za-10 katoa majibu sahihi sana. Nyerere hakuachia madaraka mapema, alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20; huo ni muda mrefu sanakwa kiongozi mwenye akili timamu kuendelea kuwapo madarakani ukitoa maamuzi makubwa ya kitaifa. Alikuwa anaplani kuachia madaraka mwaka 1980 baada ya kuunganisha tanu na asp, na akafanya mojawapo ya majukumu yake katika kipindi cha 1975-1980 kuwa ni kuunganisha tanu na asp, jambo ambalo lilikamilika mwaka 1977 chini ya usimamizi wa pius msekwa. Hata hivyo ile vita ya mwaka 1979 dhidi ya amin iliharibu mambo mengi kiasi kuwa nyerere alisema ataendelea kuyasimamia tena kwa miaka mingine mitano, ndiyo maana mwaka 1985 akaondoka ingawa alikuwa hajayanyoosha mambo hayo.