Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Ilo ni kweli kabisa kama asipofanya maamuzi mechi zijazo hawatofika mbali
 
Nadhani wewe na Paul Pogba ni watani. Ngoja tuwachie utani wenu. Ila kama siyo mtani wako basi utakuwa ulienda kuangalia mechi ukiwa negative tayari . Kwa hiyo ulihisi kila akishika mpira=goli. Pogba alicheza kwa kiwango cha kutosha kabisa! Kutolewa siyo hoja! Wengine nao ni wachezaji. Hata hivyo France ilicheza vizuri tokea mwanzo. Nadhani huijui Romania katika ulimwengu wa soka.
 

Hapana sikubaliani nawe. Pogba anajua angalia vizuri.
 
Ni mapema mno kusema chochote kuhusu Pogba tumuangalie na mechi ijayo na mfumo atakaotumia kocha.
 
Haya kaka tuendelee kufuatilia .
 
Yaani kwa mechi moja umepata majibu yako..
Sifa anazomiminiwa huyu mchezaji unaweza kudhani ni wa kiwango cha messi , sasa namna nilivyomfuatilia ( si jana tu ) nimegundua kwamba ni mchezaji wa kawaida sana na ukiangalia kwa makini huwa anapenda sana kucheza na jukwaa ( tabia mbaya ya kiswahili , kama wachezaji wa Faru dume ya manzese ) , kiukweli si kama anavyoongelewa .

Hana tofauti sana na Mwaikimba ; japo yeye anacheza kati .
 
Nashukuru wadau wengi wameamua kumpuuza pogba na kumshangilia Shujaa mpya Payet .
 
Kante ndo alikuwa hatari kwa leo

Ila pogba bado mzuri hata leo si kwamba alicheza vibaya

Hakufikia tuu kiwango cha sku zote

Pia samatta ifike sehem ajifunze kupiga penalt sasa

Samatta kinachomnyemelea ni kulewa sifa, namhurumia sana...ameshaanza kujiona kuwa amefika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…