Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]Mjumbe hujawahi kula sugar cane lililopanda kando ya maji taka?. Huwa tamu kinoma kupita ile ya kilombero ila ulishawahi ona mtu anaugua typhoid au kipindupindua kwa kula miwa iliyooteswa kando ya maji taka?. Hujawahi kuona mama sura mbaya baba usiseme wakazaa binti kigori au kisura?. Mambo ya Mungu mwachie Mungu . Week end hii kakate mdudu somewhere chinja kula wala usiulize ulize.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]Aliyesema ni mchafu na anakula uchafu, ni sawa lakini kinachopatikana ni kisafi kwa afya. Chukua umepanda mahindi ukaweka mavi ya binadamu kama mbolea yakaota vizuri na kuzaa mahindi, hayo mahindi yana mavi? Kiti moto hoyeee!! Kwa afya zenu
Sent using Jamii Forums mobile app
Athari za nyama ya nguruwe kiafya na kiimani
Nguruwe katika mwili wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa
Mdomo ni maficho ya vijidudu, bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na wanyama.
Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis). Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na wanyama.
Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis Buski) hupatikana kwa wingi nchini China.
Maradhi ya Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na wenye kuchanganyika nao, na yanaweza kuenea
kwa sura ya mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya bahari ya Pacific baada ya kimbunga. Maradhi yanakuwepo panapokuwepo nguruwe katika nchi zilizoendelea kiviwanda kinyume na madai ya uwezekano wa kuushinda uchafu wake kwa kutumia teknolojia mpya zinazoharamisha kula nyama bila ya kibali, hasa nchini Ujerumani, Ufaransa, Philippines na Venezuela.
Kwa kula minofu ya nyama ya nguruwe, (Trichinellosis) hupatwa na ugonjwa wa Balantidium Dysentery. Kwani mke hubungua kuta za matumbo kwa ajili ya kuweka mayai ambayo yanafikia kiasi cha 10,000. Mayai hayo huingia kwenye misuli kupitia damu na kugeuka kuwa ni vijiyai vyenye kuambukiza.
Ama kupata maradhi kupitia mchango wa nguruwe, ni kuwa hiyo hupatikana baada ya kula minofu ya nguruwe mwenye ugonjwa.
Minyoo hukua kwenye mchango wa binadamu na urefu wake unaweza kufikia meta saba, na unakuwa na kichwa chenye miba inayosababisha kukwaruzika kwa kuta za michango na mchupo mkubwa wa damu, na ana mirija minne na shingo. Aina za mke huzaliwa kama kwamba ni wanyama pekee na hufikia maelfu. Na katika kila mmoja kati ya mnyama, huzaliwa zaidi ya mayai elfu moja iwapo utakula Cysticercosis.
Kupatwa na ugonjwa wa minyoo ya tumbo la binadamu, hutokana na kula chakula kilichoingia mayai na kutoa lava, na huingia katika damu kupitia kiungo chochote. Na hatari yake hukisiwa kwa mujibu wa umuhimu wake.
Maradhi haya hayatokei kabisa kutokana na kupatwa na mchango usio na miba katika kichwa na wenye madhara madogo
kabisa Taenia Saginata ya ngombe.
KIIMANI
kwa upande wa Quran
"Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).
KWA UPANDE WA BIBILIANguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao (Walawi 11: 7 8).
HABARI MBAYA KWA WALA NGURUWE A.K.A KITIMOTO HII HAPA
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.
Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.
Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.
Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.
Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.
Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali, alisema Profesa Lekule.
Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.
Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.
Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.
Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika, alibainisha Profesa Lekule
Wabongo Kuleni Kitomoto Mkiumwa Ugonjwa wa Kifafa dawa ninayo ninauza shilingi Millioni 1. Ukitaka Dawa ya Kifafa bonyeza hapa.
Mzee umenena. Sisi huku tunanyang'anyana na waislamu mpaka tunaikosa hata nusu kilo! Afadhali mwezi Ramadhan ufike ili tujinafasi maana huo ndiyo mwezi pekee kitimoto inabaki buchani!Nyama ya nguruwe ni nyama nzuri kiafya kwa sababu si nyama nyekundu sana na ni rahisi kumeng'enywa.
Nguruwe pia wana magojwa kama homa ya nguruwe, minyoo. Lakini ng'ombe wana magonjwa mengi na hatari zaidi kuliko nguruwe kama Sotoka, Minyoo (tegu), TB, kichaa cha ng'ombe, homa ya bonde la ufa, midomo na miguu nk.
Pia nyama ya ngombe ni nyekundu na ngumu, inaweza kusabisha Bawasili (Kutoka nyama sehemu ya haja kubwa) na pia kusabisha kukosa choo.
Kula Kitimoto kwa furaha na afya yako. Ni tamu, haikinai na pia ni nzuri zaidi kwa afya kuliko nyama ya ng'ombe!
Ukiweza tafuna na mifupa pia kwani inatafunika kirahisi utapata madini ya chuma, kalisiamu na fosifeti moja kwa moja, madini haya yanasaidia kuongeza damu na kuimarisha mifupa na meno.
MAMBO YA WALAWIAcha kututisha nguruwe nimekula tokea nazaliwa hadi leo Nina afya ya ajabu na kuhusu swala la imani biblia imeweka wazi kuwa; Si kiingiacho kimtiacho mtu unajisi bali kitokacho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yesu alivibariki na kuvitakasa vyakula vyote tena akasema usikiite najisi chochote Mungu alichokiumbaMAMBO YA WALAWI
MLANGO 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
Bwana Yesu alisema: Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.(Mt. 5:17-18).Yesu alivibariki na kuvitakasa vyakula vyote tena akasema usikiite najisi chochote Mungu alichokiumba
Sent using Jamii Forums mobile app
MAMBO YA WALAWI![]()
nyie hamjui,ngoja nipeleke mboga mjini
Wote mpo sawa kulingana na imani zenu cha muhimu kila mmoja atimize wajibu,anayeamin nguruwe si najisi bas ale na asiyeamin bas aache si wakat wa kulumbana japokuwa ni kwa hojaMAMBO YA WALAWI
MLANGO 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
8. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
Yesu alivibariki na kuvitakasa vyakula vyote tena akasema usikiite najisi chochote Mungu alichokiumba
Sent using Jamii Forums mobile app
Bwana Yesu alisema: Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.(Mt. 5:17-18).
Aliye kuja kuruhusu kula nyama ya nguruwe alikuwa ni Nabii Paaulo kwa sababu yeye Nabii Paulo hafuati Sheria ya Torauti ya Manabii.
Hata hivyo, Nabii Paulo ndiye aliyekuja akaenda kinyume na shari’ah hiyo kwa kutoa agizo kwa barua aliyowaandikia Warumi:
“Basi, usiiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya ubishi juu ya chakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya aanguke katika dhambi” (Waroma 14: 20).
Pia, “Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake” (Waroma 14: 14).
Paulo amesema tena kuwa kila kitu alichoumba Mungu ni chema wala hakuna kinachohitaji kukataliwa (1 Timetheo 4: 3 – 5).
Wewe Ipinge Biblia inavyosema kwa akili yako. ( MAMBO YA WALAWIWote mpo sawa kulingana na imani zenu cha muhimu kila mmoja atimize wajibu,anayeamin nguruwe si najisi bas ale na asiyeamin bas aache si wakat wa kulumbana japokuwa ni kwa hoja
Sent using Jamii Forums mobile app
Ninachoamin nitaendelea kukiamin daima maana ndicho kitakachoniponya.Tafsiri ya vitabu vya Dini hasa Biblia si rahisi sana na Biblia ni pana sana inahitaj uwe na roho mtakatif ili uielewe vizur na kuizingatiaWewe Ipinge Biblia inavyosema kwa akili yako. ( MAMBO YA WALAWI
MLANGO 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
8. Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.)
Mungu amekupa macho lakini huoni ukweli.Mungu huyo huyo amekupa akili lakini hauitumii ipasavyo na Mungu amekupa masikio lakini hausikilizi na kujuwa ukweli ni upi? Sijuwi utakwenda kusema nini siku ya hukumu mbele ya Mungu wako?
Aya za Biblia zinapingana Agano la kale linakataza nyama ya nguruwe agano jipya nyie munalifuata linaruhusu nyama ya nguruwe sasa wewe unamini agano lipi kati ya hayo MA-Agano mawili?Ninachoamin nitaendelea kukiamin daima maana ndicho kitakachoniponya.Tafsiri ya vitabu vya Dini hasa Biblia si rahisi sana na Biblia ni pana sana inahitaj uwe na roho mtakatif ili uielewe vizur na kuizingatia
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hajui kuwa matembele matamu ni Yale yanayopandwa uswahilini nyuma ya bomba la kutoka bafuni!!kwenye miwa mbali sana mkuu. muulize kuhusu bata. huwa anakula?
Ulichosema ni sahihi kabisa mdau,binafsi naamin Biblia yote ambayo ndan yake kuna agano jipya na la kale pia.Aya za Biblia zinapingana Agano la kale linakataza nyama ya nguruwe agano jipya nyie munalifuata linaruhusu nyama ya nguruwe sasa wewe unamini agano lipi kati ya hayo MA-Agano mawili?