Kwanini nyumba za Chamazi, Mbagala, Chanika zinauzwa sana?

Kwanini nyumba za Chamazi, Mbagala, Chanika zinauzwa sana?

Wajuzi wa mambo habari zenu.

Nimefatilia sana nyumba za mtandaoni nimegundua nyumba nyingi zinauzwa Mbagala, Chamazi, Chanika, nmejiuliza sana sijapata jibu naombeni majibu wakuu.

Nawasilisha
Incomplete research! Fatilia kwanza wanaouza Wana sifa gani. Wazaramo Hao, ndio haohao waliiuza Kariakoo.. Wakahamia Ilala, wakaiuza Ilala wakaenda Chanika. Wanaouza hiyo Chamazi wanaenda kununua Kiponza. Na Kiponza ikianza kuchangamka Wanauza wanaenda Swelele
 
Wadau, nimeona kwenye Facebook nyumba nyingi zinauzwa Mbagala na Chamanzi, ni kwanini? Je, zina ubora wa msingi au ndo ukinunua linaanzia kupasuka?
 
Kuna siku mchepuko wangu mmoja ulipiga hela.geita ukaniomba nikamchagulie
Yaanikwanza hizo rangi kama katuni
Sikuvutiwa kabisa yaani .nikamwambia akajenge tu madale huko.sikumpenda tu yule msukuma wa watu.
 
Wanakimbia uswahili..walijenga wakidhani ni ushuani kumbe uswahili mtupu.

Kuishi na jamii za kiswahili low minded people yataka moyo..kila wikiendi hakuna kulala ni mwendo wa vigoma tu.

#MaendeleoHayanaChama
Hadi mtu anajuta kwa nini alijenga nyumba,kero za kufuatiliana maisha,makelele ya vigodoro
 
Mkuu hizo ni nyumba zisizochukua muda kukamilika na kama utamchukua mkaguzi wa majengo jibu atakalokupa ni kuamuru kubomoa tu haifai kwa matumizi ya binadamu. Nyumba zinajengwa kwa ajili ya biashara na sio kuishi wao.
Tofali biskuti.
 
Back
Top Bottom