Kwanini Nyimbo za Diamond Zinawahi Kuexpire?

Kwanini Nyimbo za Diamond Zinawahi Kuexpire?

sio za mondi tuu hata za wakongo, wabongo, wakenya n.i
 
Kabla ya kutoa Zilipendwa alikuwa amemaliza kutoa nyimbo mbili Fire na Eneka ambazo hata hivo zilichukua siku chache kabla ya kuexpire.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Siku Mona baada ya Ali Kiba kuachia wimbo wake Wa Seduce me, Diamond naye akishirikiana na Timu yake ya Wasafi waliachia ngoma ya Zilipendwa. Cha kushangaza ngoma ya Ali Kiba bado imezidi kushika chati kwenye uwanja Wa Muziki, lakini zilipendwa ndio imeshapotea na sasa Mond ameamua kuachia kibao kingine " Hallelujah" ambacho kwa sasa ndicho kimeingia huku kikiikuta Seduce me ikiwa bado imeshika chati. Sasa seduce me inapambambana na Hallelujah siyo Zilipendwa tena!!!

Kwa nini nyimbo za Diamond zinawahi kuexpire haraka?
karibu kwa maoni
Kwa sababu Mondi anawahi sana kutoa ngoma mpya, mfano leo Kiba akiamua kutoa ngoma mpya basi seduce me watu wataisahau
 
Mziki wa kwenu ndio mmejijengea hivyo ,lkn soko la kimataifa linataka kila mara usikike na ndio maana wizkid, olamide, davido, Casper nyovest, aka, yemi alade wanaachia nyimbo kila siku na kuchuja kwa nyimbo inategemea na mtu kwani usichokipenda ww usikitie hila, mm kwa nyimbo zake ukiitoa eneka zote nazikubali na hazikosagi ktk playlist ktk PC yangu na ukae ukijua hakuna msanii ambaye nyimbo zake zinapigwa na kuombwa sana ktk masherehe kama diamond platnumz ,sasa sijajua labda unazungumzia kuchuja gani.
nimeipenda point yako eti zinaombwa katika masherehe hahahahahahaha
 
Huyu kijana anajituma sana kwenye kazi yake. Ila ELIMU ni muhimu kwakweli anatoa nyimbo bila mpango! Wakati mwingine unasikia katoa ngoma hujaitazama ana nyingine.

Angejifunza namna ya kufanya biashara angepiga pesa sana
 
Back
Top Bottom