safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Mwili kikawaida huwa una njianzake pekee za kujilinda dhidi ya vitu mbalimbali(defense mechamism).
Mtu akipaliwa na punje ya wali atakohoa na hakuna anayezuia kwamba usikohoe kwa sababu kukohoa ni njianya mwili kujilinda na baada ya hapo mtu anapata afadhali.
Sasa kwenye mafua, yale mafua ni body fluid ambayo miongoni mwa kazi zake ni kuondoa uchafu kwa kutumia njia ya kujizalisha kwa wingi fluid hiyo na hatimae kuanza kuvuja nje.
Kama hali iko hivyo kwamba mafua yanayotoka kwa mtu ni njia moja wapo ya kusafisha mwil i basi maana yake ni kwamba kuyazuia mafua hayo ni kusema kwamba hautaki uchafu huo utoke ndani ya mwili.
Hiyo ina maana ya kwamba unapotumia dawa ya kuzuia mafua maana yake unatumia dawa ya kuzuia uchafu usitolewe ndani ya mwili.
Je, hii haiwezi kutufanya tuwaze kwamba matumizi ya dawa za kuzuia mafua kwa muda mrefu inaweza kusababisha matatizo makubwa kama kushusha kinga ya mwili?
Maana unapozuia mafua maana yake unazuia ulinzi wa mwili,unapouzuia kwa muda mrefu hatimae utaudhoofisha mfumo wa kinga,na hatimae sasa kifua kitavamiwa kwa kasi hapo baadae na kusababisha COPD yaani matatizo ya kifua sugu?