Kwanini nyumba za Marekani zinawekewa bendera nje?

Kwanini nyumba za Marekani zinawekewa bendera nje?

Bongo mmeambiwa wimbo wa taifa ni tunu. Bendera ni tunu mtu binafsi hapaswi kuwa nayo matokeo yake watu wanavaa bendera za marekani na mataifa mengine kuliko bendera yao. Wimbo wa taifa baada ya shule ya msingi mtu huusikii wala kuuimba tena wakati kiwanja kila kona wimbo wataifa unaimbwa. Mgeni akifika leo by next wk tayari anaijua the star spangled banner yote. Bado mnajiuliza kwanini watu sio wazalendo wakati mnawakataza wasiwe proud na tunu zao za taifa. Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
Sio Marekani tu mbona hata nchi nyingi za Afrika hasa West Africa huweka bendera kwenye nyumba zao pamoja na magari nje.

Wengine wameenda mbali kwa kupaka nyumba zao rangi zinazofanana na bendera za nchi yao.
 
Kwetu kajamba ni shida!
Bendera ya taifa shida, nguo zifananazo na polisi au jeshi kivumbi!
Kajamba nani na banana republic sheria anatunga yoyote yule!
Bure kabisa kabisa
 
Kwakua umeshindwa kwenda www.google.com ngoja nikuitie wanaoishi huko wake wakuelimishe Bufa , Kiranga, Nyani Ngabu, Graph, Mzee Mwanakijiji mpeni Elimu huyu.
Tayari nilishalizungumzia hili jambo toka 2019!

 
Wakuu mnijibu

Hivi kwanini nyumba nyingi za Marekani zinawekewa bendera nje?
wamarekani wanapenda sana kuonyesha uzalendo wao, kama vile unavyoweka sticker ya timu yako ya mpira kwenye gari. Ni kama kusema, "Hii hapa, mimi ni mzalendo wa nchi yangu, na bendera ndiyo ushahidi!" Tafsiri rahisi: wanapenda kuonyesha mapenzi yao kwa nchi kama vile ambavyo sisi tunavyopenda kuweka bendera ya Yanga au Simba mlangoni ili jirani ajue uko timu gani! 😂
 
Back
Top Bottom