Urusi ndio mwarobaini wa kukomesha mauaji ya miaka zaidi ya kumi sasa, kinyume na hapo miji itaendelea kuvuja damu kila kukicha.
Sababu ya pili ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kutaka kujenga ngome ya kijeshi Ukraine, na katika kutimiza hilo Marekani kwakutumia washirika wake wa Nato wakamshawishi avunje Mkataba wa Minsk wa 2015 pamoja na mambo mengine, ulisema Ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Urusi (Ukraine) uliokuwa Umoja wa Kisoviet ya zamani Hautaruhusiwa kujiunga na Umoj wa Ulaya. Katika kibri cha Zelensk akaomba kujiunga NATO. Moscow akajibu kwa moto.
Sababu ya tatu ya kuunga mkono Urusi ni kitendo cha Marekani kupitia shirika lake la kijasusi la CIA kuvuruga dili la Urusi la kujenga bomba la awamu ya pili la gesi maarufu kama NORD STREAM II, ambalo lingelisha gesi Ulaya yote kwa 90% tofauti na sasa mbapo Ulaya inategemea gesi ya Urusi kwa 40% tu, Marekani ameitumia Ukraine kukwamisha mradi huu na baadhi ya nchi za Nato. Kitendo hiki ilikuwa ni uchokozi wa kiuchumi na kijasusi, Jibu la Urusi limeanzia kwa Ukraine kwanza.
Mtazamo wangu kama Yericko Nyerere, vita hivi ni kati ya Urusi na Marekani, na vitaisha kwa nchi hizi mbili kukaa chini na kukubaliana terms and conditions kama mihimili miwili mikuu duniani. Na sio vinginvyo, Ukraine kwa sasa ni uwanja wa biashara ya Silaha ya ulaya na Marekani.
Baada ya vita hii Urusi ataheshimiwa na kuogopwa sana, na vikwazo hivi amini ni geresha tu, havitachukua miezi 18 vitaondolewa, Rejea vikwazo vya 1990 alivyowekewa Urusi alipoivami Afghanustan vilimwathiri nani na viliishia wapi zaidi ya Afghanistan kusambaratishwa? Haya vikwazo vya Urusi vya 2008 alipoivamia Georgia viliishia wapi na vilimwathiri nani zaidi ya Georgia kuwa eneo muhimu la Urusi hadi leo? Vikwazo vya Urusi vya juzi tu baada ya kuivamia Cremia vimefiki wapi?.
Kikwazo ambacho kilikuwa tishio kwa uchumi wa Urusi alichowekewa na EU ni hiki cha kuzuia huduma ya kibenki ya SWIFT, Lakini ndani ya saa 24 tu, Rais wa Urusi Vlamir Putin ametangaza hatua za dharula kukabili vikwazo vya kiuchumi, na haraka Urusi na China wamekubaliana kutumia huduma ya kibenki ya China ya Cross-Border Interbank Payment System, or CIPS. Kwa tafrisi hiyo nikuwa kikwazo cha uchumi hakitaiathiri Urusi moj kwa moja.
Ukweli ni kuwa Nchi nyingi duniani haziwezi kuendesha chumi zao, katika nyanja nyingi kama za kijeshi na mengineyo bila Urusi. Dunia inaihitaji Urusi kuliko Urusi inavyo ihitaji dunia yenyewe. Japo wanategemeana. Mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU) yapo 27, ukijumlisha na Marekani jumla ni nchi 28 tu, haya mataifa sio yote yanaipinga Urusi, Dunia ina nchi 195 + Donetsk na Luhansk, ni 197, Sasa jiulize nchi 164+ ziko upande upi?. Bado mtu anasema Urusi imetengwa na dunia? Basi huyo mtu haijui dunia sawasawa.
Ni wazi kwamba, Dunia leo iko mapande matatu, kuna Urusi, Kuna Uchina na kuna Marekani... Kwenye nchi 28 Uchina hayuko huko, zingatia kuna nchi za kati zenye uchuki mkubwa ambazo ni India hayuko na Ukraine, huko Brazil hayuko huko na Ukraine... Na hawa wanamuunga mkono Mrusi.... Dunia sasa inastawi na hii ndio balance ya dunia na inapumua vizuri sasa.
Na Yericko Nyerere
View attachment 2136291View attachment 2136292
Haungwi mkono na watu wangap au nchi ngap! Ukileta hoja za kitakwimu unajipa mzigo wa ku prove! Hebu soma makala tena. Umejawa hisia. Usisahau......THE MAJORITY ARE ALWAYS NOT RIGHT!Swali langu moja tu.
Kwa ufafanuzi huu wenye mantiki kubwa hivi (plausible), inakuwaje Putin anakosa uungwaji mkono mkubwa na wananchi wake hadi kutegemea kuwa na bunge ambalo ni "rubber stamp", kudhibiti upinzani kwa mkono wa chuma, kutumia vikosi vya wasiojulikana kudhibiti ukosoaji (police state), kuimarisha tawala za kidikteta huko Belarus na Venezuela, n.k.
Wnanachi wa Urusi wamesikika wakilalamikia vikwazo vya NATO na Marekani kwamba si fair kwao kwani wao "hawakumchagua" Putin kuwa rais wao! Hiyo ni vita yake binafsi! Akwamishwe yeye na wapambe wake; sio raia wote wa Urusi.
Inafahamika kuwa huko Urusi, utawala wa Putin ni "one man show": hashauriwi, hakosolewi wala hapingwi na mhimili wowote. In maana kuwa ni yeye peke yake anayejua na kuyaona maslahi ya Urusi na ya Warusi? Wananchi wa Urusi hawana habari ndugu zao wakinyanyaswa na kuuawa huko Donbass, Crimea na Georgia? Warusi wote hawaoni janja ya Marekani na NATO kujiimarisha kijeshi kutishia usalama wa Urusi kupitia Ukraine na nchi zingine jirani (former USSR)?
Hoja yako inashawishi (plausible) lakini inatia shaka - doesn't sound rational. Ingekuwa hivyo, huyu mtu angetambuliwa na watu wake kama shujaa na sauti yao kumkubali ingesikika bila mikwaruzo. Au Marekani pia wamefanikiwa kudhibiti kikamilifu sauti halali ya Warusi? Au wamewageuza Warusi wengi kuwa vibaraka wao?
Vitabu vya Yeriko vinasomwa na wenye utambuz wa awali wa masuala ya dunia. Wewe uliharib pesa yako bure kununua na ukijua level yako ni riwaya za shigongoHata mimi jana nimechoma mavitabu yake
yaani sikutegemea kama Yeriko angeandika kitu kama hikiHivi ikitokea mikoa wa Mwanza na Kagera zikatangaza uasi dhidi ya serikali ya jamhuri ya Tanzania vipi Rais atakaekuwepo ataacha hiyo Hali iendelee?vipi hatachukua hatua za kijeshi ili kulinda Taifa lake na kuleta umoja wa kitaifa? Je huoni kwamba asipochukua hatua za kijeshi ni kama atachochea mikoa mingine kujitenga?
Kwa maana hiyo je kosa la Zelenski liko wapi Mana alikua anazima uasi ili kulete umoja wa Taifa lake?
Pia tambua Ukurain ni Taifa huru hivo kujiunga NATO sio kosa
Mwisho acha kudanganya watu vikwazo vya kiuchumi lazima vitaua uchumi wa Urusi ni swala la muda tu.
Kwa hii thread Leo umepuyanga.
Hiyo inamaanisha uwezo wenu wa kuchanganua mambo unatofautiana[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]yaani sikutegemea kama Yeriko angeandika kitu kama hiki