Kwanini ng'ombe anatoa maziwa yanayokuwa kama maji?

Mynd177

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2022
Posts
2,817
Reaction score
5,141
Habari wanajukwaa la kilimo na ufugaji,

Tafadhali rejea kichwa cha mada.

Ng'ombe hapa nyumbani siku za karibuni amekuwa akitoa maziwa ambayo kwa kweli ni kama maji, hayana uzito wowote na hata ukiyachemsha hayana ladha yoyote ni kama maji.

Jambo hili limepelekea mpaka wateja kulalamika kuwa tunawawekea maji, jambo ambalo hatujawah kufanya.

Naomba kujuzwa tatizo litakuwa nini? Je, ni ugonjwa? Na kama ni ugonjwa suluhu ni ipi?

Natanguliza shukrani.
 
Pole sana kwa hilo tatizo, kusema ukweli kwanza mshirikishe Vet anaemwangalia, na pili kama alivyo sema mjumbe mmoja hapo juu madini, maji safi, virutubisho, josera,maklik, jiwe, pumba, mashudu ya alizeti,mashudu ya pamba,soya nakadhalika vitakusaidia kumbadili utoaji wa maziwa. Shirikisha mtaalamu wa mifugo Vet.
 
Nenda duka la dawa za mifugo. Kuna madini pamoja na vitamini amekosa kwa muda mrefu. Utakapoanza kumlisha hayo. Madini na kumpa chakula kizuri hali itabadilika.
Nathamini sana kwa mchango wako nitaufanyia kazi ushauri wako.
 
Pole sana kwa hilo tatizo, kusema ukweli kwanza mshirikishe Vet anaemwangalia, na pili kama alivyo sema mjumbe mmoja hapo juu madini, maji safi, virutubisho, josera,maklik, jiwe, pumba, mashudu ya alizeti,mashudu ya pamba,soya nakadhalika vitakusaidia kumbadili utoaji wa maziwa. Shirikisha mtaalamu wa mifugo Vet.
Nathamini kwa mchango wako,nitaufanyia kazi.
 
Aina ya majani anayokula hasa akila majani ya migomba kwa wingi
 
Pamoja na mambo mengine tafuta group za wafugaji wa ng'ombe wa kisasa
Wenzako wapo huko wanabadilisha live changamoto za ng'ombe wa maziwa
Na kule hata Vets wapo wa kutosha
Tafuta taarifa simple you will move
Follow the link kama utapata nafasi jiungapo

Ahsante mkuu ngoja nijiunge kutakuwa na meng ya kujifunza huko!
 
Habari wanajukwaa la kilimo na ufugaji,

Tafadhali rejea kichwa cha mada.

Ng'ombe hapa nyumbani siku za karibuni amekuwa akitoa maziwa ambayo kwa kweli ni kama maji, hayana uzito wowote na hata ukiyachemsha hayana ladha yoyote ni kama maji.

Jambo hili limepelekea mpaka wateja kulalamika kuwa tunawawekea maji, jambo ambalo hatujawah kufanya.

Naomba kujuzwa tatizo litakuwa nini? Je, ni ugonjwa? Na kama ni ugonjwa suluhu ni ipi?

Natanguliza shukrani.
Pole labda utujuze kdg unafanya zero grazing na majani unamlisha aina moja maana anatakiwa kupa full balance diet crued protein wanga vitamini na madini
 
Habari wanajukwaa la kilimo na ufugaji,

Tafadhali rejea kichwa cha mada.

Ng'ombe hapa nyumbani siku za karibuni amekuwa akitoa maziwa ambayo kwa kweli ni kama maji, hayana uzito wowote na hata ukiyachemsha hayana ladha yoyote ni kama maji.

Jambo hili limepelekea mpaka wateja kulalamika kuwa tunawawekea maji, jambo ambalo hatujawah kufanya.

Naomba kujuzwa tatizo litakuwa nini? Je, ni ugonjwa? Na kama ni ugonjwa suluhu ni ipi?

Natanguliza shukrani.

Nyasi gani mnazo mpa.tumia pumba ya mpunga laini wakati inakobolewa.

Ila na nyasi nazo za kuangalia.sio kila nyasi inatoa maziwa mazuri
 
Pamoja na mambo mengine tafuta group za wafugaji wa ng'ombe wa kisasa
Wenzako wapo huko wanabadilisha live changamoto za ng'ombe wa maziwa
Na kule hata Vets wapo wa kutosha
Tafuta taarifa simple you will move
Follow the link kama utapata nafasi jiungapo

Samahani mkuu, unaweza tuma tena hii link ili niweze kujiunga maana hii haikubali.
 
Back
Top Bottom