Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

We mwenyewe umeshindwa kuificha picha yake .... kupitia uzi wako bado unazidi kumchoresha Mzee wa watu
 
Uchunguzi ufanyike lakini busara pia itumike. Taarifa kuwa alifia hotelini ibaki kuwa ni mali ya Polisi tu kwa matumizi yao na sio kutoa kwenye media.

Kwanini wataje jina lake?
Kwahio unatupangia jinsi ya kutekeleza majukumu yetu? Kila mtu ni sawa mbele ya sheria, awe mzee au kijana akifanya mambo ya hovyo ataripotiwa na ndio utaratibu.

Mbona Kapuya alipooa kabinti ka miaka 25 mlitangaziwa wala hakukuwa na shida. Amekufa mstaafu wa enzi ya mkapa juzi ambaye pia alioa kabinti kadogo ile ni sawa ila hii mnataka tufiche?
 
Kikubwa wazee wajiheshimu. Miaka 80 unaacha mke ndani unaenda kutafuta nini hotelini na mwanamke anaeweza kuwa kitukuu chako? Fedheha za namna hii zinatafutwa kwa nguvu. Marehemu apumzike mahala anapostahili na waliobaki wajitafakari. Tulieni mlee familia zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…