Ntaeleza kwa ufupi kwa kadri ya uelewa wangu....
Sera ya vijiji iliasisiwa na Mwl Nyerere ili kuwaunganisha watu wakae pamoja ili waweze kupata huduma za kijiji kwa ukaribu kumbuka zamani watu waliishi mbali mbali hivyo ikatakiwa watu wote waishi kwa pamoja waweze kupata huduma za Afya pamoja,yakaanzishwa maduka ya Ushirika,mashamba ya ushirika yaliyokuwa chini ya serikali na pamoja na kupewa zana za kilimo ili wavitumie kwa pamoja
Hivyo Mwl Nyerere ikawa sera yake hiyo ikawa inawalazimisha watu wawe pamoja wale waliokataa ndio walikutana na dhahma ya kuchomewa nyumba zao,kufyekewa mazao yao mashambani n.k hii ilipelekea watu wengi kwenda kuishi kwe vijiji vya ujamaa wakiwa na njaa ya kutisha isiyokuwa na mfano kumbuka kuna baadhi ya familia zilikuwa na mashamba makubwa tu huko walikoishi lakini walipopelekwa katika vijiji vya ujamaa walipewa vipande vya ardhi chukulia mfano mtu ana ekari 58 na analima kwa trekta lake mwenyewe na anakuwa na uwezo wa kuvuna hata gunia 300 harafu unampeleka kwe vijiji vya ujamaa ambapo anakatiwa nusu ekari ambapo anakuwa anavuna gunia 5-10 lazima apate njaa tena iliyokithiri. Lengo la hii sera watu walipokonywa yale mashamba yao ili waweze kulima yale mashamba makubwa ya Ushirika.
Hii ilisababisha watu kuishi kwa taabu sana wakiwa hawana chakula na hata pesa ya kujikimu pia hata makazi wakawa hawana
Sera hii ilisababisha watu kuishi maisha magumu mno hali hii ilipelekea mpaka serikali kuanza kuleta chakula cha msaada(mahindi ya yanga),sera hii ilikuwa nzuri ila shida ilikuwa ni nzuri ila tatizo lilikuwa ni utekelezaji wake,mfano mtu ana ekari 58 kwa nini unamuondoa na kupokonya ardhi yake? kwa nini usimuache aendelee na shamba lake ila umpe utaratibu wa kulima mashamba ya ushirika?
Mkuu hii ndo sababu kubwa ya nchi kuingia katika hali ya kuporomoka kwa uchumi na nchi kuingia kwe njaa kali hii nayo ilimsumbua sana Mwl hata kuanza kuipigia magoti Magharibi!!