Kwanini nyumba za Chamazi, Mbagala, Chanika zinauzwa sana?

Ni biashara budda! Ni kama kuuza chapati tu...huwezi kuuza kama haijakaangwa! So huwezi kuuza nyumba kama haijajengwa!
 
Wanakimbia uswahili..walijenga wakidhani ni ushuani kumbe uswahili mtupu.

Kuishi na jamii za kiswahili low minded people yataka moyo..kila wikiendi hakuna kulala ni mwendo wa vigoma tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwenye matangazo mengi, mf. Kupatana, Facebook market n.k, utakuta matangazo mengi ya nyumba zinazouzwa zipo Mbagala Chamazi.

Ni kwa nini? Hii inatia shaka hata kununua nyumba hizo. Kunani Chamanzi?
Mkuu hizo ni nyumba zisizochukua muda kukamilika na kama utamchukua mkaguzi wa majengo jibu atakalokupa ni kuamuru kubomoa tu haifai kwa matumizi ya binadamu. Nyumba zinajengwa kwa ajili ya biashara na sio kuishi wao.
 
Wanakimbia uswahili..walijenga wakidhani ni ushuani kumbe uswahili mtupu.

Kuishi na jamii za kiswahili low minded people yataka moyo..kila wikiendi hakuna kulala ni mwendo wa vigoma tu.

#MaendeleoHayanaChama
[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kabla ya kununua kiwanja au nyumba, chunguza kwa makini kuhusu uswahili wa sehemu husika. Kama huwezi usinunue, utapigwa kipapai cha kisawasawa.
 
Kwenye matangazo mengi, mf. Kupatana, Facebook market n.k, utakuta matangazo mengi ya nyumba zinazouzwa zipo Mbagala Chamazi.

Ni kwa nini? Hii inatia shaka hata kununua nyumba hizo. Kunani Chamanzi?
Ni nyumba ambazo hazina quality kuanzia tofali, plasta, bati ,rangi na vitu vyote.... Kwahiyo haushauriwi kununua nyumba za aina hiyo
 
Wajuzi wa mambo habari zenu.

Nimefatilia sana nyumba za mtandaoni nimegundua nyumba nyingi zinauzwa Mbagala, Chamazi, Chanika, nmejiuliza sana sijapata jibu naombeni majibu wakuu.

Nawasilisha
 
Nyingi ni jenga uza,
Shimo la choo ni futi 4
Matofali ya udongo, ila plasta kalii
Nyaya za umeme ni zile za rangi rangi za spika za sh.500 kwa mita
kenchi za mbao za minazi ambazo hazijakomaa vizuri(dumuzi kama wote)

Kuwa makini
 
nyingi ni jenga uza,
shimo la choo ni futi 4
matofali ya udongo, ila plasta kalii
nyaya za umeme ni zile za rangi rangi za spika za sh.500 kwa mita
kenchi za mbao za minazi ambazo hazijakomaa vizuri

kua makini
Ukiingia hilo chaka jiandae kujenga upya!

Ujenzi wa kule ni rahisi sana nashangaa wanashindwa nini kujenga nyumba imara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…