Kwanini pesa za mauzo ya wachezaji wa simba zinaingia kwenye account ya mtu binafsi?

Kwanini pesa za mauzo ya wachezaji wa simba zinaingia kwenye account ya mtu binafsi?

Mkuu nadhani wamekuelewa wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba amabo wana dukuduku kuwa hela zao zimeliwa. Kwa haya yanayotokea ningekuwa Mo ningeitisha mchango wa usajili wa wachezaji.



Dah kweli kaka tena sa hv c ndo mambo ya uwekezaji basi inatakiwa kwenye bajet ya usajili MO atoe nusu na hawa 51% watoe nusu.. halafu tuone kama zitafika hata 1B

regards
 
Mimi ni mshabiki wa yanga lkn we ni chizi.....
nani anatoa hela za usajili kuboresha club!!!??
huyo huyo ndio apokee pesa wakati wa mauzo
Sasa kama pesa zinatoka account ya mtu mwingine, mauzo ya mchezaji pesa zinaingizwa account ya mtu mwingine, wale wakaguzi wa nyaraka za kifedha wakija wanakagua nyaraka zipi?
 
Mkuu hapa tunaongelea public terms na sio personal terms, Simba SC ni public team with an investor of its 49% shares. Na share Kubwa inayobaki ipo kwetu wanachama wa timu na kwann sasa awe na nguvu kuliko sisi wanachama tulio na nguvu, Tutakuja kujutia na hii timu yetu siku moja wanasimba, Tuamkeee
Ungetaja jina la akaunti, namba ya akaunti na benki ambayo hiyo fedha imewekwa. Ingekuwa vizuri zaidi ungeonyesha na muamala wa hiyo deposit
 
Utopolo wanatakiwa kujibiwa kulingana na unyani wao. Mnaacha kuhoji za Kisinda mnahoji hela mauzo ya chama na Luis.
 
Wewe tunajua unatumwa na gabachori kuja kufukia maovu yake humu
Sasa naamin kwanini watanzania wengi hatuna ubunifu kwenye maisha.. sababu ni wavivu wa kufikir.. na kutafuta ukweli tunapenda sana kujadili umbea bila kutafuta credibility ya taarifa husika

Labda mniambie kuna taarifa ingine imetoka sijaiona, ila kama haya yote yanatokana na Mahojiano ya Magori na EFM. mie nimesikia akisema yafuatayo

aliulizwa swali la mtego na yule mtangazaji kama
ifuatavyo

Mtangazaji kauliza:-

"Mnasema Simba misimu ya nyuma imekuwa ikipata hasara. na sasa zipo taarifa mmeuza wachezaji kwa pesa nyingi mfano chama kauzwa 1.2b. na wachezaji wote waliosajiliwa na Simba had sasa manunuz inasemekana hayajazid 1.2b.. maana yake pesa ya Miq itakuwa faida au sio?"

Magori: Kajibu

"Kwanza mjue fedha yote usajili wa sasa hv haijatokana na mauzo ya wachezaj hawa maana kwenye mauzo ya wachezaj pesa zinalipwa kwa installments.. club huwa inasema italipa mara ngap na katika vipindi vingap.. kwa sasa bado simba hawajapokea kiasi chochote kile, hata installment ya kwanza kutoka club hiz.. maana kuna makubaliano.. kwa hiyo pesa ya usajili wa sasa ilishakuwepo kwenye Bajet wala sio hii..

kwa kuongezea walau Miq tulipokea ombi lake kutoka club inayomtaka miez 3 kabla so tulishajiandaa kisaikolojia kutafuta mbadala, Kwa
chama ni hivi karibuni tu ndo maombi yamekuja"

Sasa wabongo ambao hamtak kujishughulisha kuhoji kuwa taarifa za Simba fedha kuingia kwenye account binafsi zinatoka wap mnabaki kuwatukana maskin viongoz wa watu hebu jitafakarini

hivi mnajua maswala ya malipo ya fedha kimataifa baina ya nchi na nchi?.. yaan mngejua huonutaratibu ulivyo complex kuweza kuhalalisha pesa ziingizwe kwenye account binafsi ili hali mauziano yanahudiana kati club na club wala msingepiga kelele humu

Kama MO anahitaj kuchukua hizo pesa ni rahs kwake kuzichukulia zikiwa account ya Simba maana naamin yeye ni mmoja wa signatory kuliko zilipwe direct kwenye Account yake..

Hebu jitafakarini yule Sio mdhamin sasa hivi ni sehem ya Uongoz wa Simba so Ana manage account zote hana sababu ya pesa ziingie direct kwenye account yake wakat anaweza akazipangia matumiz anavyotaka zikiwa tayar kwenye account ya Simba

Hata kama mkisema some how kuwa ana makubaliano na Simba ya kujilipa hizo pesa sababu alimnunua yeye.. ni lazima ziingie kwenye acc ya Simba then ndo Simba itoe hizo pesa kwenda kwa MO kama malipo sio Zije direct kwenye account yake..

na hivi mnajua hizi pesa ni lazima ziwe na uangaliz wa BOT.. transaction kubwa kama hiyo lazima BOT wawe wanamonitor hv mnajua kuna KODI ya Serikali hapo, sasa niambie hiyo Kodi kwenye makaratasi itasomekaje ikiwa Simba hakitakuwa na record wao kupokea hayo Malipo.

Nafikir Elimu inatakiwa itolewe kwa wa wabongo sasa hv hiz club zinaendeshwaje.. bado tunaamin mfumo ni ule wa kina Manji au Azim Dewji
 
Na yule Barbra akirudi kwao atakuwa ni bilionea kwasababu ya hizi Pesa zetu za simba
 
Hakuna ugonjwa mkubwa duniani kama UMASKINI na uhusiano wa umaskini na uchawi ni mkubwa sana. Wewe kwenye kawaha kupiga domo hujui wachezaji wanasajiliwa vipi na kwa kiasi gani, hujui wanalala wapi na kwa garama gani ,hujui wanatibiwa kwa kiasi gani, hujui safari za timu nje na ndani ya nchi fedha zonatoka wapi halafu unaongea mautopolo hapa?
 
Mkuu hapa tunaongelea public terms na sio personal terms, Simba SC ni public team with an investor of its 49% shares. Na share Kubwa inayobaki ipo kwetu wanachama wa timu na kwann sasa awe na nguvu kuliko sisi wanachama tulio na nguvu, Tutakuja kujutia na hii timu yetu siku moja wanasimba, Tuamkeee
Ukubwa hela sio tantalila , "shikamoo kelele heshima pesa".
 
Mimi ni mshabiki wa yanga lkn we ni chizi.....
nani anatoa hela za usajili kuboresha club!!!??
huyo huyo ndio apokee pesa wakati wa mauzo
Watanzania wengi dhana ya biashara ni sifuri, ujuaji mwingi sheria hiyo umeipata wapi, mbona hauzi wafanyakazi kule mohamedi enterprises? Mo anamiliki simba peke yake? Hivi hujui akikuwa akisajili msimuulize 20bn yenu?
 
Unasema umepigwa umeweka nn kushinda 49%
Hiyo ndo kauli anatumia kupiga pesa pale unyamani coz simba yenyewe tu ni brand kubwa ambayo thamani yake ni zaidi hata ya Pesa aliyosema kainvest.

Ushawahi kujiuliza kwann alishindwa kuwekeza pale African lyon, pamoja na pesa aliyonayo au kule Singida United timu ya kwao na ndio alikuwa mbunge kule.

Ukipata jibu, utakuwa umetambua namna anavyo iba pesa za kutosha bila mbumbumbu kutambua hilo

Mimi ni mjumbe tu
 
Hela nyingi uwa zinajifuata zenyewe ili deal ikibumburuka zirudi. (Uwezi kuweka hela nyingi bila dhamana ya hela nyingi)
Wanasimba tuamke simba yetu inadhalilishwa na matapeli wanaojiita wawekezaji.

Kwa kuwa simba ni timu ya umma sio mali ya mtu binafsi km mwekezaji anavyojaribu kuwahadaa mashabiki mbumbumbu. Ni kwamba pesa za wachezaji wa simba waliouzwa pesa zimeyeyuka wanaocheza na hii dili ni huyu tapeli anayejiita mwekezaji pamoja na try again.

TAKUKURU mpo wapi timu yetu inachezewa na Hawa wahuni nyie mmekaa kimya? mchukueni tupumue jamani ametuibia ataifilisi klabu akimbie nje ya nchi huyu mtu ni hatari kuendelea kukaa simba.

Tunataarfa nyingi za ubadhirifu wa pesa za klabu tukianza na hii ya pesa za mauzo ya wachezaji kupotezwa na matapeli wanaojiita wawekezaji
 
Hiyo ndo kauli anatumia kupiga pesa pale unyamani coz simba yenyewe tu ni brand kubwa ambayo thamani yake ni zaidi hata ya Pesa aliyosema kainvest.

Ushawahi kujiuliza kwann alishindwa kuwekeza pale African lyon, pamoja na pesa aliyonayo au kule Singida United timu ya kwao na ndio alikuwa mbunge kule.

Ukipata jibu, utakuwa umetambua namna anavyo iba pesa za kutosha bila mbumbumbu kutambua hilo

Mimi ni mjumbe tu
Mbona kabla yake hatukuona hiyo thamani unayosema leo
 
Back
Top Bottom