Kwanini Polisi wanakwepa kutumia neno "Kuteka" katika taarifa yao wanatumia "Kukamata"?

Kwanini Polisi wanakwepa kutumia neno "Kuteka" katika taarifa yao wanatumia "Kukamata"?

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
520
Reaction score
2,930
Yaani Polisi Tanzania wanasema wanaanza uchunguzi wa video inayoonesha watu wakijaribu "kumkamata " na "kujaribu kumuingiza kwenye gari".

Polisi kwanini wanatumia neno kukamata? Kwanini neno kuteka wanalikwepa? Mfano hiyo taarifa wangeiandika kwa kingereza, wasingethubutu kuandika" Some people who attempted to arrest Mr. Deogratius Tarimo" wasingethubutu kuandika hivyo umma na kila mtu angeshangaa sababu hao wamesema sio Police, na huo sio utaratibu wa kukamata mtu iwe ni Arrest by Police or Arrest by Private Person huo sio utaratibu.

Kwa kingereza wangeandika " ..... Some people who attempted to kidnap /abduct Mr. Deogratius Tarimo ....". Na hii ndiyo pia ilipaswa kuandikwa hata katika hii taarifa Yao. ".... Watu wakijaribu Kumteka ndug. Deogratius... ". Sababu tukio lote hilo sio ukamataji huo ni utekaji wa dhahiri, shahiri. Sasa kwanini tutekenye na kubana ulimi kwa kuita ukamataji? Kukamata? Kukamata?

Watu wakija bila utaratibu kukukamata usikubali, sababu Sheria imeweka utaratibu. Sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act ) kifungu cha 23 kinataka anayekamatwa ambiwe sababu ya kukamatwa kwake, wanaomkamata wajitambulishe kwa vitambulisho halali, pia anayekamatwa ana haki ya kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa kuhusu kukamatwa kwake na wapi anapelekwa.

Pia soma: Polisi watoa tamko tukio la jaribio la utekaji Kiluvya, wasema uchunguzi umeanza toka aliporipoti Novemba 11, 2024

Katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Dastur, A.L . R421. Mtuhumiwa aligoma kukamatwa kwa kutoambiwa sababu ya kukamatwa kwake, pia waliomkamata kutojitambulisha kwa vitambulisho vyao halali vya kazi. Mtuhumiwa alichomoa kisu akamchoma mtu mmoja kati ya watu 3 (Ambao wote baadaye walitambulika kama Askari).

Mahakama baada ya kujiridhisha na maelezo ya Mtuhumiwa ilisema Mtuhumiwa alikuwa na haki ya kuelezwa sababu na hao Askari walipaswa kumueleza sababu ya kukamatwa kwake na kujitambulisha.

Sababu unavyomkamata mtu kihuni anaweza kufanya lolote ili kujilinda akichoma mtu kisu au akipiga mtu jiwe la kichwa nayo kesi kamchoma Polisi kisu akiwa kwenye majukumu yake kwanini usingejitambulisha kwa utaratibu tangu awali. Tena sio kusema wewe ni Polisi, onesha kitambulisho, lakini kwanini uje ukamate mtu kwa gari binafsi? Lakini kwanini uje ukamate mtu bila Uniform?
 

Attachments

  • Screenshot_20241113-085828.png
    Screenshot_20241113-085828.png
    435 KB · Views: 6
  • 20241113_090236.jpg
    20241113_090236.jpg
    234.1 KB · Views: 5
Hakuna tatizo la utekaji, ni kama wakati wa korona kulikuwa na changamoto ya upumuaji🐼
 
Ww nawe polisi wanakamata ,awateki,sema Kuna watu wakikamatwa wanasema wametekwa Ili wapata huruma ya Wananchi
 
Ww nawe polisi wanakamata ,awateki,sema Kuna watu wakikamatwa wanasema wametekwa Ili wapata huruma ya Wananchi
Wakikamata mtu wanatakiwa wampeleke wapi?Inakuwaje "wamkamate" mtu halafu aokotwe jalalani ameumizwa vibaya sana, amekufa na kumwagiwa tindikali au kutoonekana kabisa?
 
Back
Top Bottom