Nchi za Waarabu za Saudi Arabia, Qatar, UAE, Kuwait, Oman na Bahrain ni nchi tajiri sana, hazina madeni na zina akiba ya matrilioni ya pesa kutoka kwenye mafuta na gas inayozihifadhi katika soverign wealth funds zao.
Familia za kifalme zinamiliki ukwasi wa matrilioni. Pamoja na haya hizi nchi wachoyo sana na hawafanyi hisani kabisa za maendelo, sijawahi kuona msaada wanaotoa kwa nchi masikini za Afrika zaidi ya kujenga visima vya maji viwili/ vitatu na kugawa msaada wa tende.

Friday, May 31, 2013
Saudi Arabia yatoa msaada wa dola milioni 24 kwa Somalia
Na Abdi Said, Mogadishu
Kampeni ya Kitaifa ya Saudia kwa Kuwasaidia Watu wa Somalia imeahidi kutoa mfuko wa msaada wa kina wenye thamani ya dola milioni 24 kwa miradi ya ujenzi mpya nchini Somalia, kwa mujibu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), ambao unasaidia kuratibu fedha hizo.
Msaada huo utakwenda kwa mikoa yote ya Somalia na utaelekezwa katika sekta za elimu, afya, kilimo pamoja na kuwarekebisha watu waliokimbia makazi yao na katika hali zote za ustawi wa jamii, OIC ilisema katika taarifa hapo tarehe 12 Mei.
Wigo wa mfuko wa misaada na ushirikishwaji wa asasi zisizokuwa za kiserikali, wazee wa kikabila, tawala za mikoa na serikali ya shirikisho katika kuamua miradi gani ya kutekeleza inaashiria mtindo mpya wa utoaji misaada nchini Somalia.
Lengo la msaada huu ni kukuza ujenzi mpya wa Somalia kupitia miradi kadhaa inayoungwa mkono na Saudia, ambayo itaanza katikati ya mwezi wa Juni, alisema Mohamed Idle Sabrie, naibu msimamizi wa ofisi ya OIC mjini Mogadishu.
Kiasi cha watu 500,000 watafaidika na msaada wa fedha, ambao utakamilika ndani ya miezi 18. Awamu ya kwanza itazingatia miradi ya mjini Mogadishu, Sabrie alisema.
Maeneo yenye uhitaji wa dharura kabisa yatachaguliwa kwanza, alisema. "Mwanzo tunataka kujua mahitaji katika wilaya na vitongoji ambavyo tutatoa misaada kwa ajili yao," aliiambia Sabahi. "Kwa mfano, wilaya [ambayo tayari inayo] shule mbili na hospitali hazitapata msaada sawa na wilaya ambayo haina kitu."
"Hasa tutawasaidia watu waliokimbia makazi yao kwa kuwawekea programu ambayo itajumuisha kuwapa chakula, dawa, elimu [na huduma nyengine]," alisema.
Serikali ya Somalia itashauriana na tawala za mikoa kuhusu utekelezaji wa programu zinazohusiana na mfuko wa msaada, kwa mujibu wa Sabrie, na shughuli ya uzinduzi itafanyika mara tu miradi itakapokuwa tayari kuanza kazi.
"Tutaweka tukio kubwa la matangazo na tunatarajia maafisa kutoka serikali ya Saudia, OIC na serikali ya Somalia kushiriki," alisema. "Ingawaje tangazo hilo lilikuwa lifanyike muda mrefu uliopita, kulikuwa na uchelewaji wa kufika kwa ujumbe wa Saudia kutokana na Shambulio la tarehe 5 Mei kwa ujumbe wa Qatar, ambapo ilihitajika kuhakikisha usalama kwanza."
Mohamed Sheikh Nur, mkuu wa utawala wa idara ya uhusiano wa utawala wa mpito mkoa wa Jubbaland kwa mashirika yasiyokuwa ya faida, aliukaribisha mfuko huo wa msaada.
"Ni ishara nzuri kwamba serikali ya Saudia inawaonesha watu wa Somalia jitihada zake za kutusaidia," Nur alisema. "Watu wa Kismayu wana mahtaji makubwa ya imsaada huu. Huduma za afya, elimu na upatikanaji wa chakula ndio masuala yenye shinikizo zaidi ambayo mradi huu utatusaidia."
Jijo Aadan,mwenye umri wa miaka 35 na mama wa watoto watatu ambaye anaishi katika kambi ya Tarabun kwa ajili ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu, alisema kuwa alikuwa amefurahi kusikia kuhusu msaada wa kibinadamu kutoka Saudia, lakini bado alikuwa na wasiwasi kadhaa.
"Nina imani kuwa tutapata sehemu yoyote ya msaada ambao Mungu ametujaalia," alisema. [Lakini] ningependa kuishauri [OIC] kuhakikisha kuwa watu waliochaguliwa kusimamia miradi hii sio watu mafisadi ambao hawatawasaidia Wasomali wenye shida."
Sabrie alisema kuwa watu wa Somalia kwa muda mrefu walikuwa wanalalamika kwa usimamizi mbaya wa miradi ya misaada wakati wa njaa ya mwaka 2011. Ili kuepuka matatizo kama hayo, alisema, "Tutafanya safari za usimamizi endelevu kwenda kila eneo ambalo tumetekeleza [programu yetu] ya msaada, na hakutakuwa na ufisadi."
"Ingawaje mahitaji yote hayataweza kufanikiwa kikamilifu, naamini kwamba mradi huu utaleta tofauti kubwa sana katika maisha ya watu wa Somalia," alisema.
Chanzo - sabahionline.co