Kwanini ni ngumu Iran kuivamiwa na Marekani na vibaraka wake (Israel) kwa vikosi vya ardhini?

Mleta mada huelewi wewe mhuru au great seal ya Marekani ina picha ya Tai ndege mbabe angani

Hakuna ndege mbabe angani kivita kama Tai

Aweza ona hata sindano ndogo ikiwa chini

Jeshi la Marekani ambao ndio wayahudi wenyewe kijeshi waliamua kuwa watajenga uwezo wa kijeshi mkubwa wa Angani ili kuwa na Air superiority kivita

Ukigombabana na Marekani au Israel kuiua atatokea wapi kukupiga sio kesi kubwa wewe kodoa tu macho angani ndiko atakakoanzia kukutwanga na atakutwanga hasa .Akisha kutwanga hasa ukawa tepetepe kutoka angani ndipo askari wa Ardhini makomandoo wabaingia kazini kukumaliza kabisa sababu military capability zako zinakuwa zimepondwa hasa toka angani

Israel kwa sasa vita na Iran iko phase one kuiponda barabara kivita toka angani na wamefanikiwa kiasi kikubwa sana kuua hadi viongozi wakuu wa jeshi la Iran

Phase two itakuwa zamu ya majeshi ya Ardhini

Mwambieni Ayatollah kuwa wako njiani kuja ardhini wanamalizia operation za kutoka angani
 
Ulishawahi kufika Iran,Iraq, Israel, Syria, Jordan, Saudia? Kama jibu ni hapana....niendelee na shughuli zangu
 
Ngoja nikuulize..... Huyu huyu USA mpaka tunaongea sasa na military superiority yake yote Afghanistan zaidi ya miaka 20 kafanikiwa kufanya nini? Taliban haikurudi madarakani ndani ya wiki tu baada ya kuondoa majeshi?
 
Hii ndio lugha ilyotumika Gaza, Ila kinachoendelea, kinasikitisha
 
Iran sio Gaza, Iran sio Afghanistan..... Usiweke hiyo nchi kwenye kundi moja na hizo nchi
 
Iran sio Palestina ndugu, hao Wapersia na sio Waarabu
Walimtungua rais wao, wameua mkuu wa majeshi, wameua wanasayansi karibu tisa wanaotegemewa wa nyuklia, walizima mitambo yao ya ulinzi na kupeleka ndege zinazoendeshwa na vibinti, wakajipigia wanavyotaka.

Kwa nchi nyingine kumuua raisi au mkuu wa majeshi pasingetosha.
Wao wairani wamefanya nini, mikerere tu!!!
 
Je, ni lazima kufanya operesheni ya ardhini ili kufanikisha kuangusha utawala au kulazimisha taifa kujisalimisha? Ikumbukwe kwamba Marekani ilitumia mabomu ya atomiki dhidi ya Japan, taifa lililokuwa gumu kujisalimisha, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Shambulio hilo dhidi ya miji ya Hiroshima na Nagasaki, lililotokea tarehe 6 na 9 Agosti 1945, lilipelekea Japan kujisalimisha bila haja ya kuendesha operesheni ya ardhini ya kijeshi.
 
Wajinga ni wengi Sana jamanii? Sijui itumike mbinu gani kuondoka na wajinga kama mtoa mada.... Sijawahi kuona vita ya namna hiyo duniani yaani unapita zaidi ya 3 kwenda kuvamia nchi nyingine?
Tanzania kuna vichaa wengi Sana
nimecheka sana,wewe ni JINGA LA MAJINGA KATIKA HII NCHI,kwani USA wanashea mipaka na afghan,iraq vietnam...maana nchi hizo zote zipo mbali nae tena sana lkn alipigana vita vya ardhini
 
vita ya sasa hivi inapiganwa kwa kubonyeza kitufee tuu...kama una mawazo ya vita ya kupeleka wanajeshibwa ardhini basi wewe ulizaliwa enzi za ujima
 
Kuweka buti ardhini kwenye nchi yoyote ile ni hatari na gharama kubwa. Pia ni rahisi kuamsha upinzani na maandamano kwa raia wako mwenyewe.
 
Wakitumia bomu la nyuklia kutatua tatizo la Iran basi watakuwa wamezaa tatizo kubwa zaidi; middle east kila nchi itqkimbilia kutengeneza ya kwake au hata kununua
Marekani akitupa bomu la nyuklia Iran basi ujue hata Urusi haitataka kuulizwa ikilitumia Ukraine
Na ikumbukwe mabomu ya nyuklia sio mabomu hatari zaidi kwenye shehena za silaha za nchi nyingi
Leo itapigwa Iran na bomu la nyuklia kesho Kuna wafia dini watarusha biological weapon Tel Aviv, unamalizia vita moja ila unafungua mlango kwa matatizo makubwa zaidi
 
Mkuu tangu jiwe afe nakwenda kuzimu mazima unaichukia Sana CCM
 
Hamna nchi yenye uwezo huo mashariki ya kati kutengeneza Nuclear weapons zaidi ya Iran, ambaye so far technically kashindwa Hadi sasa.
 
Walipovamiwa na iraq ilikuwaje ,walipopasuliwa na Alexander the great ilikuwaje? Walipo pasuliwa na Mongolia ilikuwaje, walipavamiwa na ottoman ilikuwaje Irani ni yakwaida sana sema nyie wavaa kobazi shule hamendi mpo kusoma bikra 72 tu

USSR
 
Wajinga ni wengi Sana jamanii? Sijui itumike mbinu gani kuondoka na wajinga kama mtoa mada.... Sijawahi kuona vita ya namna hiyo duniani yaani unapita zaidi ya 3 kwenda kuvamia nchi nyingine?
Tanzania kuna vichaa wengi Sana
Halafu kwa nini uende ardhini wakati betteroption ambayo ni matumizi ya ndege ipo??
 
N
Hamna nchi yenye uwezo huo mashariki ya kati kutengeneza Nuclear weapons zaidi ya Iran, ambaye so far technically kashindwa Hadi sasa.
Hajashindwa bali anaigiza kushindwa, Kuna faida kubwa kwa Iran kutishia kutengeneza bomu la nyuklia kuliko kulimiliki moja kwa moja
Geopolitics ni Mchezo mchafu sana, hii tishia tishia ya kutengeneza bomu inawafaidisha mpaka Urusi na China maana katika ajenda kubwa wanaozoongea na Marekani wakikutana ukute hata Iran inatajwa

Hezbollah + vikundi vingine vinavyoumiza kichwa Israel na USA >>> Iran >>> Russia
 
Ni kweli kwamba moja ya sababu kuu mbili zinazomfanya Iran ihangaike kuwa na uwezo wa nyuklia ni.Kwanza, kuzuia uvamizi kutoka kwa Israel, na pili, kuzuia Marekani kuweka mikono yake kwenye maeneo ya mafuta na kusimika serikali ya vikaragosi kama ilivyo kawaida yao. Hata hivyo, kuhusu hoja kwamba Iran inaigiza kushindwa, mimi sidhani kama hilo ni kweli.Endapo Iran ingetangaza au kuonyesha wazi kuwa imetengeneza silaha za nyuklia, dunia nzima ingefahamu mara moja, na kwa upande wa propaganda, wapo vzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…