Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
- Kadiri tunavyokabidhi nafsi zetu kwa Mungu, ndivyo tunavyojifungua kutoka kwa vifungo vya ubinafsi na kuanza kuona ulimwengu kwa macho ya huruma na upendo. Wakati roho zetu zinapojisalimisha kwa neema ya Mungu, mioyo yetu inajawa na uchungu wa kweli, uchungu unaotokana na kuona mateso na mahitaji ya wenzetu, hasa wale wanaosumbuliwa na janga la umaskini na ukosefu wa mahitaji ya msingi.
- Macho yetu yanapokuwa wazi kwa huruma ya Mungu, tunaanza kuhisia maumivu ya wale ambao wanateseka kwa kukosa rasilimali za maisha. Tunasikia kilio cha jirani zetu, kilio cha wale ambao hawawezi kununua chakula cha kutosha, mavazi, au mahitaji ya muhimu kwa familia zao. Tunaanza kuguswa na hali yao, na ghafla, tunajikuta tukiishi katika hali ya kutafuta njia ya kuwasaidia. Huu sio uchungu wa dunia hii tu, bali ni uchungu wa kimungu uchungu unaotufanya tuwe na mapenzi ya kweli kwa wenzetu.
- Ingekuwa ni jambo la kushangaza kama, wakati wa mifungo mitukufu na mitakatifu, tungeanza kulalamikia gharama za vyakula. mifungo huwa ni vipindi vya kujitolea, kujinyima, na kuzingatia uhitaji wa kiroho zaidi kuliko uhitaji wa kimwili. Lengo la funga siyo kulalamikia upungufu wa vitu vya kimwili, bali kujiweka chini ya neema ya Mungu na kukumbuka kuwa Yeye ni chanzo cha maisha yetu. Tunaposhuhudia njaa au shida za kifedha, tunapaswa kutafakari na kuona kama ni fursa ya kutafuta uso wa Mungu, ambaye anajaza roho zetu kwa amani na furaha isiyo na kifani.
- Kama tunabadilisha funga kuwa muda wa kulalamikia gharama za maisha, basi tunapoteza maana halisi ya mifungo ya kiroho. Funga inatufundisha kwamba upendo wa Mungu hautegemei mali au starehe za dunia, bali ni neema inayotufanya kuwa na huruma, utu, na mshikamano kwa wengine. Njaa ya mwili inapaswa kutufundisha njaa ya roho, na hiyo ndiyo inayoleta umoja na utakatifu wa kweli.