Kwanini polisi imekuwa na kigugumizi kuhusu hili swala la huyu binti aliyefanyiwa ukatili na wanajeshi wale.

Kwanini polisi imekuwa na kigugumizi kuhusu hili swala la huyu binti aliyefanyiwa ukatili na wanajeshi wale.

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Hilo tukio lina zaidi ya wiki sasa ila sijasikia polisi ikitoa taarifa za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao zaidi nimesikia mtu mmoja aliyeshikiliwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uzushi juu ya binti aliyefanyiwa ukatili huo.

hii kitu haijengi taswira nzuri kwa vyombo vyetu vya usalama na ulinzi nchini.

Huko nyuma pia iliwahi kutolewa shutuma kwa majeshi yetu ya ulinzi wanaolinda amani chini ya munesco wanawabaka wanawake huko congo.

Ni vema serikali ijihepushe na mazingira ya kuwabeba watuhumiwa hawa maana inaharibu taswira ya jeshi na ya nchi kwa ujumla.
 
Ila kama kweli Jeshi la polisi lilitaka kuficha ukweli ni aibu na fedheha sana kwao.
 
Nadhani labda baadhi ya watuhumiwa ni askari maana kwenye video Kuna sehemu wale wahuni wanamuamrisha Binti amwombe msamaha afande
 
Inasikitisha sana ,mbona Komandoo aliwekwa UBAONI? Why wabakaji ichukuje muda mrefu? protokali gani hizo?

 
Back
Top Bottom