Kwanini ni makosa kupiga picha Treni ya Usafiri wa Treni?

Kwanini ni makosa kupiga picha Treni ya Usafiri wa Treni?

MRMARTIN5000

New Member
Joined
Oct 3, 2026
Posts
4
Reaction score
4
Jana nilikua naenda kariakoo kutoka Mbagala tulivyo fika kwenye reli kulikua na treni inapita ya kawaida ya Zamani nikataka kupiga picha mtu mmoja akaniambia hiyo simu yako kama hauipendi endelea kuchukua video maana ita chukuliwa sasahivi, lakini kisa hiki si cha kwanza kama mnavyojua ukienda sehemu unahitaji kumbukumbu.

Nilisha kwenda Bukoba sehemu moja inaitwa Cha Mkwikwi kuna gati ndogo ya maboti yaendayo visiwa mbalimbali.

Nilivyo taka kupiga picha pia nilionywa na mlinzi Suma (JKT) sasa nikawaza haja gani mtanzania hapaswi kupiga picha rasilimali anazo lipia kodi?

Naombeni uelewa na ushauri wenu wakuu
 
Back
Top Bottom