View: https://youtu.be/9En_7EXBnDs?si=xhZB7iQvMx7BXY3IWakati ule walikuwa wanajiropkea Ili kujifurahisha na kufikiri wanatuzodoa pasipokujua kumbe walikuwa wanatengeneza ushahidi wa kutumika huko mbele kuwakamatisha wenyewe..
Na wakati huo ni sasa. Hawana cha kujitetea. Kilichosemwa na Polepole hakitaweza kujibiwa kwa hoja za kipropaganda na nyepesi huku nyuso zao zikionesha kila dalili ya panic na kushitushwa kusiko mithirika...
Polepole amewapa simple alternative kuifanya CCM ibaki na pumzi kidogo kwenda mbele;
Mosi "wamwage oil" ya gari lao la kizamani, CCM. Yaani piga chini Bi Samia, hapaswi kuwa mgombea Urais wa CCM. Hana uwezo wa kiuongozi, hafai hata kwa dakika mbili tu kukalia kiti hicho...
Mbili, mchakato wa kupata mgombea Urais ndani ya CCM ufanyike upya kwa kuzingatia katiba, kanuni, miongozo na utamaduni wa CCM...
Tatu, piga chini kundi la wahuni ndani ya CCM waliomzunguka huyo Mama Kizimkazi kiasi cha kutoona baya lolote na kufanya lolote aambiwalo na wahuni hawa..
Nne, Fanyeni maridhiano na CHADEMA ili kuiponya nchi na taifa na hatari iliyopo mbele kama tutafanya uchaguzi wakati washindani wa kweli wa CCM yaani CHADEMA wamefungwa kamba abusively bila kosa wala haki na kiongozi wao mkuu kuwekwa gerezani unlawfully na bila kosa lolote. Mwachieni Tundu Lissu, waache kumuonea na kuionea CHADEMA...
Wameambiwa hayo, lakini wameziba masikio na kujifanya vipofu hawaoni ubaya na uhuni. Kitakachowapata, hawatakuwa na wa kumlilia..