Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
KWANINI NI MBOWE NA SIO LISSU NA KWANINI CHADEMA HAIFI?
Mchakato wa Uchaguzi wa Chama Taifa umeanza, na tayari Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Ndugu Tundu Lissu amejitokeza kutangaza nia nia ya kuwania Uenyekiti Taifa, Ninakubaliana kwamba Tundu Lissu ni kiongozi mzuri mwenye misimamo mikali, ni kiongozi mweledi sana, Lissu ni Mwanaharakati wa asili katika maisha yake tangu hajawa mwanasiasa, kwa haraka unaweza kusema Lissu anafaaa kuwa kiongozi, Lakini si kiongozi mwenye sifa ya kuongoza taasisi hasa taasisi ya kisiasa na kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa. Achiliambali aligombea Urais 2020, Lisu anafaa kuwa kiongozi kwenye mazingira flani tu sio kiongozi wa kisiasa wakati wote, Hivyo Mazingira ya kisiasa ya wakati huo wa Magufuli yalimfaa akawa mgombea urais.
Ukiniuliza mimi, kwamba uamuzi wa Lissu kugombea Uenyekiti Taifa ni uamuzi uliotoka moyoni mwake? Nitakuambia HAPANA, Si uamuzi wake, bali ni uamuzi unaosukumwa kutoka nje ya Chadema wenye malengo “ovu” na Chadema pengine bila Lissu mwenyewe kujua. Kwamiaka mingi sana dola ilihangaika sana kuvuruga upinzani lakini uimara wa Mwenyekiti na Makamu ulifanya dola ifeli, Lakini safari dola hii imefanikiwa sehemu flani, Twende taratibu tutaelewana, Ni hivi, Yako makundi mawili yanayoratibu/yaliyoratibu uamuzi huu wa Lissu, Kundi la kwanza linaongozwa na Wanaharakati chini ya Mariam, Huyu amekuwa mtu hatari kwa Chadema kwa miaka mingi, amefanikiwa kuharibu future ya vijana wengi wa chadema hasa wale wanaoingia chadema kwa mtindino wa Harakati, Huyu ndie aliratibu na kumjaza kibri Zitto Kabwe enzi hizo kwakumrubuni na kujifanya mshauri wake na kumsaidia kusajili Chama cha ACT, Huyu hajawahi kuipenda chadema hata siku moja, na sasa kafanikiwa kumrubuni Lissu agombee uenyekiti chini ya mwavuli wa Harakati vikao vingi sana vimefanyika Nairobi, Ndoto yake ni kuona chadema inaanguka. Dola inasukuma kete kwa uangalifu sana!
Kundi la pili ni Watanzania waishio nje ya nchi maarufu kama Diaspora, hawa tangu waliposaidia matibabu ya Lissu, basi Yeye Lissu ametokea kuwaamini kupitiliza wamekuwa washauri wake wakuu, na kuna kipindi walitaka kupindua Chama kupitia mwamvuli mikutano yao kupinga uwekezaji Bandarini nk, Walifika hatua wanaomba Chadema iandae mikutano ili wao waje wahutubie lakini wanaweka sharti kwamba zusiwepo Bendera za chadema, Yaani wanatoa maagizo wao kwa viongozi wetu wa mikoa na wilaya, Bahati nzuri tukawastukia tukawapiga marufuku kutumia jukwaa la chadema, wakakosa jukwaa la mikutano wakabaki Club House na kuanza kuendesha matusi kwa mwenyekiti taifa, Pia kuna Mwanaccm anaitwa Peter Msigwa huyu ndie kiunganishi cha dola na mambo yote ya kuhujumu Chadema yanapita kwake, Anaaminika sana na Lissu pengine kuliko mtu yoyote. Hawa ndio wamemuingiza Lissu kwenye 18 za sintofahamu wakati siku 60 tu nyuma alikuwa ametangaza nia ya kuombea nafasi ya makamu mwenyekiti na alishaandika barua kwenda kwa katibu mkuu! Dola inajicho na mbinu nyingi, hatimaye imenasa!
Lakini hoja ni je, Lissu kugombea uenyekiti ni kharamu? Jibu ni kwamba sio kharamu ni haki yake na ana sifa kikatiba, Nilichoeleza hapo juu ni uthabiti wa dhamiri yake ya ghafla ya kugombea uenyekiti ilihali “alijiandaa” kugombea umakamu mwenyekiti kwakutangaza hadharani na kuandika barua kwendavkwa Katibu Mkuu, pili ni lugha na matamshi yake dhidi ya chama na viongozi wenzake yanaashiria safari yake mpya, na sasa ni mwelekeo wa tukose wote yaani tuvunje mtumbwi kabisa! Sasa ameingia anagombea uenyekiti, Hatuna budi kuingia kwenye uchaguzi, nitamchambua kwanini hafai kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, ziko sababu nyingi nitakazo zieleza hapa;
1) Lissu hajawahi kuitumikia kikatiba na kisheria nafasi yoyote ya kiuongozi aliyowahi kushika ndani ya Chadema, Mfano, Lissu alipojiunga Chadema mwaka 2004 aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Sheria wa Chama taifa, Lakini nafasi hiyo hakuifanyia kazi yaani hakuhudhuria vikao vya chama muhula wote hadi Chama kilipoamua kumpa Wakili Kibatala nafasi hiyo, Kitendo hicho kilimfanya Lissu kufika kamati kuu na kulalamika kwamba mbona kanyang’anywa nafasi yake’ Hivyo kwa Busara ya Chama Kamati Kuu ikampa cheo kingine cha Mwanasheria Mkuu wa Chama Taifa, Cheo ambacho HAKIKO KWENYE KATIBA YA CHADEMA, Hii yote chama kilifanya kama kumlinda tu. Sasa anawezaje kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa mtu wa aina hii?
2) Akiwa anatumikia cheo cha Mwanasheria Mkuu wa Chama, cheo ambacho hakiko kikatiba wala hakina majukumu rasmi, Chadema ilikuja na utaratibu wa Kanda kichama, Hivyo Lissu akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kati, Tatizo la Lissu liliendelea lilelile kutoitumikia nafasi yake, Miaka yote aliyoshika cheo cha Uenyekiti wa Kanda ya Kati, hakuwahi kuitisha kikao chochote wala kujenga chama katika kanda hiyo zaidi ya mikutano jimboni kwake tu, hali iliyopelekea Kanda ya Kati kufa, Ndipo kamati kuu ya chama ikaingilia kati, (kidiplomasia zaidi) ikamshauri achie cheo hicho mtu mwingine, Sasa mtu wa aina hii anawezaje kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa?
3) Kama hiyo haitoshi Chadema kikaendelea kumbeba, Chama kikampa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa, Tena kuonyesha Chama kinamjali na kumthamini, alichaguliwa akiwa hayupo ukumbini kwakuwa alikuwa yuko kwenye matibabu Ubelgiji, Nafasi hiyo hadi leo hii hajaitumikia kwa mjibu wa katiba, hajafanya kikao chchote tangu achaguliwe 2019 huku jukumu lake kubwa kikatiba akiwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Chama Taifa, Mashauri mengi yamefika ofisini kwake lakini yameshindwa kushughulikiwa, Hata tuhuma ambazo yeye ndie mlalamikaji ameshindwa kuzifanyia kazi kama katiba inavyotaka. Sasa mtu wa aina hii anawezaje kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa?
4) Lissu amekuwa sio mkweli mbele ya Wanachama (Muongo), Hili linadhihirishwa katika mambo kadhaa, (A) Mara kadhaa amesimama hadharani akitangaza kuwa Chama chetu hakikupata chochote katika maridhiano na serikali, na hili amekuwa akimtumu waziwazi mwenyekiti kwamba alikosea, izingatiwe kuwa uamuzi wa kuingia kwenye maridhiano haukuwa wa Mwenyekiti binafsi bali wa Chama kupitia Kamati Kuu ambako Lissu ni mjumbe wake. Ukweli wa macho ni kwamba katika maridhiano yako mambo tulifanikiwa kuyapata kama chama, na kama Taifa, na yako mambo tuliyakosa tunaendelea kuyadai. Mambo tuliyoyapata katika maridhiano ni; 1. Shughuli za kisiasa kwa maana ya Mikutano na Maandamano ya vyama vya siasa ilifunguliwa, 2. Wafungwa wa kisiasa waliachiliwa. 3. Kesi za kisiasa zilifutwa. 4. Wanasiasa waliokuwa uhamishono walirejea nchini akiwemo Lissu, 5. Wafanyabiashara walioporwa pesa zao katika akaunti zao za bank walirejeshewa, 6. Mh Tundu Lissu alilipwa mafao yake yote ya Ubunge.
Mambo tuliyoyakosa Katika Maridhiano kati ya Chadema na Serikali ni Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi, Tume ya Uchunguzi wa Mauaji na Utekaji, Tume ya Maridhiano na Hoja ya Kubadili sheria ya vyama vya siasa, na nyingine. Sasa mtu unayejitambua na umenufaika kwanza wewe binafsi na maridhiano hayo unapata wapi kusema uongo hadharani kwamba Maridhiano hayo hatukupata kitu? Huu ni uongo wa wazi kwa kiongozi mkubwa kama Lissu unamuondolea sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa.
5) Lissu amekuwa muongo kwakutuhumu viongozi wenzake majukwaani akiwaambia wamehongwa mabilioni na Abdul, Hoja hii ameisema katika majukwaa na katika vyombo vya habari, Ifahamike yeye ndie mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya chama, Lakini Lissu hajawahi kuitisha kikao na kushughulikia jambo hilo zaidi ya kwenda hadharani kinyume na katiba ya chama na kuanza kutuhumu viongozi wenzake, ieleweke, moja ya miiko ya kikatiba kwenye chama chetu ni rushwa, ambapo kosa hili ukibainika nalo unafukuzwa kabisa uanachama. Sasa baada ya kelele zake kuwa nyingi Chama kiliamua kuingilia kati, kikamtaka aeleze ndani ya vikao, akashindwa kueleza kwa ushahidi. Ndipo mmoja wa viongozi wa andamini akaomba kukifafanulia chama kuhusu undanu na ukweli wake hiki kinachoitwa rushwa ya Abdul kwa viongozi wa Chadema,
Kiongozi huyo akaeleza mbele ya Lissu kwamba yeye kama mfanyabiashara na mtu maarufu nchini ana urafiki na Abdul, kwakuwa Lissu alikuwa akilalamikia sana serikali kwamba pesa ya matibabu hajalipwa ambayo ni haki yake kwamjibu wa kanuni za Bunge, Hivyo kiongozi huyo aliona azungumze na Abdul ili asaidie serikali imlipe Lissu, Abdul akamuuliza je huyo Lissu anazo nyaraka? Akajibiwa anazo, Ikabidi kiongozi huyo amoigie Simu Lissu kwamba kuna mtu anaitwa Abdul atasaidia alipwe pesa zake, wakapanga miadi wakutane wote nyumbani kwa Lissu, baada siku kadhaa Kiongozi huyo akiwa ameambatana na Abdul wakafika nyumbani kwa Lisu wakamkuta akiwa na msaidizi wake Bwana Djumbe, hivyo kikao kikawa cha watu wanne, ambapo Abdul alimuomba Lissu nyaraka zake zote za madai ya matibabu na akamwambia azitume kwa email, zikatumwa kikao kikaisha kiongozi yule na Abdul wakaondoka zao!
Sasa wiki kadhaa baadae wakati mchakato wa malipo hayo ukiendelea chini ya Abdul, Lissu akagundua kiongozi yule aliyempeleka Abdul kwake, amemgeuka hamuungi mkono kwenye agenda zake kadhaa za mbeleni, Lissu akaamua kumzushia kwamba kiongozi huyo alimpekeka Abdul kwake ili amhonge mamilioni ya pesa na kwamba ana ushahidi wa cctv kamera za kikao, ndio akaamini amemshika pabaya kwakuwa ana video za kikao ambazo kwa ujanja wame mute sauti, Kashifa hii ikawaunganisha na viongozi wengine wengi akiwemo Mwenyekiti kwamba wamehongwa. Bahati mbaya Lissu nyaraka alizituma kwa email hiyo ni ushahidi tosha kwamba kikao kile kilihusu nyaraka hizo na sio vingine. Kiongozi huyo alizungumza kwa ushahidi wa wazi. Baada ya kiongozi huyo kumaliza kuongea, Chama kikamgeukia Lissu kujibu hoja, akakataa kujibu akisema yeye alishasema, Kilichofuata nikuwa Hoja ya Mabilioni ya Abdul na Mama yake sasahivi Lissu anaikimbia haisemi tena popote kwakuwa uongo wake umebainika wazi, Sasa mtu wa aina hii anawezaje kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa?
Mimi sitampa kura yangu!
6) Sababu ya sita inayomnyima Tundu Lissu sifa ya kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa ni ya kiuchumi, Duniani kwa modern politics pesa ni silaha muhimu ya kuiendesha taasisi ya kisisa, Ifahamike Chadema kwa sasa ni chama kisisa kilichotayari kushika madaraka ya nchi, Sio kikundi cha harakati, bali chama cha siasa ambacho utendaji kazi wake unahusu dialogue, convincing, and black-mailings, mambo hayo yanahitaji pesa sio maneno wala harakati, tena pesa utoe mfukono mwako kwakuwa chama chetu hakina ruzuku ya maana, milioni miamoja na hamsini ya ruzuku hata kuhudumia makao makuu tu haitoshi, hivyo lazima uwe na misuli ya uchumi ili uwalipe wataalamu niliowaeleza hapo juu. Zingatia wataalamu hao juu hawawezi kuwa wanachama wengi unawapa tenda unawalipa. Sasa Lissu kwa sasa hajarejea vizuri kwenye utumishi wake wa Uwakili nchini, anaishi kwakutegemea misaada ya wahisani hasa Diaspora, Chama kinaingi kwenye uchaguzi mkuu mwakani, itakuwa ni masihara kutegemea mwenyekiti wa aina hiyo awaingize kwenye uchaguzi kwakutegemea ruzuku ya milioni mia hamsini. Hivi tu sasa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi huu ikiwa utafanyikia Dar bajeti yake inafika Bilioni 1, na ikiwa utafanyikia Dodoma angalau bajeti inaweza kuwa milioni 800 hivi, Muulizeni Lissu anaweza kuchangia shingapi bajeti hii? Zitto kakimbia kuongoza chama chake sio kwamba anapenda bali kakimbizwa na uchumi, kakaa pembeni na remont anamwelekeza yule mama tu, Kuongoza chama lazima uwe na pesa zako mfukoni sio za mfuko wa mtu. Mimi sitampa kura yangu!
SASA NINI KIFANYIKE?,
Mimi Yericko Nyerere, nitamshawishi Mh Freeman Mbowe achukue fomu ya kuogombea uanyekiti Taifa tena, Na nitailipia mimi fomu yake ya kugombea uenyeti Taifa. Kwanini ni Mbowe tena? Hebu Naomba tumtazame Mbowe kama kiongozi wa Kisiasa na mafanikio yake katika ardhi ya Tanzania na kwanini bado Siasa inamhitaji kwa udi na uvumba. Sitawarudisha nyuma sana, bali tuutumie utawala wa Magufuli kama mfano hai katika hoja kuu ya andiko hili, mtakubaliana nami kuwa Rais wa nchi Hayati Magufuli aliapa kwa maneno yake kufuta upinzani nchini huku Chadema kikiwa na Wabunge zaidi ya 70 bungeni, Wengi walichukulia kama maneno raihisi tu ya majukwaani, lakini ile ilikuwa kauli ya kirais (decrees), na utekelezwaji wake ulianzia na kila mtu alishuhudia siasa za upinzani zikipigwa marufuku hadi zilipofunguliwa Januari 2023.
Chadema kama Chama Kikuu cha Upinzani nchini kinachokaribia kushika madaraka, kimepitia kanuni kuu ya asili ya Chama cha siasa kinapokuwa hatari kwa Serikali na Chama tawala ambayo ni “kujaribiwa kuuawa/kufutika”, hilo hutokei chama kinapokuwa kikubwa na kinauwezo wa kushika madaraka ya nchi. Chama chochote nje ya hapo hakiwi hatari kwa vyovyote vile, yaani kinakuwa kachama kama kijiwe cha kisiasa au kachama tumbo tu. Sasa ili dola iweze kuviua vyama vya siasa vyenye nguvu ambavyo vinatishia kushika madaraka, inatakiwa mambo makuu mawili iyatende; Mambo hayo ni, kwanza, Dola itaua uchumi wa viongozi wa vyama hivyo, hapa ndipo unawakuta akina Lipumba, Kadawi, Mbatia, Dovutwa, Zitto na wengine, kwamba ukiwa na chama kinachofanana na hawa wewe sio threat kwa dola kwakuwa wanabei tena bei elekezi, yaani hawana utajiri wa pesa na hawana biashara yoyote zaidi ya biashara ya siasa tu. Chadema na Mbowe wamevuka eneo hilo.
Jambo la pili, ili dola iue chama cha siasa chenye nguvu ya kushika dola ni lazima ipandikiza mawakala wa ujasusi wa kidola ambao kazi yao itakuwa ni kumgombanisha Mwenyekiti na Katibu, chama chochote ambacho mwenyekiti na katibu wanaongea lugha moja huwa hakivunjiki haraka hata kama utafanikiwa hatua ya kwanza pale juu ya kuharibu uchumi binafsi wa mwenyekiti wa chama. Chadema na Mbowe wamevuka eneo hilo. Sasa mpaka hapo mtakuwa mmenielewa uimara wa chama cha siasa cha Upinzani unahusu Uchumi wa Kiongozi wa chama hicho na Umoja na mshikamano baina ya Katibu na Mwenyekiti.
Hatua za kujaribu kukiua chadema zilianza mbali kipindi cha Utawala wa JK, ambapo Dola ya JK ilijaribu kumtumia Amani Walid Kabour ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, lakini kwa uimara wa Mbowe chadema haikufa, Dola ya JK haikuridhika ikaja na mbinu nyingine kumtumia Zitto Kabwe, lakini kwa uimara wa Mbowe chama kilibaki salama, na Wakati wa Utawala Magufuli dola ikamtumia Katibu Mkuu Dr Slaa kujaribu kukiua chadema lakini akaondoka yeye na mchumba wake tu, lakini kwasababu ya uimara wa Mbowe, Chama kilibaki salama. Magufuli akaweka tangazo rasmi la kirais kwamba atafuta upinzani nchini,
Kwanza Magufuli akapiga marufuku shughuli za kisiasa kwa vyama vya siasa vya upinzani nchini ambazo ziko kikatiba na kisheria, hili lilikuwa pigo la kwanza kwa siasa na demokrasia nchini. Hatua ya pili ilikuwa ni wapinzani kusulubiwa kwa mkono wa mahakama, hili limeshuhudiwa uwingi wa wapinzani nchini katika mahakama za nchi nzima na kila aliyekosoa utawala wa Magufuli alionja mahabusu, Mbowe ni mmoja wao,
Hatua ya tatu ikawa ni kununua wapinzani huku utekaji wa kisiasa ukishamiri, wanasiasa wengi wa upinzani wakashindwa kuhimili, wakajisalimisha mikonini mwa dola na chama dola wakitafuta usalama wao kisiasa, wengi wakazawadiwa vyeo na madaraka, Lakini Mh Mbowe akakataa katakata kupiga magoti kwa watawala na kukiua Chadema sawa na ilivyouawa CUF, TLP, NCCR Mageuzi nk. Eneo hili liliondoka na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Vincent Mashinji akaenda kudhalilishwa kwa kupewa u DC mtu aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama kikuu cha Upinzani nchini
Hatua ya nne ikawa kuwaondolea uchumi viongozi wa vyama vya upinzani na wote wenye mrengo tofauti na utawala, hapa Mbowe akiwa ndio mlengwa na aliathirika zaidi kuliko mtu yoyote, kwenye hatua hii ndio watu wetu wengi uzalendo kwa wananchi uliwashinda wakaamua kujisalimisha hata Hayati Edward Lowasa aliyekuwa mgombea wetu urais ambae umma ulimpigia kura zaidi ya milioni sita, alishindwa kuhimili kibano hiki akakimbia kujisalimisha ccm. Mbowe akawagomea.
Kwa Mbowe walianza na kuharibu mashamba yake kule hai alikokuwa amewekeza zaidi ya 6 billions akiwa ni mfanyabiashara wa pili barani afrika kwakuuza mboga na matunda katika soko la ulaya, hapa akiwa nyuma ya Uhuru Family wanaoongoza kwa Afrika. Mradi huu uliharibiwa kutoka kwenye bilioni 6 hadi kuwa sifuri kabisa kwa hoja za kijinga kwamba analima kwenye vyanzo vya maji, kumbuka mradi huo ulikuwepo tangu kabla ya Uhuru wa Tanganyika ambapo mzee Aikael Mbowe baba wa Freeman ndie mwasisi na watu wamazingira walikuwepo hawajawahi kutoa sababu hizo, mradi huu uliajiri zaidi ya watanzania 2,600, na mradi huo ulilipa kodi ya zaidi ya 3 billions kwa mwaka, watu wote hawa wakakosa kazi na serikali ikakosa kodi, Mbowe akagoma kuhama chama na kuuza chama.
Mbowe akaharibiwa biashara yake nyingine ambayo ni klabu ya starehe Bilicanas iliyokuwapo mtaa wa mkwepu posta jijini Dar es Salaam, kwa hoja za ajabuajabu klabu yenye mtaji wa karibu 8 billions iliyoajiri Watanzania zaidi ya 200 na inayolipa kodi zaidi 2 billions kwa mwaka, ikavunjwa, yaani sio kuvunjwa tu kwamaana ya kuifunga, bali ikavunjwa kabisa na jengo kanakwamba kuna ujenzi unaanza, lakini mwaka wa tano huu pamebaki mbuga ya kuoshea magari na kuegesha nagari tu. Mbowe huyuhuyu hakutikisika,
Baada ya hapo Mh Mbowe akiwa bado imara, akaamua kwenda kuanzisha mashamba huko Morogoro akawekeza zaidi ya 6 billions, tena ni kilimo cha umwagiliaji, huwezi amini kufumba na kufumbua mashamba yake yote yakiwa na mazao, yalifyekwa yote huku msimamizi aliyekuwa diwani akiuawa kwa utata, hoja zao ni zilezile nikwamba amelima kwenye vyanzo vya maji, Mbowe huyuhuyu hakutikisika, Mbowe akagoma kupiga magoti akabaki na Chadema,
Wakaona haitoshi, akaunti zake zote zikafungwa, sio kufungwa tu bali zikachukuliwa pesa zote zaidi ya 6b katika akaunti zote 4 alizopoteza, yaani wakataka abaki mchangani kabisa, Mbowe akasimama wima hakutikisika akagoma kuuza chama, Lengo lote ni kuhakikisha Chadema inaanguka, na ili kuiangusha inabidi umuangushe Mbowe kiuchumi na kimedani. Unaweza kuona dhamira na machaguo ya dola kwamba haijalishi unachangia pato la taifa kwa kiwango gani bali ni kuhakikisha upinzani unakufa Tanzania
Wakaja na mkakati wa kimahakama, wakacheza nae mahabusu weee kesi ya mauaji ya Akwilina aliyeuawa na Polisi, lakini mshitakiwa akawa ni Chadema (Viongozi) kwakinachoitwa maandamano bila kibali huku mlengwa ni Mbowe, Mbowe akafungwa na wenzake na kulipa faini ya Milioni 350, kisha akakata rufaa mahakama Kuu akashinda. Baada ya kuona kila mbinu inafeli, wakaamua kumuundia jaribio la kumuua kule Dodoma ambako pia waliwahi kujaribu kumuua Mh Tundu Lissu. Kwa Mbowe katika purukushani wakamvunja miguu yote miwili.
Hali ikawa mbaya wakati tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu 2020, Katika kujihakikishia Usalama, Mbowe akaona atafute ulinzi binafsi wa watu wenye mafunzo imara, na chaguo likawa atafute wanajeshi wastaafu au walioacha kazi serikali, Akawapata makomandoo wanne, Dola baada ya kuona sasa Mbowe ana ulinzi wa Makomandoo wakamfuata Mbowe kwa mdomo wakimtuma Mkuu wa Polisi Kinondoni kipindi hicho Ramadhani Kingai, kwamba saaa tunakubambikia kesi ya Ugaidi hautachomoka.
Kama masihara kweli Walinzi wa Mbowe wakakamatwa wakiwa kazini na kubambikiwa kesi ya Ugaidi na kisha wakamuunganisha Mbowe kwamba alifadhili ugaidi huo kwa laki sita pale alipo kuwa akiwatumia pesa hiyo ya kununulia nguo (suti) ili wapendeze wakiwa wanamlinda. Kesi iliendelea baada ya Dola kuona inakwenda kudhalilika mbele ya dunia kwakuwa jumuiya za kimataifa zilikuwa zikihudhuria kesi hiyo, Dola ikaamua kuifuta na Rais Samia akaomba azungumze na Mbowe ikulu, na huo ndio ukawa mwanzo wa kile kinachoitwa Maridhiano. Kwa nadharia ya kawaida Mbowe ameweza kusimama imara dhidi ya Taasisi hii, Tukiruhusu jaribio lolote la kuiangusha taasisi hii ni ushindi kwa maadui, na hilo Mbowe amekataa kata kata.
Ndani ya mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu shughuli za kisiasa zifunguliwe Jabuary 2023, Mbowe ameingia mtaani kujenga Chama kupitia Chadema Digital mguu kwa mguu nyumba kwa nyumba, na kuendesha oparesheni nchi nzima, chama kikafufuka, kwa miaka 7 ambayo shughuli za kisiasa za upinzani zilifungwa, chama kilikuwa kimefutika kwenye mitaa, akakifufua mitaa yote nchini, Chama kilikuwa hakina uhai katika Kata, akakifufua na kupata uongozi katika kata zote nchini, Chama Kikafanya chaguzi za Mitaa, Kata Wilaya na Majimbo, Chama kikafanya chaguzi za Mikoa na Kanda, Chama Kikashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji kwa kusimamisha 98% ya Wagombea nchi nzima japo Dola ilikuja kuwakata wote na kubaki 34% tu. Kubwa zaidi kwa miaka mingi Chama hakikuwa na Jengo la Ofisi yake Makao Makuu, Mbowe amesimamia Ruzuku ya Chama na Kununua Jengo la Ghorofa Mikocheni eneo ambalo linathamani kubwa ya ardhi nchini. Hii ni hatua muhimu kwa Chama kinachojiandaa kushika Dola. Kwahiyo hoja za maccm kuwa Chadema haina ofisi akaiua rasmi.
Nampa saluti kubwa sana ya Ukombozi Kamanda Mbowe, Mbowe anaijua siasa, Mbowe anahekima, anashaurika na anaheshimu taaluma na wataalamu. Mhimu zaidi vijana wa Taifa hili tujifunze, siasa sio kama ibada za kanisani au msikitini ambako mila na destuli huaminiwa na kufuatwa.Tunaposhiriki siasa za kisasa tunashiriki kwakutumia akili ya juu sana sio asili ya juu. Wanachadema uchaguzi ni wetu, Tukilinde chama chetu, tusiruhusu dola iue chama kwamtego huu uliopo mbele yetu, tusimame wima kumlinda Mbowe na taasisi yetu iwe salama!
Mimi Yericko Yohanesy Nyerere, Nitamchagua Freeman Aikael Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa!