Kwanini nawachukia wanaume?

Kwanini nawachukia wanaume?

Pole sana, inaonekana uliweka mbele sana shida zako kuliko utu wako. Ni Kweli ulikuwa na hali ngumu kimaisha lakini ungejitahidi kupata njia nzuri yakutatua matatizo yako kuliko kutumia mwili wako. Wapo Wanaume wastaarabu ambao wanaweza kumsaidia mtu bila kuwa na wazo la ujira wa ngono. Ni wakati wako kusahau yale yote mabaya uliotendewa na kuichukia tabia yako ya kuutumia mwili wako kama kitega uchumi kisha chagua maisha yanayo mpendeza mwenyezi mungu na uhakika utafanikiwa.
 
Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!
 
wanaume tunapaswa kushawaishiana 'kuchukia'
tabia za ku take advantage unapomuona msichana ana shida na kaja kwako umsaidie...
Halafu Boss such incidents zinatokea sana sema wengi wanaona aibu kutoka mbele na kusema na hawana guts za kusema.
 
Ha;afu Boss such incidents zinatokea sana sema wengi wanaona aibu kutoka mbele na kusema na hawana guts za kusema.

watu tunapaswa kujifunza kupiga vita haya mambo...
leo dada wa mwenzio ,kesho dada yako.....
 
wanaume tupo poa sana.mwanamke ukikosa upendo wa mwanaume ni sawa na maua yasiyo mwagiliwa maji.pole sana.mia

Hata mimi nawachukia mademu ila kutokuwa nao ndio shida siwezi kabisa. Umesema unawachukia wanaume lakini unapenda sex. Hata ungekuwa changudoa kivipi, kuna mmoja utakuwa unamrudia mara nyingi na huyo utakuwa unampenda kidogo. Kwa hiyo naona kama ni contrdiction kusema unapenda kuwapa uroda lakini huwapendi.

Uko chuoni kwa sababu pengine ya uchangu doa, kwa hiyo ndio waliokufikisha hapo sio? Unawapenda .

On the other hand, watu wengine wanapata psychological problems hasa pale wanapogundulika utundu wao ambao wangenda iwe siri . Kwa hiyo wanajiexpress this way kumaintain balance. Otherwise hii story umetunga tu. "He who hates a man hates his/her father too"
 
Pole mamii, nikisikia hizi story huwa naanza kuwafikiria wanangu, hivi siku nikitoweka ktk uso wa dunia hii itakuwaje, ooh! God help them. Mcharuko endelea kumuomba Mungu tu, chamsingi komaa na shule ndio itakayokutoa, kuhusu kupenda ipo siku utapenda utakapompata anaekupenda kwa dhati. God be with U.


Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?
 
moyo wangu umeniuma kama vile nina jipu....pole sana!!

Naomba ubadili hii ID yako mpendwa!!! Hustahili hata kidogo kujiita hivi...
 
Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!

Ni ngumu sana kupima kutokana na historia ila siku ukipata nguvu ukapima utakuwa huru sana my dear, kumbuka kuwa sio lazima kabisa uwe nao saa hizi! Sio lazima kabisa aisee, ukiweza kupima itakuwa poa sana ila najua ugumu uliopo, hata ingekuwa mimi sijui kama ningepima, upime kwani unaumwa nini kwanza?
 
Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!
Najua ni ngumu hasa ukianza kufikiria lakini piga moyo konde na fanya maamuzi magumu kwenda hospitali ili ujue afya, i know it ain't that easy but sometimes inabidi ufanye maamuzi ambayo yanaweza kukuumiza au yanaweza kuwa na manufaa kwako na kwa mwingine hapo baadae
 
watu tunapaswa kujifunza kupiga vita haya mambo...
leo dada wa mwenzio ,kesho dada yako.....
Ndio maana Mungu ni wa ajabu sana laiti kama ungekuwa unajua mwenzako anafikiria nini sijui ingekuwaje au tungeishi vipi?
 
unawachukia wanaume kwa kuwa na wewe walikuchukia maana waliona unajirahisisha ili upate mahitaji yako nao wakakutumia! nahisi wewe ulianza uhuni mapema ukiwa mtoto na bahati mbaya uhuni wako umekomaa! ina maana hukuwahi kupata akili nyingine zaidi ya kuuza uchi wako?! I am not supporting you!
 
Tatizo sitamani tena kuwa na mwanaume, sina uhakika kwa siku
za mbele lakini nahisi kuwa ni jambo ambalo limefutika katika akili
yangu! Nasikia aibu na ndo maana kabla ya kupost hii thread
nimeamua kufungua ID mpya kwanza kwani ile ya kwanza kuna
watu wananifahamu!

kwa hali hiyo ya kuona aibu naamini unakaribia kuachana na tabia hizo
usijali huko mbele yote yatakuwa sawa

Pole sana mshirikishe zaidi Mungu
 
Kwanza nakusihi achana na hiyo biashara ya uchangudoa kazania shule lakini Mpendwa ukipima ndo utaishi kwa amani, nenda kapime, ujue afya yako bado mapema, ila ukikutwa ni +ve plz, plz usilipe kisasi kwa kuwaambukiza watu kwa makusudi, ni dhambi kubwa mbele za Mungu.

Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!
 
Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!

Mbona ni kawaida kuogopa kupima HIV? Kumbe shida sio chuki bali ni matokeo ya kupenda kupita kiasi. Yaani wengi mno halafu nyama kwa nyama? Wewe kapime tu , Hauko peke yako kwenye hilo la HIV. BTW machangudoa hujilinda wasipate magonjwa wakashindwa kupiga kazi. Wewe Vipi?
 
Nimeacha, kuna kipindi nilifanya Field sehemu fulani nilimweleza yule
mama mkurugenzi wa pale mambo ninayokabiliana nayo katika maisha
alilia sana. Akajitahidi kunifanyia mpango ambao umenisaidia mpaka sasa
kuachana kabisa na biashara hiyo. Hivi ninavyozungumza ninasimamia
biashar a za huyo mama!
Mcharuko, hiki kisa kimeniuma sana. Pole sana kwa yote.
Nimefarijika kusikia umewacha na angalau unapo pa kushika. Ninachokushauri hapa ni kuwa MWAMINIFU kwa huyu mama na chapa kazi kama kwamba biashara za huyo mama ni za kwako.
Kabla ya post hii, nilifikiria bado umo na nilikusudia kukushauri UWE MWANGALIFU na gonjwa. Maisha ya m'mke anayejiuza ni magumu: vipigo, kudharauliwa, kulazimishwa kutenda asiyotaka ikiwemo kutotumia kinga n.k. Shukuru Mungu kuwa umefika hapo bado ukiwa salama. Bado ninakushauri uwe mwangalifu sana. Ninakutakia kila la heri.

Tatizo sitamani tena kuwa na mwanaume, sina uhakika kwa siku
za mbele lakini nahisi kuwa ni jambo ambalo limefutika katika akili
yangu! Nasikia aibu na ndo maana kabla ya kupost hii thread
nimeamua kufungua ID mpya kwanza kwani ile ya kwanza kuna
watu wananifahamu!
Bado ni mapema sana. Maumivu waliyokuwachia yatachukua muda kufutika. Katika kipindi hicho, uzoefu utakusaidia kuchagua nani anafaa, siyo kwa bla bla bla zao bali vitendo. Mtu mwema haonekani kwa maneno yake wala vitendo vya muda mfupi bali upendo, asiyehitaji fidia kwa msaada wake. Naamini iko siku utapenda na utapendwa. Ni haki yako.
Kwa mara nyengine:
POLE SANA (kwa past yako)
HONGERA SANA (kwa present)
KILA LA HERI (katika future).
 
Pole Mcharuko, nafikiri ulivyoweza kujitambua ni hatua nzuri sana. Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufika hapo ulipo (chuo), tumia vyema nafasi uliyoipata. Ni vyema ukatafuta sasa washauri wa mambo ya saikolijia ili wakupe mbinu za kuachana na tabia hiyo. Pia anza kujaribu kuwa na marafiki wa tofauti na wale wa awali (yaani wale mliokuwa mnaenda pamoja ktk uchangudoa). Usisahau kumwomba Mungu. All the best.
 
Pole sana kwa masahibu yaliyokukuta na jitahidi kujikwamua kupitia elimu na huo uwe mwanzo wa kupaa juu kieleimu. Hata hivyo dubwana linaloitwa binaadamu(both wanaume na wanawake) ni la ajabu. mwanaume mmoja ni tofauti na mwingine na vivyo hivyo kwa wanawake. Toka watimuliwe kule paradiso maisha yao ni ya mashaka, yasiyoaminika na yasiyotabirika. Wewe yamekukumba hayo lakini kuna wanaume nao wanakumbwa na vitimbwi vikubwa kutoka kwa wanawake! Lakini hayo yote yanatokana na utashi na silka ya mtu binafsi na si tatizo la kijinsia km ambavyo unataka jamii iamini hivyo. Kama wanawake wote wangekuwa malaika kiasi hicho, matukio ya watoto kutupwa chooni ama kutelekezwa porini baada ya kuzaliwa yasingekuwepo! Tatizo ni udhaifu wako wa kushindwa kuthubutu na kuamini kuwa, licha ya changamoto zilizokuandama, ulikuwa na uwezo wa kukabiliana nayo head-on, bila ya kutegemea msaada wa hao wanaume fisadi. Ungekuwa na ujasiri huo leo hii ungekuwa unaongea mengine, kwani kuna wanawake waliokabiliana na makubwa kushinda hayo, lakini kwa jitihada zao na baraka za mwenyezimungu, walijinasua bila kujidharirisha. Mwisho hujakutana na mwanaume wako na uliokutana nao ni wafanyabiashara wa ngono ambao kwao wanapotoa ngawila wanachotegemea ni huduma - si mapenzi!! Tafakari.
 
Back
Top Bottom