Kwanini Passo zinauzwa bei rahisi mitandaoni?

Fuqin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2018
Posts
306
Reaction score
625
Mambo vipi wadau.

Leo nilienda showroom maeneo ya Magomeni kuangalia gari ya bei rahisi nikakuta Passo ni milioni 8.5 ndo bei rahisi zaidi. Sasa nikapita mitandaoni kuangalia bei za Passo Used nikaona mpaka milioni 5 unapata tena namba D.

Sasa nataka kujua, kwanini wanauza bei rahisi mitandaoni? Je, ni matapeli au hizi gari ni vimeo?
 
Hapo umezungumzia mpya alafu ukazungumzia used bei haziwezi kufanana we umeingia mtandaoni umetaka used na sio mpya.
 
Passo no nzuri sana niliwahi kuwa nayo, ukipata ya Piston NNE bei inakua juu kidogo, ni bneoi ndogo kwakua ni CC ndogo, Passo ni CC 990 kwahio huwezi kukukta gari ya CC 990 ikauzwa 17m. ni nzuri pia kwenye consumption.
 
mi nina passo ya piston 3 toka 2014, na nina rav 4 pia nimenunua mwaka huu january... ila mara nyingi nikiwa na town trip passo ni choice yangu.. mafuta lita 10 natembelea 180km.. kwa town trip ni nyingi sana... yaani ni sawa na elfu 20 wiki nzima mpaka weekend kwa mtu anaekaa ubungo anafanya kazi posta
 
Passo achana nayo mkuu, kabla sijaanza kuitumia nlikuwa nachukia sura yake, ndani ina eneo kubwa sana, pia fuel efficiency, nliendesha toka dar nonstop hadi mwanza saa sita usiku nlikuwa mwanza. Mafuta ya 120,000/=
 
Daah Kumbe vile vya piston 3 vina consumption nzuri sana ya mafuta.
 
Sio kila gari yenye no D Itakua mpya au yenye hali nzuri ila ni kwa sababu imenunuliwa na kufika hapa nchini kipindi ambacho usajili wake kule tra upo kwenye herufi D usinunue gari kwa kigezo cha no D nunua gari kwa kigezo cha uzima wa engine na mwaka iliyotengenezwa
 
Hizi mambo zinanitoa mate mpka basi ,ndinga yaani we acha tu una2 yaani maisha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…