GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Marekani ina jumla ya vituo vya Kijeshi (overseas military bases) 38 katika mataifa mbalimbali! Ukiacha Marekani, kuna mataifa mengine zaidi ya kumi na tano yenye vituo vya kijeshi sehemu tofauti tofauti.
Ni gharama sana kulihudumia Jeshi. Ukiona nchi inaamua kuanzisha vituo vya kijeshi nje ya mipaka yake, ujue inapata faida inayoendana na gharama inayoingia.
Ndiyo maana nchi ndogo kama Singapore nayo ina vituo vya kijeshi katika nchi mbili, Brunei na Taiwan.
Kwa jinsi Tanzania ilivyozisaidia nchi nyingi Afrika kupata uhuru, ilikuwa rahisi sana kwa Tanzania kuweka vituo vyake vya kijeshi huko. Kwa sasa tungekuwa na military bases Msumbiji, Zimbabwe, Comoro, Uganda, Afrika Kusini, Angola, Namibia, n.k.
Ingawa si nchi zote Tanzania ilishiriki moja kwa moja kuzisaidia kupata uhuru, lakini mchango wa Tanzania bado ni mkubwa, hata kwa amani zinazofurahiwa na hizo nchi kwa sasa. Nani asiyefahamu, kwa mfano, kuwa Tanzania ndiyo iliyomuondoa Dikteta Amin Uganda?
Fedha, muda, ardhi, na rasilimali nyingine za Watanzania zilisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru. Si vitu tu, lakini pia na wanajeshi wa Tanzania. Tena, kuna waliopoteza maisha kwenye hizo "operation".
Japo sijajua kwa undani faida ya hivyo vituo vya kijeshi, lakini naamini kuna maslahi nchi inayoweka huko vituo vya kijeshi inayapata. Inasemekana Paul Kagame ameshaweka vituo vyake vya kijeshi katika mataifa mawili hapa Afrika, Msumbiji na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kitendo cha Kagame kufanya hivyo ni ishara tosha kuwa kufanya hivyo kunawanufaisha. Si unajua Kagame ni "Mjasiriamali?" Anaweza kuziona fursa ambazo wengine hawazioni.
Kama Nyerere angeamua kuweka vituo vya kijeshi, inawezekana ingetunufaisha kama nchi. Labda,
1. Tungeweza kurudisha gharama zilizotumika kugharamia vita vya ukombozi kwenye hizo nchi!
2. Nchi ingeweza kutumia ushawishi wa Jeshi letu katika nchi husika kutengeneza fursa zitakazowasaidia Watanzania kunufaika huko!
3. Jina la Tanzania lingekuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa
Naweza nisiwe sahihi sana, lakini ninafikiria hizo zinaweza zikawa miongoni mwa faida ambazo tungezipata!
Kwa nini mzee wetu, J. K. Nyerere hakuliona hilo?