Kwanini nawachukia wanaume?

Kwanini nawachukia wanaume?

"Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?"
unalalamika lakini inaonekana unaipenda kazi yako!wanasema kila MALAYA huwa anastory ya kutokea!
Baba Juice, nilitaka kutukana lakini nimekumbuka ni miongoni mwa
mambo ambayo nimeanza kuachana nayo. Hebu fikiria mwenyewe
kama una ubinadamu miongoni mwa mambo ambayo tulikuwa tunakumbana
nayo ni kuwa unakutana na mwanaume ambaye mwisho wa siku
hataki kukulipa na ukiendelea kumdai anatishia kukuletea Polisi, Kupigwa
kutukanawa ni vitu ambavyo tunakumbana navyo, Napenda nikuambie
tu kuwa Mungu ndo anajua ukweli wa yote, Lakini ni ukweli kwamba wako
wanaofanya kwa kupenda. Yuko dada mmoja tulikuwa naye lakini yeye
hakuna alichokuwa anakosa kutoka kwa wazazi wake!
 
salamu na kwa wakaka/wababa/wababu wanaotafuta wachumba humu.
eimen,Bwana asifiwe sana,nuru ya Bwana ikuangazie na umwone TF hana mana mbele ya Bwana,na TF umwachie Bebii na SL,utafute wa kwako nje ya TF,eimen.
 
Mcharuko pole saana Mpenzi na hii story ulotoa hapa.... INASIKITISHA kwa kweli. Pole saana. However Men are funny creatures... Mwanaume yeyote yule haaminiki dear.. wapo exceptions ambao waweza kua waaminifu but majority wako hivo.. in other words ina maana it is better woote uwachukulie wako hivo ili ujue jinsi ya kuwa-handle. Wanaume awe babako, awe Mjombako, awe babuyo, awe kakako, awe binamu.. woote hao wana possibility kubwa ya kukulala wewe.... it is a sad fact but true.

Back to you.... Wee ni more of a psychological problem. inaonesha you enjoy sex, ila tu kuwaamini ndo kero kwako, kumuamini mmoja wao akawa your shoulder ndio inakua shida... However you should know kua as much as they are funny creatures wana umuhimu saana katika maisha yetu in one way or another... Na the good thing ni kua you and only you have the power ya kuamua ni jinsi gani wakutreat... you want them to treat you like shit; they will treat you like shit! You want them to treat you like a hooker: they will treat you like a hooker! You want them to treat you like a queen; they will treat you like a queen! In short you just have to study em' know the type of guy you like... And stick to him.

Note that sio kazi ndogo kujitune uweze wapenda... But jaribu dear for ni muhim. Best of Luck.

Pamoja Saana
ADI.

Pole sana bibie inawezekana kufuta yote mabaya uliyoweka juu ya kuwachukia wanaume ni ngumu kwa mara 1 ila naamini kama utawaona wataalam wa masuala ya mahusiano(kama dismas lyasa) wanaweza kukusaidia kutoka katika hilo tatizo. Amini IMPOSSIBLE = I ' M POSSIBLE.
 
Mcharuko,

Pole sana ila kuna mwanafalsafa moja wa kichina anaitwa Lao Tzu alisema hivi maisha yamejengwa na vitu vitatu. yaliyopita ambayo yashapitwa na wakati. Yajayo ambayo hujui kama utayafikia. Ya sasa ambayo ndio unaishi. Yaliyopita yashapita na huwezi kuyabadilisha mshukuru mungu mzima wa afya na usamehe. Yajayo huna uhakika kama utayafikia. Yasasa ndio unayoishi ni bahati kwani ndio unayoishi hivyo shukuru mungu na ujenge maisha yako. Usiseme hutapenda mwanaume kwani bado unayo nafasi ya kupenda moyoni. Do not live with regrets and denials forget the past is gone focus on the present and future.
 
Pole. Shukuru hao wanaume si damu yako. Si ambao ni machangudoa tu waliyopitia hayo, hata walio kwenye ndoa wanaweza kushuhudia ya unyama walio wahi fanyiwa. Kilio cha hayo kitakuwa chako tu mpaka unaingia kaburini, kifupi no body cares. Your still young unaweza kubadilisha ukurasa wa maisha yako. Focus on life you dreamed before and find new good and great opportunities. Utashangaa mwenyewe watakapokuja wanaotamani kuwa na wewe maishani na si kitandani tu. I believe you are strong woman and fighter, fight for your dreams. Hayo ni mapito tu, still you can make your tommorrow.
 
Pole sana Mcharuko inasikitisha sana kuona wale walio marafiki wa karibu wa Baba yako nao walikutongoza, lakini si wanaume wote wako hivyo na labda chuki kubwa uliyokuwa nayo kwa Wanaume itapungua au kupotea kabisa pale utakapojaliwa kumpata mwanaume atayekupenda kwa mapenzi ya kweli. Pole sana.
 
Ahsante kwa mtazamo wako, nimefundishwa mengi huko juu nazidi kusikia uchungu ninaposoma
Comment mbalimbali. Nipo hapa Jf kwa siku nyingi kiasi nimeingia kwa ID hii ili niweze kutoa ukweli
hata hivyo imenichukua muda toka kujiunga mpaka kufanya kile nilichodhamiria mwisho wa yote
nimefundishwa kusamehe. NIMEKUSAMEHE!

Hapa JF wengi wakikosa cha kufanya hutunga stori za namna nyingi kusudi wapime mitazamo ya watu. Kama wewe ni mwaJF wa muda mrefu basi hili unalielewa kuwa wengi ni watunzi wazuri humu, ndio maana nimetoa maoni jinsi nilivyohisi kuwa ni stori zile zile.

Kama kweli haya ni ya kweli na yamekutokea na unakiri kuwa umetenda na kuwa umetubu na umemwomba Mungu msamaha wa dhambi zako na kwa kuwa husingizii kukosa wazazi ni chanzo cha haya na kuwa ni shetani alikuzidi kete basi niseme kuwa nami nayafuta maoni niliyoyatoa juu yako na kama yamekuumiza nafsini mwako unisamehe.

Pili, Sisi sote ni wadhambi hakuna mfano wa kutoa wa kiumbe kilichozaliwa na Eva kuwa hakina dhambi. Jiridi tu Mungu wako anakupenda sana. Huna sababu ya kukata tamaa. Kama unaweza kuwa mwanaJF kwanini ushindwe kukabiliana na tabia na mwenendo wako? Naamini kuwa huku kuwa mwanaJF ni kuwa unapenda maendeleo yako binafsi na ya nchi yako. Kwa hiyo usikate tamaa na uwasamehe wote waliokukosea na Mungu atakulipa.

Samahani kwa posti zangu za awali. Na uwe binti mzuri.
 
kisa cha kugusa nafsi! nianze kwa kukupa pole.

mfumo wa uchumi kwa jamii za kiafrika umetawaliwa na wanaume, na inasikitisha kupata rabsha na mikiki ya mfumo huu ukiwa na umri mdogo!

usikubali historia yako ikuzuie kuisha maisha yako ya sasa na baadae. jifunze kutokana na matukio ya kimaisha.

nakushauri sitisha mahusiano kwa muda, hadi hisia mbaya kwa wanaume zipungue.
 
Ahsante kwa mtazamo wako, nimefundishwa mengi huko juu nazidi kusikia uchungu ninaposoma
Comment mbalimbali. Nipo hapa Jf kwa siku nyingi kiasi nimeingia kwa ID hii ili niweze kutoa ukweli
hata hivyo imenichukua muda toka kujiunga mpaka kufanya kile nilichodhamiria mwisho wa yote
nimefundishwa kusamehe. NIMEKUSAMEHE!
Strange!!...............

Taito ya thread "kwanini nawachukia wanaume"

Utasameheje wakati bado una chuki?
 
Bi Mcharuko:

Hii post imenifanya nitoke mafichoni kwa muda!

Wanawake wengi (hasa ambao wazazi wametegana au wamefariki) wamepitia katika njia hii na mwisho wa siku wamefanikiwa na wametoka!

Usikate tamaa - ila nakushauri kama umefikia kiwango cha kwenda chuoni basi punguza idadi ya wanaume - au kuwa na mmoja ambaye anaweza kukusaidi all the way up..

Pole sana once again!

Narudi shambani!

kipindi cha palizi eeh?
pole sana Mcharuko..what a sad story
 
pole mcharuko pole sana mdogo wangu.ushauri wangu kwako futa iyo chuki uliyonayo dhidi ya wanaume itazidi kukuumiza nafsi. Jifunze kusamehe na kusahau uliyopitia ili uanze maisha afresh. Kila la heri
 
Basi tusamehe na sisi wanaume tulioponzwa na hayo mabaradhuli yaliyokufanyia undava!!!
Yupo mtu kanieleza kuwa kuna Yaliyopita, yaliyopo na yajayo
sijui kwa yajayo lakini kwa sasa sielewi labda nionane na wataalam
wa saikolojia kama nilivyoelezwa lakini kiukweli michango mingi imenipa
moyo kiasi cha kupata hisia za mabadiliko ingawa si sana.

Unajua Asprin Kuna mengi sijayasimulia hapa ambayo na mimi nimeyafanya
lakini kutokana na ukatili wenu ndo nimekuwa hivyo. Kuna wakati tulikuwa
tunawawekea dawa wanaume wakilala tunawaibia chochote walichonacho
kwa usalama wangu na wenzangu sipendi kutoa mifano zaidi juu ya hili.
 
saikolojia inaonyesha kuelezea yoote yaliokusibu umekwisha pona kabisaaa!
POLE SANA DADA YANGU IMENISIKITISHA!
 
Nimeacha, kuna kipindi nilifanya Field sehemu fulani nilimweleza yule
mama mkurugenzi wa pale mambo ninayokabiliana nayo katika maisha
alilia sana. Akajitahidi kunifanyia mpango ambao umenisaidia mpaka sasa
kuachana kabisa na biashara hiyo. Hivi ninavyozungumza ninasimamia
biashar a za huyo mama!

Pole sana jamani,story yako kweli imenisikitisha plz anza kuwa na positive altitude kwa sasa,anza kuwa na urafiki na watu ambao watakupa mawazo ya maendeleo kama huyo mama,achana kabisa na contact za hao watu wa zamani,usijilazimishe kupenda wanaume kwa sasa hiyo hali itatoka taratibu na utapata akupendae kwa dhati na kukuheshimu,pia anza kuwa na mawazo ya kuwa wewe si mcharuko bali ni kiumbe mzuri wa mungu
Anza kwa kubadili ID yako na kujipa jina positive
 
-Anza kwa kuomba toba kwa Muumba wako uachane na dhambi ya kujichukia wewe mwenyewe pamoja na kuwachukia wanaume.
-Anza kujithamini wewe mwenyewe kwanza ujione kuwa ni wa thamani mbele za Mungu! Kataa aina yoyote ya unyonge ndani mwako, ukijiweka ktk unyonge kuwa wewe ni yatima basi utabaki ktk unyonge hivo hivo. Mungu wetu anaitwa "Mungu wa WAJANE na YATIMA"
-Tunza mwili wako kuwa ni HEKALU la ROHO MTAKATIFU hivyo usiruhusu kitu chothote kile kiunajisi.
-Usianze kuhangaika kutafuta upendo wa kweli kwa sasa...huu utakujia wakati muafaka pale ambapo utaweza kujipenda na kujithamini wewe mwenyewe pamoja na kumtumainia Mungu wako katika kila kitu....
-Jifunze kujisemea maneno mazuri wewe mwenyewe kwa kuwa "mauti na uzima vimewekwa katika uwezo wa ulimi wako". (Mithali 18: 21)
 
pole sana dada lakin kuna msemo ya kuwa no matter how long the 9t mite be, bt morning wil come. Mim nakushauri utafte chanzo kngne cha mapato ktakacho kuwezesha kusoma. Not all men are like that lakn kwa sasa most men are. Nina hakika unaweza change ucfkiria sana kuhusu yaliyo pita angalia yaliyoko mbele haya maisha yako na wewe ndiye dereva dadangu
 
Back
Top Bottom