Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
1._ Ukweli ni vyema tukautamka hadharani bila ya kujiumauma.
Ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni ukweli usiofichika ya kuwa tumechokwa kwa sababu tumekuwa tukipinga kila hatua ambayo ndiyo msingi na sababu ya kuanzishwa Jumuiya hiyo.
2. Sababu ya kuanzishwa Jumuiya mbona tumeiweka kando?
EAC ilianzishwa ili kuziunganisha nchi za ukanda wa mashariki mwa afrika ili ziwe na sauti kubwa katika uendeshaji wa dunia kwa msingi mmoja tu "umoja ni nguvu" lakini sisi na werevu wetu kama upo wa tambo za tuna ardhi na na maliasili lukuki na kwamba kujiunga na wenzetu tutafukarika huku tukujua hatuna nyenzo za kunufaika na yale yote ambayo Muumba katupatia.
Ukizifanyia kazi kwa undani ngonjera zetu utabaini kuna upotoshaji wa khali halisi na huku wageni wanajiporea ardhi na maliasili nyinginezo bila ya shari au zengwe lolote lile ili mradi wenye nafasi serikalini wapoozwe kwa ulaji wa bei poa.................Ama kwa uhakika, wajinga ndiyo tuliwao!
3. Kama ardhi tunayo mbona migogoro ya ardhi imetuchachamalia?
Wanandugu ni vyema tukawa wazi yawaje kila kukicha tunakatana viwiliwili kisa ni mapambano ya umiliki ardhi kati ya wafugaji na wakulima ukiachilia mbali uvamizi wa maeneo ya wazi, miliki za barabara na hifadhi za mbuga zetu ambazo kwa pamoja zinathibitisha ardhi siyo nyingi kama tunavyojigamba na haipaswi kuwa kikwazo cha kulisukuma gurudumu ndani ya EAC.........................
4. Kama Jumuiya hatuko tayari nayo mbona tunawakwaza wenzetu ambao wako tayari?
Muungwana anapoona hana ubavu na jambo fulani huwaruhusu washiriki wenzie waendelee siyo kujitetea ya kuwa anasubiri........"kulimwa talaka."
Huu ni utetezi wenye lengo la kuonyesha hatupendwi kumbe hatupendeki kutokana na misimamo yetu ya kukwamisha utekelezaji wa malengo ya msingi ya kuanzishwa kwa EAC............................
5. Mfumo wa Kupiga kura ndani ya EAC ni lazima ugeuzwe kulinda masilahi ya wengi wape!
"Wengi wape" ndiyo njia pekee ya kuinusuru EAC na mfumo uliopo wa kila nchi inaweza kupiga "kura ya veto" itasababisha EAC kufa kama kile kifo chake cha mbwakoko 1977.........................kama nchi yetu yenye utapeli lukuki haitaki suala la ardhi na maliasili kuwa sehemu ya EAC basi turuhusiwe kuwa mwanachama asiyelazimishwa kushiriki katika maamuzi fulani fulani lakini nasi tusiwe kikwazo cha kuwaruhusu wenzetu kuendelea kufanikisha maamuzi ya EAC...........That is what I call a fair deal to all!