Kwanini nikimsikiliza Ahmed Ally wa Simba SC naelimika zaidi, ila nikiwasikiliza Haji Manara na Hassan Bumbuli wa Yanga SC nalewa?

Kwanini nikimsikiliza Ahmed Ally wa Simba SC naelimika zaidi, ila nikiwasikiliza Haji Manara na Hassan Bumbuli wa Yanga SC nalewa?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally ni Msemaji (Mzungumzaji) mzuri, ametulia, hana papara, anajua nini cha Kuongea na wakati gani, ana PR nzuri, Mtanashati kuanzia katika Mavazi, Akili na Mvuto hivyo Simba SC imempata Competent Club Spokesman / Spokesperson kikubwa imuamini, imtunze na imsikilize pia katika Mawazo yake.

Kuna Timu zingine pamoja na kwamba zina Wasemaji wa Wanachama (wa Klabu) na wa Mdhamini (Tajiri) lakini ukiwa unawasikiliza unaweza ukatafuta la maana na ukalikosa ila cha pekee ambacho hutokikosa Kwao ni Majungu, Wivu, Uswahili na Kujipendekeza na Kujibebisha kwa Tajiri huku wakijijua kuwa Wao ni Wanaune na Tajiri ana Mke wake mzuri tu ambaye hata bado hajamuacha.

Naipenda sana Personality ya Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally kwani ni Corporate kabisa na popote akienda atavutia na Kushawishi walioko hasa Kibiashara tofauti na wengine ambao Meno yao ya Rangi Mbili na Pua zao Kubwa kama Honi za Mabasi ya Mwendokasi zitawakimbiza Wadau wa Kibiashara wanaoenda Kuwaona.

Mightier nikimsifu Mtu jua yuko vizuri.
 
Nakukubali sana mtani wangu, lkn punguza utani unaogusa uumbaji wa MUNGU sio sahihi sana!!tutaniane kwa mambo mengine ila uumbaji wa MUNGU usiuguse!!maana analipiza kizazi cha kwanza hadi cha nne!
Sijaona sehemu yoyote ile niliyemsema au niliyowasema Watu wako labda Wewe unaowajua useme ni Msemaji gani wa Klabu ana hayo Meno Rangi Mbili na ni Msemaji gani mwingine wa Klabu ana Pua Kubwa kama Honi za Magari ya Mwendokasi?

Nasubiri.......!!!
 
Sawa mtani kama ni kweli hakuna sehemu uliyoandika basi tuyaache hayo!
 
Nakukubali sana mtani wangu, lkn punguza utani unaogusa uumbaji wa MUNGU sio sahihi sana!!tutaniane kwa mambo mengine ila uumbaji wa MUNGU usiuguse!!maana analipiza kizazi cha kwanza hadi cha nne!
Ni kweli kuukosoa uumbaji wa mwenyezi mungu ni dhambi ameteleza, ila kiukweli huyu jamaa ni mwanamichezo mwenye akili kipindi yupo mtangazaji Azam sikuwahi kuzani wala kufikiria huyu ni shabiki mwenzangu wa Simba sport club
 
Yuko smart sana, namsikiliza apa anaongelea swala la VAR kamuelimisha mwigulu vizur sana
Mwigulu Mchemba yeye anangalia Yanga yake tu kukosa alama tatu dhidi ya Mbeya City.

Inawezekanaje kuwa na VAR kwenye shamba la mpunga la Manungu Complex!?

Ndo maana anaelimishwa na Afisa Habar mwenye TIN Number Ahmed Ally kwamba Sheria Number One ya soka ni Kiwanja.
 
Mwigulu Mchemba yeye anangalia Yanga yake tu kukosa alama tatu dhidi ya Mbeya City.

Inawezekanaje kuwa na VAR kwenye shamba la mpunga la Manungu Complex..!?

Ndo maana anaelimishwa na Afisa Habar mwenye TIN Number Ahmed Ally kwamba Sheria Number One ya soka ni Kiwanja.
Ukichunguza alichoongea mwigulu, alisema angalau viwanja kumi viwe na V.A.R na sio viwanja vyote. Kama imewezekana kuwekwa taa viwanjani hakika na hili la Video assistant litawezekana.

Ova.
 
Ukichunguza alichoongea mwigulu, alisema angalau viwanja kumi viwe na V.A.R na sio viwanja vyote. Kama imewezekana kuwekwa taa viwanjani hakika na hili la Video assistant litawezekana.

Ova.
Viwanja bora Tanzania ni Mkapa, Azam Complex, CCM Kirumba, Amani Zanzibar

Unaweka VAR viwanja kumi unacha viwanja vingi vibovu ndo umefanya nini? Kwani Ulaya ambako tunapenda kuiga walianza na VAR

Huyu droo imesababisha anze kupumua kwa shida..!
 
Kosa la Hassan ni lipi?
Kusema waamuzi wa Tanzania wajirekebishe?
Kusema TFF iangalie viwango vya waamuzi?
Ni Nani Kwa hakika anaridhishwa na waamuzi wa nchi hii?
Ni wewe? Wewe unaona wanatenda haki?
Anapotokea Mtu akasema udhaifu wa Mahakama ya mpira kutokana na yaliyomkuta mahakamani ni Nani mwenye haki ya kumsemea?
 
Mkuu usisahau pia kuna karatu (japo haujaanza chezewa ligi), ccm kirumba mwanza, ccm samora iringa, sokoine mbeya, itumike tu ile VAR ya kiafrika sio lazima tutumie ya Ulaya.

Ova.
 
Kosa la Hassan ni lipi?
Kusema waamuzi wa Tanzania wajirekebishe?
Kusema TFF iangalie viwango vya waamuzi?
Ni Nani Kwa hakika anaridhishwa na waamuzi wa nchi hii?
Ni wewe? Wewe unaona wanatenda haki?
Anapotokea Mtu akasema udhaifu wa Mahakama ya mpira kutokana na yaliyomkuta mahakamani ni Nani mwenye haki ya kumsemea?
Kwanini waamuzi wajirekebishe baada ya Droo ya Mbeya City? Mbona wakati mnashinda haya hayakuwepo.

Kitu kimeanza Kugonga ndo maana yake..!
 
Kabwili alisema kule yanga kuna wenzake kawaacha,mmoja yupo kwenye hao wawili,

JamiiForums-1748518016.jpeg
 
Back
Top Bottom