Kwanini nchi ya "Mozambique" tuliamua kuuita "Msumbiji" tofauti na nchi zingine za jirani zinazopakana na Tanzania zilizobaki na majina ya Kiingereza?

Leo ndiyo ninajua Job kwa kiswahili ni Ayubu...
 
Nimemuuliza mtoa mada ili ajue kwamba kiswahili ina namna yake ya kuita nchi na nchi
Mkuu, afrika ya kusini na south africa si unaona kuna tafsiri ya moja kwa moja kati ya kiingereza na kiswahili tofauti na mozambique na msumbiji?
 
Mzizima kuwa Dar es Salaam!!!!!
 
Sijui kwanini hatuiiti hivyo, lakini hata kama tungeiita Ingilandi sio mbaya. Je, unajua asili ya jina Msumbiji?
Na ndio maana lugha ni makubaliano yenye lengo la kuleta kuelewana, kama Minister tumeona tumuite waziri na speaker tumeona tumuite spika hayo ni makubaliano yetu baina ya watumiaji wa lugha, usiulize kwanini minister hatujamuita minista, otherwise hiyo ni sawa na kusema kwanini ugali haukuitwa wali, well inawezekana, ni suala la makubaliano tu, kwamba kuanzia leo mtu akisema ugali anamaanisha chakula kitokanacho na mchele, na mtu akisema wali anamaanisha chakula kitokanancho na unga wa mahindi, ni suala la kukubaliana tu ili maelewano katika mazungumzo yawepo ili kukamilisha mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…