Kwanini ni Mbowe na sio Lissu na kwanini CHADEMA haifi?

Baada ya miaka mingi kupita, leo Wacha na Mimi nichangie kidogo kuhusu yanayoendelea Chadema.

Ukitaka mabadiliko lazima uoneshe Nia ya kubadilika na si kuendelea kufanya mambo Yale yale. Wananchi wengi wamekatishwa tamaa na namna upinzani unavyokabiliana na serikali dhalimu ya CCM.

Kuna matukio mengi yamefanyika kutoka mwaka 2015 Mpaka leo ambayo yamerudisha nyuma Ari na morali ya wananchi kushiriki katika demokrasia na kwa kiasi kikubwa wamekata tamaa.

Mtu mmoja ambaye walau ameonesha kuwa na msimamo wa kukabiliana na hali tangu kipindi hicho kwa mtazamo wangu ni TAL. Huyu mtu hakika anaonesha wazi wazi ana Nia thabiti ya kuleta mabadiliko kwani Hana hata chembe ya hofu kwa Yale anayoamini yanaweza kuleta haki.

Nilidhani CDM wameliona hili kama sie watu ambao tupo nje ya CDM vile ambavyo tumeweza kuona. Nashangaa ndani ya CDM hawataki mabadiliko ilhali wanataka mabadiliko ndani ya nchi, hapa tunashangazwa wengi.

Haileti picha nzuri kuona TAL anapingwa wazi wazi na kuanza kuonekana kama ni mtu Baki wakati ameweka rehani uhai wake kusaidia vugu vugu la mabadiliko kupitia CDM.

Wengi tungependa ashike nafasi ya kuu pale CDM tuone namna Gani ataleta mbinu mpya za kukabiliana na CCM.

Mbowe amepata muda wa kutosha na kwa kweli mbinu zake hazijatosha kabisa kukabiliana na CCM ambao wanatumia Dola kuendelea kubaki madarakani.

CDM msichezee fursa hii tena, manalo jukumu la kuonesha Jamii kuwa mnaweza kubadilika kulingana na mazingira na kusaidia Jamii ya Tanzania ambayo imebaki bila msaada kwa ukoloni wa CCM.

Ahsante
 
Ingekuwa ni mtaala curriculum ya Elimu, Mbowe ni mtaala uliopitwa na wakati, ambao lazima uwe revised kukidhi mahitaji ya wakati huu

Lissu ni mtaala au curriculum ambayo inaendana na mahitaji ya wakati.

Mbowe hana jipya bkwa sasa, ni Lissu, ni Lissu mwenye kukidhi mahitaji ya sasa ya CHADEMA dhidi ya CCM .


Umesema uamuzi wa kuwania u Mwenyekiti wa chama hauotoki moyoni mwa Lissu,unatoka nje, Tuambie wewe uamuzi wa andiko lako não ni wako Toka moyoni au umetumwa??


Watu mliozoea kutumwa kutumika ni rahisi kuwafikilia wenzenu não wametumwa wanapofanya jambo flani.

Lissu is there for Leading the party next year 2025.


NI YEYE, NI YEYE, NI YEYE,NI YEYE,NI YEYE
 
Usiwadanganye ikitokea mbowe akaendelea kuwa chaiman watu wataikimbia cdm itakufa

Wewe tunakujua Unafanya kazi ccm
 
Aisee huyu jamaa kumbe ni takataka hivi......hoja zake za kumkataa lisuu za kitoto sana
 
Andiko refu lisilo na maana zaidi ya mpuuzi mmoja kupigania tumbo lake! Nikuulize swali moja tu: nguvu na ushawishi wa chadema ya 2015 ni sawa na chadema ya leo? Anguko hilo nyie wachumia tumbo hamlioni? Mmeshawahi kufanya research kujua wananchi wanakichukuliaje chama kwasasa au mnakaa maghetton na kuandika magazeti ya kupost JF?
Nikwambie: Huku mtaani chadema imepoteza mvuto na ushawishi kwa vijana na wanawake ambao ndo mtaji mkubwa kisiasa...wengi wanakiona kama chama cha wachumia tumbo na shida ilianzia kipindi kile kapokelewa Lowassa na ikawa kubwa zaidi kwenye hayo mnayoita maridhiano ambayo kiuhalisia ni maridhiano ya kuridhisha matumbo ya viongozi tu! Ilifika kipindi Chadema kikawa chama cha kupambana na watetezi halisi wa maslahi ya wananchi na si kupambana na wakandamizaji wa haki hizo! Kwasasa tumaini pekee lililobaki ndani ya Chadema ni kufumua safu nzima ya uongozi hasa kichwani kabisa (mwenyekiti) na mtu pekee anayeweza kuirejesha Chadema ilee anaweza kuwa Lissu labda na Heche ila hao wengine wote wameshaonesha udhaifu wao mbele ya dola na hawaaminiki. Mkitaka kushupaza shingo shupazeni then mtaniambia baada ya uchaguzi wa 2025.
NB: Kuna namna uongozi wa Chadema chini ya FAM unacheza huu mchezo kwa maelekezo ya Lumumba.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…