Kwanini ndoa nyingi za Bomani (Serikalini) zina Afya 'Kimahusiano' kuliko zile za Makanisani mwetu?

Ndoa za kanisani ni za show off mtu mpaka anafunga ndoa bomani wengi ni watu makini na maisha yao wanafunga ndoa kwa ajili yao ila kwa wakanisani wanafunga ndoa kwa ajili ya watu wanaowazunguka wanaowazu
 
Masuala ya ndoa ni kutanguliza Mungu tu ndugu yangu. Stability ya ndoa haina kanuni maalum aidha iwe bomani ama kanisani. Yaaani ni kama vile baadhi wa watu wanavyoamini eti ndoa za watu wa kipato cha chini hudumu zaidi kuliko za matajiri kitu ambacho si kweli hata kidogo.
 
Hapo (colored) is surely ila NDOA za kanisani sijui msikitini ni matatizo makubwa, pamoja na ibilisi kuzinanga kwa nguvu ili azisambataratishe ila zinaongoza kwa matatizo ukiondoa ile show off.
 
Ngoja nimtafute Mrembo hapa hapa JamiiForums ili nikafunge nae Ndoa ya Bomani ( ya Serikali ) ili niishi kwa Afya, Amani na Furaha na hiyo ya Kanisani nawaachia tu wengine.
Kwasababu kule kwingine kuna kaudanganyifu fulani "...alichokiunganisha Mungu binadamu hawezi kukitenganisha" hiyo statement inawapa jeuri wanawake kwamba hawawezi kuachika, matokeo yake wanakuwa wasumbufu na jeuri kupita kiasi mwisho wa siku wacha mbwai iwe mbwai

Wale Katiba wanakuwa na hofu fulani ...hakuna guarantee
 
ndoa za bomani (serikali) hazina influence ya watu, dini, wapambe, wazazi, marafiki n.k... ndoa za bomani zinafungwa na maamuzi ya dhati ya hao wapendanao, hazinaga hulka na mihemko na zinashirikisha watu wachache sana sana. Tha's why zinadumu.
 
Lile swali la ndoa yako itakuwa ya mke mmoja au wake zaidi ya mmoja nadhani ndio linasababisha hivyo kwenye ndoa za serikali
 
Ndoa zote hizi iwe umefunga kanisani au msikitini Vibali vinatoka serikalini

Sasa tafakari... na cheti kina toka serikalini hapo una weza tafuta jibu zaidi...

Walifunga misikitini zenji Au makanisani watakutana na nembo kubwa ktk cheti imeandikwa SMZ

Huku Tz bara kana mchungaji/askofu aliwahi ulizwa na mamlaka kuwa kibali cha kufungisha ametoa wapi???

Hivyo ufungishi tu ndoa kienyeji kuna sheria na taratibu za nchi kwa ustawi wa jamii
 
Kwanza ungeweka uwiano wa idadi ya Ndoa zinazofungwa Mahakamani,kanisani na msikiti ilituone tofauti yake.
Maana kama uwiano wa ndoa zifungwazo mahakamani ni sawa na uwiano wa Ndoa 2 kwa siku ukilinganisha na Ndoa 1000 kwa siku kwa upande wa Dini,basi bado Ndoa za Dini zinaongoza pia kwa kudumu.
 
Ngoja nimtafute mrembo hapa hapa JamiiForums ili nikafunge naye ndoa ya Bomani ili niishi kwa afya, amani na furaha. Hiyo ya Kanisani nawaachia tu wengine.
kwani sheria inasemaje? Au mpaka kifo kiwatenganishe, na kuongeza mke wa pili vipi wanaruhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…