Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Yericko Nyerere punguza chuki Kwa Lissu.

Yaani pesa za Mbowe ndio zinazompa uhakika wa kuendelea kuwa Mwenyekit wa chama.

Hii NI aibu,,

Umezungumzia ruzuku tu na kuonesha kwamba haitoshi kuendesha chama, hujataja kabisa ada za wanachama na michango ya wadau Kama marehem Mzee Sabodo.

Swali langu Kama ruzuku haitoshi na mnamtegemea Mbowe kujazia fedha za mfukoni mwake je hizo hela Mbowe anakikopesha chama au vipi?

Kwa mazingira hayo ya kutegemea fedha za Mbowe si ni dhahir chama ni cha Mbowe?
 
Hii ni thesis?
 
Wewe yericko wa ajabu, Andiko lako limeegemea kwenye kuonesha ni kwa namna gani Mbowe hatakiwi kutokuwa mwenyekiti wa CDM na zingine hizo ni blah blah. Ni nani nchi hii asiyeheshimu harakati za mbowe kuijenga CDM? Kupingwa kwenye uenyekiti haimaanishi hatuthamini mchango wake, tunamaanisha “we thank him for his service” Wengine wapewe nafasi watufikishe mahali pengine.

Baadhi ya waTz mna tatizo la kuwapenda viongozi kimapenzi, Mpenzi ndiye hana mbadala, ni ajabu kutuonesha kuwa nafasi ya mwenyekiti haina mbadala.

Yericko mnafiki sana wewe, na kudhihirisha unafiki wako hautakuja kujibu comment hata moja humu. Kama ulivyotueleza strength za Mh. Mbowe kwenye uongozi, tuchambulie na udhaifu wake kiuongozi.

Haya Lissu hafai, tunaomba mbadala mwingine ambaye si Mbowe! Mbowe amefanya vingi apumzike, Kama sivyo hata CCM imefanya vingi iendelee kupewa nafasi sivyo?
 
..hela za kugeuka uwe Fala bora kufa masikini.
 
Shangaa heti hawa ndo walikua wanapinga JPM akimaliza miaka kumi hasiogezewe mda Mungu anajua kuwaumbua wanafiki Kenge nyinyi
 
Kuna siku mambo haya yatakuja kujulikana hadharani kuwa FAM alihusishwa/ alishirikishwa katika mpango wa kumpiga risasi TAL.
 
Baada ya miaka 20 ya uongozi chini Mbowe pamoja na mafanikio mengi hana kipya cha kuonyesha, zaidi anajenga udumavu na watu wasiotaka mabadiliko kama Yeriko hapa.

Ushahidi wa kwamba Mbowe hana kingine cha kuongeza zaidi ya kupunguza nguvu za CHADEMA ni tendo hili la aibu kwa chama kikuu cha upinzani kutoa tuzo kwa Mwenyekiti wa chama tawala miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Lissu ataeneelea kuwagaragaza kwenye hoja zake.
Pesa anazopaswa kulipwa kisheria kwa utaratibu wa kiserikali mlitaka mlipane kwa nyuma ya Mlango?

Mtu asiyeshughulika na watekaji na watesaji lakini mna mahusiano mazuri tu kwa jina la Kujifanya Wafanyabiashara?
Wanachama wanatekwa wanapotea na serikali haichukui hatua yoyote lakini unataka Lissu achukue pesa zao kwa nyuma ya Mlango?

Lissiu ni Mtumishi wa Mungu hatangulizi maslahinyake binafsi mbele ya Watanzania.
Na kwa hakika Hoja za Lissu umezithibitisha kuwa ni za kweli.
 
Kwa miaka 20 Mbowe hajawahi pata mshindani wa kweli, Lissu awepata joto, hapa kuhusu dhamira ni hisia zinaongea, Lissu katangaza nia wote tumeona, hajasemewa na mtu.
Chadema kama Chama Kikuu cha Upinzani nchini kinachokaribia kushika madaraka, kimepitia kanuni kuu ya asili ya Chama cha siasa kinapokuwa hatari kwa Serikali na Chama tawala ambayo ni “kujaribiwa kuuawa/kufutika”,
Chama kikuu cha upinzani kikampa tuzo chama tawala, kwa mtu yoyote hata asiyemwanachama wa chadema hii move Mbowe alifeli.
 
Kama hafai kugombea urais waliona anafaa? Unataka kutuaminisha kuendesha nchi inahitaji mtu dhaifu na kuendesha chama inahitaji mtu imara kama mbowe? Je wanaweza kutomba radhi eatanzania kwa kumdimamisha lisu?
 
Kwaiyo aendelee na Uenyekiti hadi kufa kwake au?? Watu mnataka mabadiliko lakini nyinyi hamtaki kumbadili Mwenyekiti,,,mbona Mtei mwanzilishi alikaa miaka 5,,Makani pia miaka 5,,,,, Kwanini huyu baada ya miaka 20 ,hamsemi inatosha. Jambo gani ambalo hajafanya miaka 20 atalifanya miaka 5 ijayo,,,,,,,Lissu ni wetu pia tumkabidhi Chama arudishe morali ya wana CDM
 
Ukute nyie ndo watekaji!! Chadema mngekuwa na Akili mngepigania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Katika watu ambao CDM ilitakiwa iende nao kwa staha basi TAL. yani anachukua fomu mnajidai kama hamumuoni na mbowe naye anachukua mnaenda kwenye uchaguzi mnamchagua mbowe. Hapo Lissu anakuwa kwenye mtego wa demokrasia inabidibakaushe.


Lakini Lissu akishindwa kwa kujua kwamba kuna vijana walitumika kumchafua mitandaoni(walitumwa na walilipwa na nani?) Basi watakuwa wametengeneza mpinzani mkubwa wa chadema ndani ya chadema...balaa kubwa hilo. Mwisho ni chama kufa


NB: Wananchi wengi wanamuamini zaidi Lissu kutokana na aliyopotia na wengi aliojitolea kuwatetea bure mahakamani...kumpiga vita ni kuwakwaza wananchi na hapo ni zitaanza zile kelele za chama cha kaskazini sijui n.k

I thought chadema were smarter... 😭
 
kwahiyo mbowe akifariki leo chama kitakufa?
maana naona shida yako sio lissu, shida yako ni mbowe abaki madarakani, maana yake wewe binafsi pamoja na mamilion ya wanachama hakuna mwenye uwezo wa kuongoza. Na kama tafsiri yako ni hiyo, basi uongozin wa Mbowe umefeli na haujawahi kuwa na succession plan.
 
Huna akili
 
Mbowe ameshatangaza kugombea nafasi ya uenyekiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…