Hii ni kutokana na post uloisoma nyuma kukatazwa kwa milio ya simu. Lakini ukajisifia kuhusu "mambo yetu yale", ni jinsi gani inavoonesha ulivyokuwa akili mchungwa kwa kuona faghari watu wakidhalilishwa mbele ya camera, sijui dini yako ndo inavofundisha ivo? Ili nikupe elimu kidogo sababu za kukatazwa izo ringtone ni pale kuwa lengo la Quran halifikiwi. Quran inatakiwa isomwe na isikilizwe. Unapoweka ringtone maana hupotea kabisa, ikilia lengo lako sio kuisikiliza bali lengo lako ikushtue kuwa simu inaita na ubaya zaidi, kupokea simu kabla aya haijamaliza, ni kupoteza maana totally.
Mtoa mada, nikuulize, KENYA inaaongozwa na sharia nayo? Na wewe nikuelimisha, hakuna nchi inayohukumu kwa kutumia sharia law kikamilifu ndio maana ukaona hakuna amani, vipi amani itakuwepo kama kuna dhulma? Katika uislam sheria inamgusa kila mtu, leo nambie lini mfalme wa saudia akaguswa na sharia? Sharia si kwa wananchi tu, bali ni kwa watu wote mpaka kiongozi, na kitu chengine ni mfumo wa kuwepo kwa vyama, na kuwepo kwa rais ambae dini haijui. Soma historia ya Dola za Kikhalifa. Katika zama za ukhalifa ilifikia wakati hakuna ata maskini wa kupewa sadaka au Zakka, pia kulikuwa na system ambayo, kama unavoona mailbox lile la barabarani, wakati wa dola ya kiislam ilikuwepo kwa ajili ya kuwekwa pesa, mwenye shida huenda akachukua kiasi akitakacho, lakini pia hakupatikana wa kuzichukua kwa sababu hakukuwa na mwenye shida ya mali, na watu walikiwa wakiishi na amani kabisa. Hakuna nchi yoyote inayohukumu kwa sharia law, sharia ya kiislam inataka kiongozi awe KHALIFA (sio raisi au mfalme) tena awe anaijua dini juu chini chini juu, anachaguliwa kwa shuraa (mashauriano) sio uchaguzi kama huu wa ccm na cuf, tena sio kila mtu anamchagua bali wenye elimu ya dini ya hali ya juu yaani maulamaa. Sharia inamtaka Khalifa ahakikishe kila mtu anapata milo 3 ya kushiba uhakika kabla yeye kiongozi mwenyewe hajashiba. Wapi duniani leo kuna dola ya kiislam? Kasomeni Islamic Caliphate mjifunze