Kwanini ni muhimu kwenda na fundi akague unaponunua gari? (mambo ya muhimu ambayo watu hawayafanyi wanaponunua magari yao)

Kwanini ni muhimu kwenda na fundi akague unaponunua gari? (mambo ya muhimu ambayo watu hawayafanyi wanaponunua magari yao)

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Ukiachana na mambo ambayo watu wengi wanaangalia wanaponunua magari used ambapo mengine ni madogo. Kuna mambo ambayo huwa ni ya kiufundi zaidi ambayo huwa ni vizuri pia yakaangaliwa. Kwa watu ambao wameshawahi kununua magari na yakawasumbua sana wanaweza kuelewa vizuri zaidi ni kitu gani ambacho nimeandika katika maelezo hapa chini. Asilimia kubwa ya mambo niliyoandika yanahitaji utaalamu kuyajua hivyo ni vizuri ukapata mtu ambaye anauelewa na mambo hayo kama unataka kununua gari.

Nimejaribu kuelezea mambo kadhaa ambayo watu hawayaangalii wanaponunua magari lakini yana umuhimu mkubwa sana. Hebu tuyaone:

1. Gari iliyowahi kupata ajali
Wauzaji wengi atakuambia kwamba gari yake haijawahi kupata ajali hata kama imewahi kupata ajali. Sisemi kwamba mtu asinunue gari ambayo imeshawahi kupata ajali. Ila asilimia kubwa ya gari zilizopata ajali huwa hazifanyiwi maintenance ya Airbags vile ambavyo inatakiwa, Wengi huishia kununua Airbag nyingine na kufunga wakati inatakiwa gari hiyo ibadilishwe Seat belts, PB ignitor pamoja na airbags zake.

Seatbelt huwa ni muhimu kubadilishwa kwa sababu huwa inakuwa na ignitor. Kama hiyo ignitor ililipuka wakati wa ajali basi huo mkanda haufai tena hata unauona unalock ukiuvuta kwa mkono.

Kama utanunua gari ambayo haikubadilishwa vitu hivyo na kuangaliwa upya mfumo wake wa Arbag basi itakuwa ni kama unaendesha gari ambayo haina airbag na hata ukigonga kitu katika speed ya 50 Kph basi unaweza kuondoka kwa sababo airbag haitodeploy na seat belt ni kimeo.

2. Gari isiyowaka baadhi ya taa za dashboard unapoweka Switch ON
Ukiachana na suala la hizo taa kuungua. Baadhi ya watu huzima taa hizo makusudi ili kuficha tatizo fulani katika gari hili. Linaweza kuwa tatizo ambalo linaweza kupelekea uharibifu kwenye gari lako(Hasa engine) au tatizo ambalo linaweza kukusababishia ajali(faults katika safety features kama Airbag na ABS). Pia taa yoyote ya dashboard inaweza ikagoma kuwaka kwa sababu ya faulty iliyopo kwenye circuit ya hiyo taa.

3. Gari ambayo ports zake za diagnosis hazifanyi kazi. (DLC 3 kwa OBD2 na DLC1 kwa OBD1)
Gari ya aina hii unaponunua ukae ukijua kwamba inaweza kukupa ugumu kutambua baadhi ya matatizo pale itakapopata shida kwa sababu hakuna mashine itakubali kusoma ikiwa port hizo zina shida. Hivyo ni vizuri zikakaguliwa hata kama zikiwa na shida ifahamike kama inaweza ikarekebishwa au kama haiwezekani basi ughairi kununua hiyo gari au ununue ukiwa unalijua hilo.

4. Gari ambayo matatizo yake ni ya msimu
Mfano wa matatizo ya msimu ni zile gari ambazo zinasumbua kuwaka wakati wa asubuhi. Au gari ambayo ukitembea nayo kwenye tambarale unaona ni nzima ila ukifika mlimani ndo utajua hujui. Muuzaji anaweza kaa kimya na ww ukatest gari ukaona ni zima. Matatizo kama haya yanaweza kujulikana ikiwa gari itafanyiwa diagnosis kabla ya kununua. Na utatuzi wake unaweza kuwa rahisi kama kubadilia spea au mgumu ikiwa shida ipo kwenye wiring(inategemea).

5. Gari ambayo matatizo yake hayajatengeneza Error code yoyote kwenye control box
Kuna gari ambazo zina matatizo ambayo hayajacreate error code(DTC) yoyote. Kwa maana hiyo gari hata ukienda nalo kwenye diagnostic mashine hutopata code yoyote na itaonesha gari ni zima isipokuwa tu kama mashine mnayotumia inasoma live data na anayekupimia awe anajua kuanalyse hizo live data.

Mfano wa matatizo ya aina hiyo ni Gari ambayo inatumia mafuta mengi kuliko kawaida na haioneshi code yoyote kwenye mashine wala kuwasha taa yoyote kwenye dashboard. Kama gari yako inapaswa itumie 1L kwa 15Km kwenye Highway halafu ww unapata 1L kwa 8Km basi kuna shida mahali. Na shida hiyo inaweza kuonekana ikiwa gari yako itafanyiwa diagnosis. Live data stream za Diagnosis machine huwa zinaonesha kama matumizi ya mafuta kwenye gari lako ni ya kawaida au si ya kawaida pia zinaweza kukufanya ukajua matatizo mengine ambayo hayaweka code yoyote kwenye control box.

Mwisho
Kama unaplan kununua gari na ungependa kuangaliziwa mambo niliyoyaelezea hapo juu na diagnosis ya gari lako kiujumla tunaweza kuwasiliana.
 
Kabla ya kuuza Carina Yangu nilimwambia mteja wangu atafute fundi wake nakumbuka fundi alifungua oil cap kuangalia kama oil pump inasukuma vizuri pia aliingia uvunguni mwa gari huku gari IPO Kwenye D....
Labda inisaidie JITU LA MIRABA MINNE huyu fundi alikuwa anataka kujua TATIZO gani kipindi gari IPO Kwenye D

Aiseee... Tunatofautiana ujuzi mkuu.

Siwezi kujua moja kwa moja. Japo kuingia uvunguni na umeweka D ni risk kiasi chake.
 
Ukiachana na mambo ambayo watu wengi wanaangalia wanaponunua magari used ambapo mengine ni madogo. Kuna mambo ambayo huwa ni ya kiufundi zaidi ambayo huwa ni vizuri pia yakaangaliwa...

Ahsante sana. Hii ni elimu tosha.

Ila kuna mafundi wanakuzunguka, wanakula na muuzaji alafu unaaambiwa chuma kipo mahali pake kumbe ni kimeo tu.
 
Ukiachana na mambo ambayo watu wengi wanaangalia wanaponunua magari used ambapo mengine ni madogo...
Smahani mkuu, nilienda kwa fundi kubadili gear box flui, nikaambiwa ninunue lita tatu na nusu maana ndo ujazo wa gearbox yangu (kwa madai ya fundi), nikafanya hvyo.

Gari ni toyota Allex 1nz fe, baada ya kubadili gari inachelewa kubadili gear na ikibadili hadi inastuka. Mbaya zaidi ni kwenye milima haichanganyi kabisa, inaishia speed 30 tena baada ya flat foot.

Nilijaribu kuangali google ujazo wa fluid wa gari yangu nikakuta ni lita 6.9, wakati fundi alinambia ni lita 3.5. Je tatizo la gari kukosa nguvu huenda likawa ni uchache wa ATF?
Screenshot_20200608-104344_Chrome.jpg
 
Ahsante sana. Hii ni elimu tosha.
Ila kuna mafundi wanakuzunguka, wanakula na muuzaji alafu unaaambiwa chuma kipo mahali pake kumbe ni kimeo tu.

Yeah ni ishu ambayo inaumiza sana watu.
 
Smahani mkuu, nilienda kwa fundi kubadili gear box flui, nikaambiwa ninunue lita tatu na nusu maana ndo ujazo wa gearbox yangu (kwa madai ya fundi), nikafanya hvyo...

Mkuu, Ninachokifahamu ni kwamba unapomwaka ATF kwa kufungua tu ile bolt ya chini kule kwenye Oil pan kitakacho toka pale huwa ni 60% tu ya ATF yote. Kuna ATF ambayo huwa inabaki kwenye Oil pan, Valve Body na Torque converter.

Ukipiga hesabu kwa hiyo snerio yako. Kuna uwezekano mkubwa ATF iliyowekwa ni chache kuliko inayotakiwa. Hivyo kitu cha kwanza ni muhimu kuangalia kwenye dipstick kama kweli inatosha.

Halafu pia. ATF mliyoweka ndio ambayo imeandikwa kwenye dipstick ya hiyo gearbox?
 
Mkuu, Ninachokifahamu ni kwamba unapomwaka ATF kwa kufungua tu ile bolt ya chini kule kwenye Oil pan kitakacho toka pale huwa ni 60% tu ya ATF yote. Kuna ATF ambayo huwa inabaki kwenye Oil pan, Valve Body na Torque converter.

Ukipiga hesabu kwa hiyo snerio yako. Kuna uwezekano mkubwa ATF iliyowekwa ni chache kuliko inayotakiwa. Hivyo kitu cha kwanza ni muhimu kuangalia kwenye dipstick kama kweli inatosha.

Halafu pia. ATF mliyoweka ndio ambayo imeandikwa kwenye dipstick ya hiyo gearbox?
Mkuu samhani, kama utaweza naomba kujua maana halisi na tofauti yake wanaposema 4 speed, 5speed au 6speed automatic transmission n.k.
 
Mkuu samhani, kama utaweza naomba kujua maana halisi na tofauti yake wanaposema 4 speed, 5speed au 6speed automatic transmission n.k.

4- speed transmission maana yake gearbox yako ina range 4 za speed na RPM. Mfano ni A343F iliyomo kwenye asilimia kubwa ya Land Cruiser.

5-speed transmission ina range 5 za speed na RPM. Mfano ni A650E ambayo imefungwa kwenye Toyota Crown Majesta ya mwaka 2000 mpaka 2004.

Wakati 6 speed transmission ina range 6 za speed na RPM. Mfano ni A960E ambayo imefungwa kwenye Toyota Mark X ya kuanzia mwaka 2004 na kuendelea.
 
4- speed transmission maana yake gearbox yako ina range 4 za speed na RPM. Mfano ni A343F iliyomo kwenye asilimia kubwa ya Land Cruiser.

5-speed transmission ina range 5 za speed na RPM. Mfano ni A650E ambayo imefungwa kwenye Toyota Crown Majesta ya mwaka 2000 mpaka 2004.

Wakati 6 speed transmission ina range 6 za speed na RPM. Mfano ni A960E ambayo imefungwa kwenye Toyota Mark X ya kuanzia mwaka 2004 na kuendelea.
Shukran
 

Pia 6 speed transmission inachanganya haraka sana ukilinganisha na 4 speed transmission. Kwa sababu 4 speed tranamission itakuwa na range kubwa sana ya kucover speed kabla ya kubadili gear tofauti na mwenye 6 speed ambaye kwake gear itabadilika katika range fupi fupi.
 
Back
Top Bottom