Kwanini Nyama huwa hainogi ukiwa mwenyewe

Kwanini Nyama huwa hainogi ukiwa mwenyewe

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Sasa sijui kwa nini inakuwa hivyo nyama huwa hainogi ukiwa mwenyewe,

"Niko hapa mjini Eneo flani hivi mwenyewe tu nimeagiza kitimoto Nusu na Robo (robo tatu) na viazi vya buku jero.

Nyama iko vizuri lakini nipo tu nashindana nayo mwenyewe ata Nusu sijafika naona Tumbo limenisaliti.

Nilikuwa na njaa lakini sasa najiona naelekea kupigwa KO, hata hamu imekata naona kama najilazimisha tu.

Macho yangu nimeyatoa kodo kutazama pembeni labda nitakuta pisi kali nilivute tusukume wote lakini wapi

Mzigo umenishinda bora nikiwa na washkaji zangu au mlupo ndio inakuwa mwake

Hizi nyama kwa nini huwa hazinogi ukiwa mwenyewe?

Cc Zero iq

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utamu wa msosi upo kwenye katabia ka kugombania au kujiwekea hifadhi (hata kama ni kwa siri). Hiyo ni principle ya wanyama akiwamo mwanadamu. Ndio maana wataalamu wa kufuga nguruwe wanakwambia akiwa peke yake bandani hatanenepa maana anakuwa mvivu kula, ila ukiwaweka kuanzia wawili, watagombania chakula hata kama kinawatosha, na katika kugombania ndipo anajikuta ananenepa
 
Mkuu yaani hapa bila ya picha sawa na fid q kuimba singeri.
 
Back
Top Bottom