wakuu tujuzane hapa kwa nini pikipiki au baiskeli zina uwezo mkubwa wa kutembea kwa matairi mawili tu tena wakati huo inakua imebeba watu wa 2 mpaka wa 3 na haianguki,kuna physics au mathematics gani imekua applied hapa? na kwa nini gari lisingekua linatembea kwa matairi mawili tu kama pikipiki? jamani wataalam tujuzeni hapa ni uchawi gani umetumika.
Habari,
Jinsi hasa ambavyo baiskeli huweza kujiwianisha 'usimamivu-katika- mwendo' wa namna yake, kisayansi bado hakuna maelezo rahisi yenye kukidhi kudadavua hasa
finomena hii.
Kuna mawazo mengi mwenyekujifikirisha anaweza kuanza kujiuliza kiuchunguzi na kuleta fikra mbalimbali juu ya jambo hili.
Moja ya fikra hizi za kimaumbo na mwendo ni sifa za
kijiroskopia. [1]
Vitu vyote vinavyojizungurusha kwa kasi huzalisha namna ya ukatikati ama kitovu cha kazi. Ukati huu kuwa unaelekea kwenye kukadirisha sifa mbili ; ya kwanza ni kuzaa 'usahani' kulingana na mwelekeo wa mzunguruko wenyewe; na pili kusababisha 'mhimili' wa kazi--huu ndiyo msingi wa jiroskopia.
Wenyekuchunguza kutoka namna hii ya asili wamechunguza na kubaina hata hivyo hili si kamili hasa kwenye kufumbua siri ya baiskeli ifanyavyokazi.
Fikra nyingine imekuwa ikidhaniwa ni gurudumu la mbele kuwa ndiyo msingi wa muwianisho; lakini hii pamoja na ile ya kudhani uskani kuwa umenyooka kiusawa ndiyo sababu vyote vinathibitishika sivyo. [2]
Zangu:
Kuna vitu tunaweza 'kuvijua' kwa kuona na tathmini; lakini vipo ambavyo mbinu hii haina msaada.
Badala ya kuona tu, tunaweza kutumia modeli za kijiometria kuweza kubaini mshahibiano wa tabia--maumbo, nishati, sifa na tabia.
Ninatumia sura ya
usahani,
umbo pia na
mzunguruko; kujaribu kukadirisha kinachoweza kudhaniwa ni uwepo wa
uvuto,
chembe na
mwendo. Nikifikia pazuri nitashiriki lugha, ujuzi na ufundi wa kuona pasipo kuona ila kwa kupitia ushahidi wa kile kisichoonwa--dhahiri isiyodhahirishika ila kwa hadhi na tabia ya jambo.
====
Rejea
1.
Gyroscope - Wikipedia, the free encyclopedia
2.
www.youtube.com/watch?v=YHCounW3VO0
http://www.google.com/url?sa=t&rct=...DotJAA7wE6ZO_OQd30sCZnw&bvm=bv.89381419,d.d24