najaribu kutafuta jibu rahisi na sahihi
Na akikuuliza hivi utamjibuje? baba.. na mimi nikiwekewa mabawa na mtambo wenye nguvu na kasi naweza kuruka hadi marekani?
Of Cozi mwananngu wewe utakuwa bingwa !! Tutakufungia mitambo miwili mgongoni yennye kupuliza hewa na kukurusha juu na kupaa hadi utakapo!! Sasa ona mfano wake.............Na akikuuliza hivi utamjibuje? baba.. na mimi nikiwekewa mabawa na mtambo wenye nguvu na kasi naweza kuruka hadi marekani?
Swali la kitaalam jibu lake huwa ni la kitaalam kama unataka jibu rahisi basi mjibu ni uwezo wa Mungu muumbaji wa vyote, vinavyoelea, vinavyotambaa na vinavyopaa.
Aulizaye anataka kujua, hebu saidia huyu mtoto anauliza ....Baba...baba..kwanini ndege inaelea angani? Mwenye kujua jibu asaidie hapa.
cha kutambua ni kuwa miracle does not exist only your ignorance is miracle.
ndege inavyoruka ni jambo rahisi sana ni kitu kinaitwa "up lift force"
hebu angalia tiara kama unaijua imetenngenezwa kwa mkunjo fulani sasa unapoivuta kwenda mbele kwa kasi ile hewa mahali tiara inakopita inakuwa ni kama upepo unapita kurudi nyuma. sasa ule msuguano kati ya tiara na upepo kutokana na ule mgongo uliojikunja kama kuinuka juu kuna nguvu inatokea ya kuelekea juu na hiyo ndiyo inainua tiara.
ndege hivyo hivyo mabawa yake yametengengezwa kwa mgongo kama wa tiara hivyo injini zinaposukuma ndege kwenda mbele kwa kasi ule mgongo wa kwenye mabawa kutokana na msuguano na hewa unatengeneza uplift force.
hivyo ndege ina injini ambazo zinaisukuma kwa mbele na ile kasi inatengeneza nguvu ya mwinuko katika mabawa.
Duh kweli haya ndio ya kumwambia mtoto?
Kasome Bernoulli's Principle of Aerodynamics, Newton's third law of motion in relation to rocket /jet propulsions na combustion.
Baada ya hapo naamini utaelewa kwanini ndege inapaa
Asante mkuu kwa faida yangu pia niliipenda sana physics, bt chemistry ilinitupa mbali test ya kwanza 4m 1 nilipata 5/100
Unadhani mtoto atakuelewa kweli?