Kwanini nchi yetu hairuhusu watu kulipwa kwa Paypal? Kuna sababu gani ya msingi?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wandugu kwanini Tanzania hawaruhusu watu kupokea malipo kwa Paypal, njia rahisi kabisa?

Siku hizi kuna kazi nyingi sana mtu unaweza kufanya mtandaoni. Ni wewe tu na bando lako na simu yako au Kompyuta yao. Unaweza kufanya kazi ipo US au kokote duniani. Na njia rahisi ya malipo ni kupitia paypal. Kuna wengine wanablogs na sites zingine ambazo wanapiga pesa. Na kote huko njia rahisi ya malipo ni Paypal. Lakini hii njia haifanyi kazi Tanzania.

Kuna sababu gani ya msingi?
 
Hiki suala inabidi waziri wa biashara alitolee ufafanuzi mzuri.
 
Nadhani hata PayPal nao hawapo nchi zote kimalipo ila serikali yetu ijiongeze kwa kasi ya technology ili wananchi wake nao wafaidike kama kule India na Nigeria.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Tatizo huwa tunahisi Tanzania ni taifa teule, yaani halihitaji maingiliano na mataifa mengine. Ni uoga wa bure kuogopa paypal wakati nchi zingine zinatumia, na maisha yanasonga. Lazima Watanzania tujue, hii Dunia ina nchi nyingi sana, tumeikuta, na tutaiacha.
 
Wandugu kwanini Tanzania hawaruhusu watu kupokea malipo kwa Paypal, njia rahisi kabisa?

Siku hizi kuna kazi nyingi sana mtu unaweza kufanya mtandaoni. Ni wewe tu na bando lako na simu yako au Kompyuta yao. Unaweza kufanya kazi ipo US au kokote duniani. Na njia rahisi ya malipo ni kupitia paypal. Kuna wengine wanablogs na sites zingine ambazo wanapiga pesa. Na kote huko njia rahisi ya malipo ni Paypal. Lakini hii njia haifanyi kazi Tanzania.

Kuna sababu gani ya msingi?
Wanataka upokee kwa njia ya M-Pesa labda [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], utani tu,
Anyway vp kuhusu kulipa? Mana mimi mwaka 2016 nilipa mtu kwa njia ya Paypal, je kuna mabadiliko ama? Nilihamisha pesa kutoka Bank Account yangu (EQUITY) na kupeleka kwenye Paypal account yangu then nkafanya malipo. Sijui kwa sasa kama kuna mabadiliko
 
Sijajua kulipa kwa paypal, lakini tatizo la kulipa nje halipo kabisa. Mfano Visa ya equity inalipa bila maneno. Hata mpesa mastercard inafanya malipo vizuri. Shida ipo kwenye kupokea pesa.
 
Usilaumu sana. Teknolojia inakwenda kwa kasi kuliko uwezo wetu wa kufikiri ndio maana bado tupo zama za mawe. Maana hili jambo lilishaongelewa sana lakini ikabaki stori tu.
 
Sijajua kulipa kwa paypal, lakini tatizo la kulipa nje halipo kabisa. Mfano Visa ya equity inalipa bila maneno. Hata mpesa mastercard inafanya malipo vizuri. Shida ipo kwenye kupokea pesa.
Hapo nimekupata mkuu, sikujaribu kama naweza kurudisha pesa kutoka paypal account yangu kwenda kwa Bank Account. Nitajaribu ili niwe na ushahidi binafsi
 
Wanataka upokee kwa njia ya M-Pesa labda [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], utani tu,
Anyway vp kuhusu kulipa? Mana mimi mwaka 2016 nilipa mtu kwa njia ya Paypal, je kuna mabadiliko ama? Nilihamisha pesa kutoka Bank Account yangu (EQUITY) na kupeleka kwenye Paypal account yangu then nkafanya malipo. Sijui kwa sasa kama kuna mabadiliko
Kulipa inawezekana lakini kupokea uwezi
 
Nadhani awamu ya sita na zijazo zitafungua milango...maana awamu ya Tano ilibana Sana financial transaction kwa kigezo Cha pesa chafu ...BOT wakipush itaruhusiwa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sio paypal pekee bali hata skrill huwezi pokea pesa.
Nchi yeru bado iko nyuma sana katika malipo ya kimtandao hasa hii ya kimataifa

Skrill inafanya kazi mkuu,kutuma na kupokea.Nimelink kadi ya kibongo na inakubali kutuma na ku withdraw bila tatizo
 
Back
Top Bottom