Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mnyonge Mnyongeni lakini Haki yake Mpeni. Ni kweli Mimi Mwashambwa Lucas ni Mwana CCM kindakindaki ,tena mwana chama lialia wa CCM.ambaye kila mtu anafahamu hilo popote pale niwapo.
Lakini Ukweli ni Kuwa sisi wana CCM tuna Amini kabisa kuwa kama kuna mtu amewakuza vijana na wanasiasa wa upinzani hapa Nchini mpaka wakapata umaarufu na majina makubwa .basi hakuna mwenye uwezo wa kumfikia Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa upande wa vyama vya Upinzani.
Huyu mtu amekijenga CHADEMA katika mazingira na wakati ambao kila mmoja hakuwa na muda wa kuunga mkono upinzani hasa CHADEMA.amekijenga CHADEMA wakati ambao hakuna mtu au mfanyabiashara au tajiri alikuwa yupo tayari kutoa pesa zake kukisaidia chama hiki. Amekijenga CHADEMA kipindi na wakati ambao hata bendera tu zilikuwa hazipo mitaani na wala kilikuwa hakifahamiki kwa watu wala kuzungumzwa midomoni kwa watu .
Lakini kwa Moyo wa ujasiri na uvumilivu wa hali ya juu na kwa gharama kubwa ya jasho na Damu aliendelea kupambana kuhakikisha anakipeleka chama kwenye Mioyo ya watanzania na kupata uungwaji mkono wa watu. Alihakikisha kuwa anajenga chama kitakacho pata Imani na kuungwa mkono na umma wa watanzania.
Na kweli mafanikio alipata na kweli alitusumbua sana CCM Huku majimboni na kwenye kata pamoja na mitaa hasa ya mijini na kwenye miji CCM tulipata upinzani mkubwa sana . Japo tulishinda na kuendelea kutawala kwa wingi Bungeni na katika mabaraza ya Madiwani katika halmashauri mbalimbali .kwa sababu tu wananchi waliendelea kuwa na imani na sisi na kuangalia yale ambayo tulikuwa tumeyafanya katika utekelezaji wa ilani ya chama chetu cha mapinduzi.
Huyu mtu Mheshimiwa Mbowe amewapigania sana wanasiasa mbalimbali akiwepo Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa kuhakikisha anapata ubunge na hata kumteua Bungeni kuwa waziri kivuli.nafasi iliyoendelea kumpatia nafasi na kujulikana zaidi na watanzania.
Mbowe ndiye aliyempatia na kufanikisha Mheshimiwa Msigwa nafasi ya kugombea Ubunge Iringa Mjini. Na ndiye aliyefanya akashinda ubunge kwa sababu Mheshimiwa Msigwa alikuta tayari chama kimejengwa vyema na kukubalika na kuaminika kwa wananchi mbalimbali na hatimaye kumchagua yeye Mheshimiwa mchungaji Msigwa kuwa Mbunge wake.
Ni ngumu sana kuielezea safari ya mafanikio ya kisiasa ya Mheshimiwa Msigwa bila kuzungumzia Mchango chanya wa hali na mali wa Mheshimiwa Freeman Mbowe. Ni ngumu sana ndugu zangu. Hata katika uchaguzi wa kanda ya Nyasa kulifanyika kazi kubwa sana ya kuhakikisha Mheshimiwa Msigwa anapita na anashinda wakati ule wa awamu ya kwanza.
Ndio maana majina yaliyokuwa pia yanapewa nafasi ya kushinda na kuleta ushindani mkali kama vile Ole Sosopi aliyekuwa makamu mwenyekiti wa BAVICHA yaliwekwa kando. Nasema haya kwa sababu mimi nilikuwa nafuatilia vyema na kwa ukaribu sana uchaguzi ule na kujua kila kitu kilichokuwa kinaendelea katika kanda hii ya Nyasa kwa hawa wapinzani wetu .
Sasa nashangaa ni kwanini Mheshimiwa Msigwa Anamchukia sana Mheshimiwa Freeman Mbowe kuliko hata shetani. Anamchukia Mheshimiwa Mbowe kuliko hata Lissu ambaye amekuwa mwanasiasa wa Hovyo na wala hakuwa na mchango wala msaada wowote ule katika kushinda kwake ubunge . Maana naye ni wakuja tu CHADEMA na aliikuta CHADEMA ikiwa imejengwa na ina wabunge Bungeni.
Mimi nashangaa kwanini Mchungaji anamchukia Mbowe na kumuunga mkono Lissu. Sasa najiuliza je ataendelea kumuunga mkono lissu na kurejea CHADEMA baada ya lissu kuwa Mwenyekiti? Maana inaonyesha adui yake mkubwa alikuwa ni Mbowe tu. Je ataendelea kuishambulia na kuikosoa CHADEMA ya Lissu rafiki yake au atakaa kimya?
Je anasema nini juu ya lugha chafu na za kibaguzi ambazo zimekuwa zikitolewa na Lissu kumshambulia , kumdhalilisha na kumtweza Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan?
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.