Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mimi sioni haja ya Rais na Marais wastaafu watatu (Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa) kuwepo pale. Kwani ni national issue? Au kwa lipi jema alilofanya Polycarp Kadinali Pengo? Upuuzii mtupu. Watu wa dini waendelee na mambo yao ya kiroho na wanasiasa waendelee na siasa ...
......walipewa mwaliko na wakahudhuria ..hawakulazimishwa .........wangeweza pia kuacha kwenda..sasa wewe shangaa kwa nini wamehudhuria wote...!
ni vigumu kwa mtu mwenye akili kupuuza role ya kanisa katika huduma za jamii....hasa pale unapokuta karibu asilimia 40% ya huduma za jamii zinatolewa na kanisa........watanzania wengi wapo vijijini....na huko ndiko wanakotoa huduma,...hawana haja ya kufungua kwa wingi huduma hasa za afya mijini ambako mnapata private hospitals ,,,,..vijijini watu wengi wana shida na wanapewa huduma nzuri kwa kuchangia kidogo au bila malipo..........sasa kama mtu anataka kuwaona hawa kina pengo hawana maana basi na yeye apeleke huduma huko ...afikiri ni rahisi!!!!
afteral wale unaoshangaa kwa nini wamehudhuria pale ...watoto wao ndio wanaosoma....st.marian,kifungilo,st.joseph....etc.
Hii ndiyo habari nilitegemea kusikia toka kwa mtu mzima huyu lakini nadhani anaona raha tu na utukufu alokuwa nao..Kisha ukisoma hakumtaja Mwinyi ambaye niliwahi kusikia lawama zao sikutaka kuamini kama nilivyokataa kuamini ya Mwalimu na kanisa hilo...Hata hivyo yawezekana alikuwa akimpa somo MKAPA ajirudi. Just imagine MKAPA na madhambi yake dhidi ya watanzania anaenda kutembelea kaburi la Nyeyere?
MtindiowaUbongo,
Mkuu acha unazi hauna maana sisi watu wote wazima hapa..soma vizuri maelezo ya huyu kiongozi wa dini utaelewa nachozungumza.. Ni Ujinga mtupu... samahani lakini, - kwani kila unaposhukuru kuwezeshwa wewe ina maana kuna wengine hawakuwezeshwa..
Kwa nini wewe unashindwa kuamini upande wa madai ya kutowezeshwa ila unaamini na kukubali upande wa kuwezeshwa kama sii mvua ilikunyeshea!
Mimi sioni haja ya Rais na Marais wastaafu watatu (Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa) kuwepo pale. Kwani ni national issue? Au kwa lipi jema alilofanya Polycarp Kadinali Pengo? Upuuzii mtupu. Watu wa dini waendelee na mambo yao ya kiroho na wanasiasa waendelee na siasa ...
......gagnija ..inawezekana wewe sio mkatoliki ..lakini kwa kifupi kanisa katoliki huwa halitegemei wala kukubali kumtegemea muumini mmoja kwa mapato....hata kama unayo pesa ya kujenga na kulisha kanisa lote peke yako hawatakubali zaka yako peke yako...kwani kanisa ni la watu wote,mkapa anajuwa utaratibu huo...hata kama anatoa sadaka atakuwa kama waumini wengine wenye uwezo tu....
nikirudi kwenye mada ...nemebahatika kupata huduma za makadinali RUGAMBWA na PENGO....wote walikuwa na mshango mkubwa kila mmoja kwa wakati wake.
Wakati wa utawa wa cardinal pengo ...ndio wakati serikali iliruhusu kanisa kuendelea na huduma za shule na hospitali,amefanikiwa kiasi kikubwa kujenga mashule mengi .....sasa hivi hapa dar karibu kila parokia inayo shule.....na kila kitongoji kuna kanisa...amefanya juhudi kubwa sana kuunganisha nguvu za waamini,...
amefanikiwa kwa upande wa upashanaji habari kwa kuanzisha magazeti na kuimarisha redio [au uanzisha]....na kuanzisha televisheni .
mahospitali yamefunguliwa kwenye parokia nyingi.....
kwa kushirikiana na maaskofu wengine ...baada ya kuruhusiwa na serikali ndani ya miaka 15 ....wameweza kuimarisha hospitali ya rufaa ya BUGANDO,....pia wameweza kuimarisha hospitali zao zilizoenea kila wilaya nchini[ambazo nyingi ndio zinatumiwa na serikali kutoa huduma ya hospitali za wilaya kwenye maeneo ambayo bado serikali haina hospitali zenye hadhi hiyo.....
katika kipindi hicho wameweza kujenga vyuo vikuu ,iringa,mwanza,moshi,etc...vyote vikijulikana kama st.augustine... pia wameweza kujenga chuo kikuu cha teknelojia dar es salaam [st.joseph college of engineering and technology]...tunawashukuru maaskofu,mapadre,watawa,waumini na wote wenye mapenzi mema kwa mafanikio hayo makubwa...ambayo mengi yametokana na juhudi za ndani na michango ya waumini...hasa katika enzi hizi ambazo misaada kutoka ulaya kuendesha makanisa imeshakoma.....na misaada mingi kutoka rome inaelekea sehemu zenye maafa ya vita,...etc[ie congo,east europe,darfur etc]
Hii swali ndilo ungemuuliza Pengo aliyesema na kusifia, na ndio maana nikasema mzee mzima kachemsha!.. inafanya watu wajiulize maswali mengi!..Hivi unaweza kusema serikali ilimwezesha nini Pengo? Halafu sikujua kuwa ukitoa shukrani kwa mtu ina maana alikupa kitu, tena alikuteua na kukupendelea kutoka ktk umati wa wengine!
Mtindiowaubongo,
Hii swali ndilo ungemuuliza Pengo aliyesema na kusifia, na ndio maana nikasema mzee mzima kachemsha!.. inafanya watu wajiulize maswali mengi!..
ungemuuliza Pengo
maneno ambayo kila siku waislaam wanapigia kelele
Hivi unaweza kusema serikali ilimwezesha nini Pengo?
%
TUWE MACHO NA AKINA PENGO
MWISHONI NATANGAZA MASLAHI YANGU KAMA MKATOLIKI NA TENA MWANAFUNZI WA ZAMANI YA SEMINARI
KWA HILI NAMENGINE PENGO AMEKUWA AKICHEMSHA, HUWA NAJIULIZA NI KWELI ALISTAHILI KUWA KARDINALI? WAKO WNAOSEMA ALIYESTAHILI NI MTUMISHI WA MUNGU MHASHAMU ASKOFU MAYALA, HUYU SIJUI ALIDANDIA NAMNA GANI
HE CAN BORROW A LEAF FROM RT REV.PIUCE NCUBE THE THEN ARCHIBISHOP OF BULAWAYO
Marais kwani hawana maisha binafsi?
Ishu ipi ina-qualify kwako kuwa ishu ya taifa?
Kama humuheshimu Pengo, waheshimu basi wale wafuasi wake anaowaongoza, kama huwezi basi subiri na wewe zamu yako..!
Katika kuichangia maada hii ni bora watu tukaweka UDINI WETU PEMBENI KIDOGO,then tusimamie kwenye ukweli.
Mimi nadhani kuna mambo mazuri pia ambayo hawa viongozi,HASWA KIONGOZI MTAJWA HAPO JUU amewahi kuyafanya katika utawala wake.
Pia kwenda kumkumbusha mkapa KUHIJI kwenye kaburi la mwalimu NI JAMBO JEMA TU.Kuhoji kwamba KWA NINI ASIENDE YEYE PENGO,naona kama ni hoja ambayo haijaenda darasa.
ANYWAYS,NI MTIZAMO TU!
i love you all
Pengo amtaka Mkapa kwenda kuhiji Butiama
Basil Msongo
Daily News; Saturday,February 21, 2009 @19:00
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amemtuma Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwenda kuhiji alipozikwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na kufikisha shukurani zake kwa kazi aliyoifanya kujenga mazingira yaliyoliwezesha Kanisa kupata mafanikio.
Msinielewe vibaya hapa...sijui kama hawa jamaa ni members..lakini ipo Dar Lodge na ina wakubwa wengi tu. Yaliyofanyika awamu ya tatu mengi yaliwapa favor freemasons kuliko wengine wote. Tazameni vizuri na wenye jicho la kujua members watupe habari. Ila nijuavyo mimi, hawa jamaa wapo mpaka ndani ya kanisa.
Maana haiingii akilini kuona kwanini Kardinali wetu anatumia fimbo yake ya kiuchungaji kuendesha move kama hii ya kumfanya Mr Clean awe clean wakati wote tunajua ametota kwenye kashfa ambazo zinamtaka yeye binafsi atueleze yote yalivyokuwa na sio Kadinali on his behalf. Jamani hapa Kwa kardinali kuna nini?
RIP Yona Fares Maro.duty has no sweet hearts
daah!! lini hio mkuu?RIP Yona Fares Maro.